Wauguzi wagoma wakidai marupurupu yao Kenya

wahudumu wamegoma Nairobi
Image captionWahudumu waliomiminika katika Kaunti ya Nairobi wakidai malipo bora

Wagonjwa nchini Kenya wameanza kujawa na hofu baada ya wauguzi kuapa kuendelea na mpango wao wa kutekeleza mgomo au kuanzia leo Jumatatu.

Katibu mkuu wa Muungano wa wauguzi nchini kenya Seth Panyako alisema siku ya Jumamosi kuwa iwapo mahitaji yao ya kurudi kazini hayataangaziwa, basi hawatakuwa na chaguo jingine bali kufanya mgomo isipokuwa wauguzi katika kaunti ya Mombasa, Migori na Machakos ambao wamelipwa marupurupu yao kulingana na mkataba huo.

Amesema kuwa majadiliano kati ya serikali kuu na zile za kaunti yalioafikiwa mnamo tarehe mbili mwezi Novemba 2017 kwa huduma na marupurupu hayajaafikiwa.

Serikali ilikuwa na siku ya Jumapili pekee kuzuia mgomo huo.

Kaunti zitakazoathirika

Amesema kuwa kaunti ambazo wauguzi wake hawataripoti kazini ni Pokot Magharibi, Kisumu, Nairobi, Kisii, Taita-Taveta, Nyandarua, Trans Nzoia, Elgeyo Marakwet, Wajir, Nyeri na Kitui, hadi pale makubaliano hayo ya Novemba 2017 yatimizwe.

Matamshi yake yanajiri huku waziri wa leba Ukur Yatani akiwataka wauguzi kusitisha mgomo huo.

Mgomo wa wahudumu katika Kaunti ya Nairobi

Waziri huyo alisema kuwa ameteua kamati ambayo itaangazia maswala yote na kuandika ripoti katika kipindi cha siku 30.

Amesema kuwa swala tata ni kutotekelezwa kwa makubaliano ya kurudi kazini ambayo yaliafikiwa kati ya wahusika na kushuhudiwa na maafisa muhimu wa wauguzi, baraza la magavana na wizara ya Afya.

Akijibu hilo mwenyekiti wa baraza la magavana nchini kenya Wycliffe Oparanya aliihakikishia wizara , wauguzi na raia kuhusu juhudi zao za kushirikiana na kamati ilioundwa ili kutatua mgogoro huo.

Ajenda nne kuu za rais

Lakini akizungumza, Seth Panyako alisema kwamba baada ya kutoa ilani ya kufanyika kwa mgomo huo mwezi Novemba mwaka jana , wizara ilinyamaza na kuamua kubuni jopo la maridhiano siku ya Ijumaa.

”Tunaona kwamba huu ni mchezo unaofanywa na wizara kwa lengo la kukandamiza ajenda nne kuu za rais Uhuru Kenyatta . Kama Muungano wa wauguzi hatutakubali hilo”, aliongezea panyako.

Muungano huo umesitisha mgomo huo katika kaunti tatu.

Hatahivyo kaunti nyegine 18 bado hazijapokea ilani ya kurudi kazini baada ya kuonyesha kuwa ziko tayari kuafikia makubaliano hayo ya kurudi kazini.

Kaunti hizo ni Mandera, Tharaka Nithi na Vihiga huku zile 18 zikiwa Baringo, Laikipia, Meru, Bungoma, Nyamira, Isiolo, Kajiado, Kakamega, Kericho, Kilifi, Lamu, Nandi, Narok, Makueni, Turkana, Uasin Gishu, Bomet na Tana River.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *