wanda imesisitiza kuwa haijafunga mpaka baina yake na Uganda

Waziri wa mambo ya nje wa Rwanda, Richard Sezibera amekanusha ripoti ya kwamba taifa hilo limefunga mpaka kati yake na Uganda.

Sezibera alisema hayo katika mkutano wake na waandishi wa habari katika makao makuu ya wizara ya mambo ya nje mjini Kigali mapema leo Jumanne.

”Shughuli ya ujenzi wa barabara katika mji wa mpakani wa Gatuna umefanya magari kuelekezwa katika mpaka wa Kagitumba,”

Waziri huyo alinukuliwa katika Twitter yake rasmi ya kazi akiongeza kuwa ujenzi huo utakamilika mwezi Mei mwaka..

Kuhusiana na uhusianao wamataifa hayo mawili alisema: “Uhusiano wetu kwa sasa sio mzuri vile lakini tunashughulikia hilo”

Bwana Sezibera aliongeza kuwa Rwanda inaendelea na majadiliano na majirani zake kuhusiana na masuala kadhaa ikiwa ni pamoja na kuzuiliwa kiharamu kwa raia wake nchini Uganda.

Image captionUjenzi wa barabara katika mpaka wa Gatuna upande wa Rwanda

Alisema kuwa suala la kuunga mkono makundi yaliyojihami yanayopinga Rwanda pia ni baadhi ya mambo yanayojadiliwa.

Wizari Sezibera pia amekanusha ripoti ya vyombo vya habari kuwa zinazodai kuwa taifa hilo limepeleka vikosi maalum vya kijeshi katika mpaka wake na Uganda tangu ilipochukua hatua ya kuifunga.

“Hakuna wanajeshi waliyopelekwa mpakani. Hakuna ubaya wowote ikiwa Rwanda imeamua kuimarisha usalama wa mpaka wake japo hilo halijafanyika.”, alisema.

”Nataka kuwahakikishia wanyarwanda kuwa wako salama!”

Huku hayo yakijiri Uganda imeishutumu Rwanda kwa kufunga mipaka baina ya nchi hizo mbili.

Alhamisi iliyopita mamlaka ya mapato ya Rwanda iliamrisha maroli ya mizigo kutotumia tena mpaka wa Gatuna kwa madai ya shughuli za ujenzi wa kituo kimoja cha mpakani ‘one stop border’ baina yake na Uganda.

Mkwamo wa shughuli katika mpaka wa Rwanda Uganda.

Eneo hilo lina umuhimu mkubwa kibiashara kieneo.

Ni eneo ambalo huruhusu kupita kwa bidhaa kutoka mji mkuu wa Uganda Kampala, au Mombasa pwani ya Kenya.

Wakaazi hapo wanasema ni kama ‘ghala kwa biashara kutoka maeneo hayo’.

Akizungumza na BBC, Diwani Abel Bizimana katika eneo la Kisoro anaeleza kwamba, ‘Hali haijabadilika. Tunaathirika kama viongozi wa kieneo, kama jumuiya ya wafanyabiashara na wateja pia tunaowahudumia.’

Abel ameeleza kuwa maisha yamebadilika pakubwa.

Kutokana na matatizo ya kibiashara na udhibiti wa watu kutoka na kuingia katika eneo hilo, watu ambao kawaida huja kupokea bidhaa kutoka mjini na wilaya ya Kisoro sasa inaarifiwa hawaji tena, wakiwemo hata waendesha boda boda ambao pia wamesitisha shughuli zao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *