Wakenya wajizolea faida kutokana na uuzaji wa tunda la parachichi

Tunda la parachichi limesifika kutokana na faida yake kwa afya
Tunda la parachichi limesifika kutokana na faida yake kwa afya

Parachichi kwa tosti ya mkate, saladi au juisi? Kuna njia nyingi za kula tunda hili maarufu kote duniani huku wakenya wakijizolea faida zinazotokana na uuzaji wake.

Katika mgahawa wa At Le Grenier iliyopo mtaa wa kifahari wa Riverside jijini Nairobi, baadhi ya wakenya na na raia wa kigeniwanafurahia “toast à l’avocat” yaani tosti ya makate kwa parachchi.

Mmililiki wa mgahawa huo Yan Welffens anasema “Umuhimu wake kwa afya umeangaziwa katika kila jarida na mitandao ya kijamii”

Kwanini balozi wa EU Tanzania ameitwa nyumbani?

Abdul Nondo ashinda kesi ya ‘kujiteka’

Trump anafaa kuwa na hofu uchaguzi Marekani?

“Mkwe wangu anakula tunda la parachchi kila siku – haondoki nyumbani bila kula bakuli lake la tunda hili, kwahivyo, najaribu kumuigiza nione kama na mimi nitazeeka [vizuri] kama yeye.”

Ongezeko la ulaji wa tunda hili limeongeza mahitaji yake katika miaka ya hivi karibuni.

Peter Kariuki akikagua majani ya mmea wa parachichi katika shamba lake
Image captionMkulima wa Kenya Peter Kariuki anasema parachichi zina faida na gharama ya ukuzaji wake bei nafuu

Kwa kujibu wa kituo kinacho simamia biashara ya tundo la parachichi katika mataifa yanayoendelea, uuzaji wa tunda hilo katika soko la ulaya iliongezeka karibu mara tatu kati ya mwaka 2013 na 2017.

Faida inayotokana na ongezeko hilo la ununuzi iliwafikia maelfu ya wafanyibiasha wa nyanda za juu za Kenya ambao maisha yao yamebadilika pakubwa.

Bei imeongezeka mara mbili

Peter Kariuki mkulima ambaye amemaliza kuuza parachichi zake msimu huu katika eneo la kati nchini Kenya, alivuna jumla ya matunda 400,000 katika shamba lake.

Serikali ya Tanzania ‘yamruka’ Makonda

“Umekua msimu mzuri sana- bei ya tunda moja iliongezeka karibu mara mbili ukilinganisha na ile ya mwaka jana,”

A graph showing the growth in Kenya's avocado exports since 2011

Bwana Kariuki pia anasema mmea wa parachichi pia humea mwituni na kwamba hana haja ya kunyunyuzia dawa ya kuzuia wadudu au kutumia mbolea.

Alikuwa mkulima wa kwanza katika eneo la kati mwa Kenya kukuza tunda la parachichi zaidi ya miaka 30 iliyopita.

“Nilikuwa nikifanya kazi kama ajenti wa biashara katika uwanja wa ndege miaka ya 1980, na ni hapo ndipo nilijifunza kuhusu uuzaji waparachichi nje ya nchi.”

Dada watatu wa Nigeria washika mimba wakati mmoja

Bahatialiyokuwa nayo ni kuwa baba yake mzazi alikuwa nafanya kazi katika Taasisi ya utafiti wa kilimo karibu na nyumbani kwao.

Alinunua miche yake ya kwanza katika taasisi hiyo na kupanda shambani kwake.

parachichiHaki miliki ya pichaBOSTON GLOBE/GETTY IMAGES

Vitu tano muhimu kuhusu tunda la parachichi:

  • Ni jamii ya matunda kama vile ndimu, zabibu na tomato
  • Ina viwango vya juu vya protini kuliko aina nyingie za matunda
  • Wataalamu wa lishe bora wanasema tunda la parachichi linamsaidia mtu kudhibiti kiwango cha mafuta mabaya mwilini.
  • Mexico ndio taifa linalokuza parachichi kwa wingi zaidi kuliko mataifa mengine duniani na linakadiriwa kuchangia 45% ya soko la kimataifa.
  • Barani Afrika Kenya ndio mkuzaji mkubwa wa tunda la parachichi.
  • Marekani inaagiza kwa wingi tunda hilo duniani ilkifuatiwa na Uholanzi.

Miti 200 ya tunda a parachichi katika shamba lake sasa imekomaa, na inampatia pato la karibu dola 20,000. Na hahitaji kufanyia kazi nyingi miti hiyo

“Tunapunguza matawi ya miti hii mara moja kwa mwaka.”

Anawaajiri watu wa kuvuna matunda wkati zinapokuwa tayari kwa ajili ya matayarisho ya kuuza nje ya nchi.

Wakulima wachache kama Kariuki wanauza nyingi ya matunda ya parachichi inayouzwa nje ya Kenya

Mfanyibiashara Lucy Njeri anasema soko la parachichi mwaka huu imekuwa mbaya
Image captionMfanyibiashara Lucy Njeri anasema soko la parachichi mwaka huu imekuwa mbaya

Watu wengi wanaendelea kung’oa miti ya kahawa na michai na badala yake wanapanda miti ya parachichi.

Msimu wa mvua nyingi iliashiria mavuno mazuri kwa mkulima kama Kariuki.

Lakini kwa mfanyibiashara kama Lucy Njeri – hakufurahia. Anasema

“Haikua msimu mzuri wa mauzo,” mfanyibiashara huyo wa miaka 30,ambaye anaendesha biashara ya chakula ya Saipei na mume wake.

Mbinu ya asili yadhibiti umakini wa wanafunzi Zanzibar

Bi Njeri anasema aliuza nje ya nchi zaidi ya tani 1,200 ya matunda ya parachichi msimu huu hususan bara Ulaya.

“Uuzaji katika soko hilo umepungua hali ambayo imeathiri bei ya ya zao hilo”

Anasema hali hiyo ilichangiwa na ukuzaji mwingi zaidi wa zao hio mwaka huu

Bei ya tunda la Parachichi katika soko ya kimataifa imeongezeka katika miaka ya hivi karibuni
Image captionBei ya tunda la Parachichi katika soko ya kimataifa imeongezeka katika miaka ya hivi karibuni

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *