Waandishi wa habari wawili wa CPJ waliokamatwa nchini Tanzania wameachiwa huru

Kushoto ni Muthoki Mumo, na wa kulia ni Angela QuintalHaki miliki ya pichaCPJ
Image captionKushoto ni Muthoki Mumo, na wa kulia ni Angela Quintal

Mamlaka nchini Tanzania zimewaachia huru waakilishi wawili wa kamati ya kimataifa ya kuwalinda waandishi wa habari CPJ, Muthoki Mumo na Angela Quintal, ambao mamlaka hizo zilikiwa zimewazulia eneo lisilojulilikana.

Idara ya kimataifa wa uhusiano na ushirikiano nchini Afrika Kusini (DIRCO) ilisema waandishi hao sasa wamerudi kwenye hoteli yao.

“Balozi wa Afrika Kusini Bw Thami Mseleku amekutana nao na kuzungumzia kile kilichotokea. Kisha atazungumza na mamlaka za Tanzania. Msemaji wa DIRCO Bw Ndivhuwo Mabaya, alizungumza na Bi Quintal leo asubuhi,” Wizara ya mashauri ya nchi za kigeni ya Afrika Kusini ilisema kwenye mtandao wa Twitter.

Chama cha wahariri wa habari nchini Kenya kimelaani kukamatwa kwa waandishi hao wa habari na kutoa wito kwa serikali ya Tanzania kuwaruhusu kukamilisha kazi yao.

Maafisa waliojitambulisha kama wafanyakazi wa idara ya uhamiaji nchini Tanzania waliwakamata Quintal na Mumo kwenye hoteli yao mjini Dar es Salaam, kwa mujibu wa CPJ.

Maafisa hao walichukua bidhaa za wawili na hawakurudisha pasi zao za usafiri wakati waliombwa.

Quintal na Mumo kisha wakatolewa hotelini na kupelekwa eneo ambalo halikujulikana, Mara baada ya kukamatwa, ujumbe wa twitter ulitumwa kutoka akaunti ya Quintal, ukisema “Mungu ni mkuu tumeachiliwa na tunarudi hotelini,” na kuzua hofu kuwa mtu fulani alitumia simu zake.

“Ujumbe wa @angelaquintal haukutumwa naye,” aliandika mpwa wake Quintal, Genevieve Quintal, ambaye pia ni mwandishi wa habari. “Hii inaonyesha kuwa kuwa kuna mtu anatumia simu yake.”

Akaunti za Twitter za Quintal na Mumo zimezimwa tangu wakati huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *