Tetesi za Soka Ulaya Jumapili 21.10.2018: Hazard, Sterling, Ake, Rooney, Malcom, Barella

Eden Hazard

Chelsea wanataka kumfanya Eden Hazard kuwa mchezaji anayelipwa kitita cha juu zaidi katika Ligi ya Premier kwa kumpa ofa ya mshahara wa dola 350.000 kwa wiki. (Express)

Mwanamfalme wa Saudi Arabia Prince Mohammed bin Salman anatarajiwa kukutana na wamiliki wa Manchester United familia ya Glazer wiki chache zinazokuja, kuwasilisha ofa ya dola bilioni 4 kuinunua klabu hiyo. (Mirror)

Manchester City wanakataa kubadilisha msimamo wao kuhusu masharti ya mkataba wake na Raheen Sterling, na kuongeza hofu kuwa mchezaji huyo wa miaka 23 wa England anaweza kuondoka msimu ujao. (Mirror)

Raheen SterlingHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionRaheen Sterling

Real Madrid wako tayari kumpa ofa Sterling mwezi Januari. (Express)

Manchester City wanatathmini ofa ya pauni milioni 40 kwa mchezaji wa Bournemouth Nathan Ake mwezi Januari. Mchezaji huyo mwenye miaka 23 wa Uholanzi pia amehusishwa na Manchester United na Tottenham. (Sun)

Tottenham wanapanga kumuendea kiungo wa kati wa Blackburn Bradley Dack, 24, kutokana na ripoti nzuri za majenti. (Express)

Meneja Manchester United Jose Mourinho anataka kumleta mlinzi wa Fiorentina Nikola Milenkovic. Mchezaji huyo wa kimataifa raia wa Serbia anawekewa thamani ya dola milioni 40 na klabu ya Italia kwa kuwa wanajua anawindwa na United, Tottenham, Chelsea, Arsenal na Juventus. (Star)

Jose MourinhoHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionJose Mourinho

Arsenal wanataka kumsaini wing’a wa Barcelona raia wa Brazil Malcom, 21, mwezi Januari kwa mkopo. (Star)

Meneja wa Arsenal Unai Emery amekiri kuwa alikuwa anataka kumsaini mshambuliaji wa sasa wa Arsenal na Ufaransa Alexandre Lacazette mwanzo wa msimu wa mwaka 2016 – 2017 wakati akiwa meneja wa Paris St-Germain. (Mirror)

Kiungo wa kati wa Cagliari mwenye miaka 21 raia wa Italia Nicolo Barella, ambaye analengwa na Arsenal na Liverpool hatajiunga na klabu nyingine kwa sababu za pesa bali kwa sababu za ndoto. (Calciomercato)

Nicolo BarellaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionNicolo Barella

Meneja Mauricio Pochettino anasema Tottenham inataka kuwasaini wachezaji Januari, baada ya kutomsaini mchezaji yeyote wakati wa msimu wa joto. (Enfield Independent)

Mlinzi wa Real Madrid Marcelo, 30, anasema wachwzaji wako chini ya shinikizo kutoka kwa meneja Julen Lopetegui baada ya kupata pigo lingine siku ya Jumamosi (Marca)

Bora Zaidi Kutoka Jumamosi

Mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho anaamini kwamba Hazard ataisaidia Chelsea kushinda taji la ligi ya Uingereza msimu huu. (Daily Star)

Mshambuliaji wa man United Anthony Martial ,22, ambaye hana kandarasi na klabu hiyo mwisho wa msimu huu analenga kuondoka katika klabu hiyo. (Mirror)

Anthony MartialHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionAnthony Martial

Mchezaji anayelengwa na Tottenham na Juventus Anthony Martial amekataa ofa kadhaa za kuandikisha kandarasi mpya na United. (RMC Sport via Calciomercato)

Nahodha wa klabu ya Juventus Giorgio Chiellini, 34, amemwambia kiungo wa kati wa Manchester United Paul Pogba, 25, kwamba anakaribishwa tena katika klabu hiyo ya Itali.. (Mirror)

Chelsea itajaribu kumsaini mshambuliaji mpya mnamo mwezi Januari baada ya kupoteza subira na mshambuliaji Alvaro Morata, 25. (Sun)

Pep GuardiolaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionPep Guardiola

Mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola amesema kuwa mchezaji wa Borussia Dortmund na Uingereza kinda Jadon Sancho huenda asirejee katika klabu hiyo katika kipindi chake cha ukufunzi. (Manchester Evening News)

Manchester City imeanza mazungumzo na winga Leroy Sane, 22, kuhusu kumuongezea kandarasi yake , licha ya kwamba raia huyo wa Ujerumani ana takriban miaka miwili na nusu iliosalia katika kandarasi (Telegraph

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *