Tetesi za soka Ulaya Jumanne 05.02.2019: Insigne, Pogba, Rashford, Hudson-Odoi

Lorenzo InsigneHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Liverpool imewasilisha ombi la takriban Euro milioni 70 kwa mshambulaiji wa Napoli Lorenzo Insigne, mwenye umri wa miaka 27. (La Repubblica kupitia Sport Witness)

Bayern Munich itarudi na ombi la £ milioni 35 kwa winga wa Chelsea Callum Hudson-Odoi, mwenye umri wa miaka 18, katika msimu wa joto baada ya kushindwa kumsajili mchezaji huyo wa timu ya England ya wachezaji wa chini ya miaka 19 mwezi Januari. (Mail)

Mshambuliaji wa Manchester United Marcus Rashford, mwenye umri wa miaka 21, anafanya mazungumzo kuhusu mkataba mpya katika klabu hiyo ambayo huenda yakaongeza mshahara wake kwa mara mbili hadi zaidi ya £150,000 kwa wiki. (Telegraph)

Mchezaji wa kiungo cha kati wa United Paul Pogba aliwahi kutafakari kuondoka katika klabu chini ya mkufunzi wa zamani Jose Mourinho, kwa mujibu wa kakake, Mathias. (Telefoot kupitia Mirror)

Mshambuliaji wa Tottenham Vincent Janssen, mwenye umri wa 24, ameambiwa na meneja Mauricio Pochettino kwamba atajumuishwa katika kikosi cha timu hiyo katika ligi kuu ya England, licha ya kutojumuishwa katika timu ya Spurs tangu Agosti 2017. (Evening Standard)

PogbaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Meneja wa Arsenal, Unai Emery atakuwa na £40 milioni pekee kutumia msimu wa joto, baada ya kushindwa kusajili mchezaji kwa mkataba wa kudumu mwezi Januari. (Mirror)

Emery anataka kusaini angalau wachezaji watatu wapya msimu wa joto, akiwemo beki wa kushoto. (Mail)

Gunners wamekuwa wakimsaka beki wa kati wa Red Bull Leipzig raia wa Ufaransa Ibrahima Konate, mwenye umri wa miaka 19. (Bild – kupitia ESPN)

Mkataba wa mkopo wa mchezaji wa kiungo cha mbele wa Fulham Andre Schurrle kutoka Borussia Dortmund utamalizika msimu wa joto – mwaka mmoja mapema kuliko ilivyopangwa – iwapo timu hiyo ya Cottagers itashushwa daraja kutoka ligi kuu ya England. (Kicker – Kijerumani)

Hertha Berlin inataka kuendelea kuwa na mchezaji wa kiungo cha kati wa Liverpool Marko Grujic, mwenye umri wa miaka 22, kwa mkopo kupita hata baada ya mwisho wa msimu. (Liverpool Echo)

Mkataba wa mkopo wa Andre Schurrle kutoka Borussia Dortmund utamalizika msimu wa jotoHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMkataba wa mkopo wa Andre Schurrle kutoka Borussia Dortmund utamalizika msimu wa joto

Barcelona inataka kumsajili mchezaji wa Ajax mwenye umri wa miaka 19 Matthijs de Ligt katika msimu wa joto na itabidi ilipe euro milioni 75. (Mundo Deportivo Kihispania)

Cristiano Ronaldo amemeuita aliyekuwa mchezaji mwenzake wa Real Madrid James Rodriguez, ambaye kwa sasa anacheza kwa mkopo Bayern Munich, katika jitihada za kumshawishi mchezaji huyo raia wa Colombia mwenye miaka 27, ajumuike naye Juventus. (Marca)

Bora kutoka Jumatatu

Mario BaloteliHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Mshambuliaji wa Marseille Mario Balotelli, 28, anasema kuwa anataka kumaliza kazi yake ya kusakata soka kwa kuichezea timu yake ya nyumbani ya Brescia nchini Itali. (goal)

Mkufunzi wa Everton Marco Silva anasema kuwa anajua kwamba yuko chini ya shinikizo baada ya kikosi chake kushindwa na klabu ya Wolves na kusalia katika nafasi ya tisa katika jedwali la ligi ya Uingereza. (mirror)

Klabu ya Leeds inataka kumnunua winga wake wa zamani Aaron lennon, 31, kurudi katika klabu hiyo kwa kupitia kumsajili kutoka klabu ya Burnley mwisho wa msimu huu. (sun)

Ibrahim DiazHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Mshambuliaji wa Stoke City Bojan Krkic ,28, huenda akahamia katika klabu ya ligi ya Marekani New England Revolution ambayo imejitolea kumlipa mara mbili marupurupu yake huku dirisha la uhamisho nchini Marekani likiendelea kuwa wazi hadi tarehe mosi mwezi Mei. (sun)

Real Madrid haitamuuza kwa mkopo mwisho wa msimu huu kiungo wa kati wa Uhispania mwenye umri wa miaka 19 kinda Ibrahim Diaz ambaye walimsajili kutoka Manchester City. (AS)

Aaron lenon

Shirikisho la soka la Uingereza FA linataka kuanzisha refa wa kwanza atakayesimamia mechi za ligi ya wanawake ya.. (telegraph).

Kiungo wa kati wa Newcastle Sean Longstaff, 21, huenda akaitwa na timu ya Uingereza ilio na wachezaji wasiozidi umri wa miaka 21 baada ya kushirikishwa katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo.(Chronicle)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *