Rais wa Sudan awekwa katika wakati mgumu na wanaompinga

Waandanmanaji nchini Sudan, wakiandamana kuipinga serikali
Waandanmanaji nchini Sudan, wakiandamana kuipinga serikali

Mamia ya watu wameandamanamashariki mwa mji wa Sudan wa al- Gadarif, wakati maandamano ya didi ya Rais wa nchi hiyo Omar al Bashir yakiingia katika wiki ya tatu.

Mashuhuda wanasema kuwa majeshi ya ulinzi yametumia mabomu ya abomu ya kutoa machozi kutawanya kundi la watu, ambao walikuwa wakiimbia wakisema Uhuru, Amani na Mapinduzi kwa Sauti ya watu.

Maandamano hayo yaliandaliwa na Jumuia ya Maprpfesa nchini Sudan, ambayo inamtaka Rais Bashir kujiuzulu.

Akizungumza katika kituo cha jeshi katika mji wa Atbara amelaani kila alichokiita usaliti wa kuchoma mali kwa makusudi na kusababisha madhara.

Ramani ya SudanHaki miliki ya pichaATLAS
Image captionRamani ya Sudan

Wakati huo huo Uingereza, Marekani, Canada na Norway zimetoa taarifa ya pamoja, ikisema kwamba zimeshtushwa na taarifa za vifo na kujeruhiwa kwa wale wote walioshiriki maandamano hayo ya kudai haki zao.

Taarifa hiyo imedai pia kusikitishwa na utumiaji wa silaha za moto unaodaiwa kufanywa dhifi ya waandamanaji.

Katika hatua nyingine maandamano ya kuiunga mkono serikali yanaweza kufanyika leo katika mji mkuu wa nchi hiyo Khartoum.

Maandamano ya kuipinga serikali kwa mara ya kwanza yalianza katikati mwa mwezi Desemba mwaka jana kufuatia kupanda kwa gharama za maisha.

Imeelezwa kwamba bei ya mkate ilipanda mara tatu katika baadhi ya maeneo na gharama za mafuta imeongezeka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *