Mo Dewji: Mfanyabiashara mkubwa Afrika Mashariki atekwa Dar es Salaam

Mo DewjiHaki miliki ya pichaMO DEWJI
Image captionMfanyabiashara tajiri Tanzania,Mo Dewji

Taarifa ambazo bado hazijathibitishwa na vyombo vya usalama nchini Tanzania zinasema kuwa mfanyabiashara maarufu Mohammed Dewji maarufu kama Mo Dewji ,ametekwa leo alfajiri wakati alipokuwa akielekea mazoezini.

Kwamujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, Mo alifika katika hoteli moja ya kifahari katika eneo la Oysterbay jijini Dar es Salaam kama ilivyo ada yake kila siku alfajiri kwaajili ya kufanya mazoezi ya viungo. Hatahivyo, punde aliposhuka tu kwenye gari yake, watu wasiofahamika walijitokeza na kufyatua risasi hewani kisha kumnyakua mfanyabiashara huyo na kutokomea nae kwenye gari lao.

BBC imefanya mazungumzo na Kamanda wa polisi wa kanda maalum ya Dar es Salaam kwa njia ya simu, Lazaro Mambosasa ambaye amesema wamepata taarifa hiyo na wanaifuatilia.

“Tumepata taarifa juu ya tukio hilo na polisi wanalifuatiria kwa karibu”Mambosasa aeleza.

Waziri wa Muugano na Mazingira Tanzania Januari Makamba ambaye ni rafiki wa karibu wa Mo Dewji ameandika katika ukurasa wake wa Twitter kuwa amezungumza na baba mzazi wa Mo ambaye amethibitisha kuwa mfanyabiashara huyo ametekwa.

Mo Dewji mbali na biashara pia ni mwanasiasa na amekuwa mbunge wa Singida Mjini kwa miaka 10 mpaka alipoacha mwaka 2015. Dewji pia ni mpenzi wa michezo na amewekeza katika klabu ya mpira ya Simba ya Tanzania.

Kwamujibu wa jarida maarufu la masuala ya fedha na utajiri, Mo mwenye umri wa miaka 43 ndiyo tajiri namba moja Afrika Mashariki, na pia tajiri mdogo zaidi Afrika. Kwa mujibu wa jarida hilo, Mo anautjiri wa dola bilioni 1.5

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *