Maalim Seif: Yanayotokea chini ya Magufuli, hatujawahi kuyaona Tanzania

Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad anasema mazingira ya kisiasa nchini Tanzania yamebadilika sana na upinzani unakandamizwa zaidi.

Rais John Magufuli mara kwa mara amepuuzilia mbali tuhuma kwamba amekandamiza demokrasia nchini humo.

Maalim Seif, amegombea urais mara kadha Zanzibar, amezungumzia pia mzozo kati ya viongozi wakuu wa chama hicho na Profesa Ibrahim Lipumba, ambapo anasema anaamini uamuzi wa mwandani huyo wake wa zamani kurejea katika chama hicho kama mwenyekiti baada ya kujiuzulu awali si sahihi.

Amemwambia mtangazaji wa BBC Dira ya Dunia TV Zuhura Yunus kwamba mpaka sasa CUF haina mwenyekiti, lakini anaamini hatima ya chama hicho bado ni nzuri hata wanapoendelea kusubiri uamuzi wa mahakama kuu mwezi Januari kuhusu hatima ya Prof Lipumba chamani

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *