Kylie Jenner amekuwa bilionea mwenye umri mdogo zaidi duniani

Kylie Jenner

Kylie Jenner amekuwa bilionea mwenye umri mdogo zaidi duniani, kwa mujibu wa orodha ya mabilionea ya gazeti la Forbes.

Kylie ambaye ndiye mdogo zaidi katika familia ya Kardashian amepata utajiri wake kutokana na biashara ya vipodozi.

Akiwa na umri wa miaka 21-alianzisha na anamiliki kampuni ya vipodozi ya Kylie Cosmetics, biashara ya urembo ambayo imedumu kwa miaka mitatu sasa na kuingiza mapato ya takriban dola milioni $360m mwaka jana.

Alifikia mafanikio haya mapema kuliko muasisi wa mtandao wa kijamii wa Facebook Mark Zuckerberg ambaye alikuwa bilionea akiwa na umri wa miaka 23.

“Sikutarajia chochote. Sikujua hali ya baadae.

“Lakini kutambuliwa inafurahisha. Ni jambo zuri la kunitia moyo,” Bi Jenner aliliambia jarida la Forbes.

Shughuli zakwama katika uwanja wa ndege Kenya

Orodha ya Forbes inaonyesha muasisi wa The list shows Amazon , Jeff Bezos, akiendelea kushikilia nafasi ya kwanza kwa binadamu tajiri zaidi duniani.

Jumla ya utajiri wake ni dola bilioni $131 ,kulingana na jarida la Forbes, ameongeza hadi dola bilioni 19bn kutoka mwaka 2018.

Lakini kiwango cha mapato ya mabilionea wote kwa ujumla kimeshuka kutoka dola trilioni $9.1

Miongoni mwa mabilionea ambao utajiri wao unapungua ni muanzilishi wa Facebook Mark Zuckerberg.

Umeshuka kwa dola bilioni $8.7bn katika kipindi cha mwaka uliopita ulishuka kwa dola bilioni $62, kwa mujibu wa orodha ya jarida la Forbes

Hisa zake katika Facebook wakati mmoja zilipungua kwa thamani yake ya theluthi moja wakati kampuni ilipokua ikikabiliana na kashfa. Hisa za kampuni ya mauzo ya mtandaoni ya Amazon zimefanya vizuri na hivyo kuboresha akaunti za benki za Bwana Bezos na mwanya kati yake na Bill Gates, ambaye yupo katika nafasi ya pili ni mpana kiasi, ingawa utajili wa bwana Gates umepanda kwa doala $96.5bn kutoka dola $90bn alizokuwa nazo mwaka jana.

Kwa mabilionea wote waliotajwa kwenye orodha hiyo ni wanawake 252 tu na mwanamke tajiri zaidi aliyejitafutia utajiri mwenye ni mogul Wu Yajun wa Uchina kupitia kampuni yake ya makazi , akiwa na utajiri wenye thamani ya takriban dola bilioni $9.4bn.

Idadi ya wanawake waliojitafutia utajiri wao imeongezeka kwa mara ya kwanza na kufikia hadi wanawake 72 kutoka wanawake 56 mwaka jana.

Mkurugenzi Mkuu wa Amazon Jeff BezosHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionJeff Bezos – bado ni tajiri anayeendelea kuwa tajiri

Orodha ya jarida la The Forbes ya mabilionea ni kielelezo cha utajiri cha tarehe 8 Februari 2019.

Gazeti hilo hutumia viwango vya bei katika masoko ya hisa vya siku hiyo na viwango wa mauazo ya pesa kutoka kote duniani.

Kulingana na Forbes kuna mabilionea wachache wakiwemo takribani 2,153 miongoni mwao wakiwa katika orodha ya mwaka 2019, kiwango hicho kikiwa kimeshuka ambapo mwaka 2018 vwalikuwa 2,208 . Kwasehemu moja , hii inaelezea ni kwa nini wastani wa utajiri wao ni sawa na thamani ya dola $4bn, ikiwa ni chini ya dola bilioni 4.1bn.

Forbes pia ilibaini kwamba mabilionea 994 miongoni hali yao ya utajiri sio nzuri ikilinganishwa na mwaka jana.

Luisa Kroll, ambaye ni naibu mhariri wa masuala ya utajiri katika jarida la Forbes, amesema: “Hata nyakati za mtikisiko wa uchumu na raslimali mjasiliamali hupata njia za kupata utajiri .”

Mabilionea duniani

Watu wenye utajiri zaidi duniani

Kuna raia 52 wa Uingereza kwenye orodha. Walioko juu ni Hinduja brothers, Srichand na Gopichand, ambao wanamiliki Hinduja Group, wakiwa na jumla ya utajiri wenye thamani ya dola bilioni $16.9bn.

Nyuma yao ni James Ratcliffe, muasisi wa kampuni ya kemikali ya Ineos, mwenye utajiri wa dola bilioni $12.1bn, ambaye ametajwa kama tajiri binafsi.

Jim RatcliffeHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionJim Ratcliffe humiliki asilimia 60% ya kampuni ya Ineos, kampuni ya kemikali aliyoianzisha

Tajiri mwingine anayeibuka ni Safra Catz ambaye ni Mkurugenzi mwenza wa kampuni ya programu ya Oracle, ambaye kwa mujibu wa jarida la huingiza mapato ya dola milioni $41m ya mshahara na ameorodheshwa kama mmoja wa wakurugenzi wanawake wanaolipwa mshahara mkubwa zaidi duniani.

Mark ZuckerbergHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionHisa za kampuni ya Facebook ziliporomoka na kupunguza utajiri wa Mark Zuckerberg

Marekani ina mabilionea 607, idadi hiyo ikiwa ni kubwa kuliko nchi nyingine yoyote duniani.

Uchina inachukua nafasi ya pili ikiwa na mabilionea 324. Lakini orodha ya mabilionea imeshuhudia mabadiliko makubwa – ina mabilionea wapya 44 kwenye orodha huku 102 wakitoka kwenye orodha hiyo.

Kuhuka kwa thamani ya euro kumewaponza mabilionea wa Ulaya ambao hawakujitokeza kwa wingi kwenye orodha ya matajiri wa dunia, huku wakionekana wawili tu miongoni mwa watu 20 tajiri zaidi dunia. : Mkurugenzi mkuu wa kammpuni ya Ufaransa ya bidhaa za burudani LVMH Bernard Arnault (aliwekwa nafasi ya 4), na muasisi wa kampuni ya Index inayomiliki maduka kama Zara-Amancio Ortega (akaorodheshwa katika nafasi ya 6 ).

Forbes linasema kuwa watu 247waliokuwemo kwenye orodha ya mabilionea mwaka jana kwa sasa wametoka. Miongoni mwao ni Domenico Dolce na Stefano Gabbana, wanamitindo na waanzilishi wa Dolce & Gabbana.

Mwenyekiti wa kampuni ya usambazaji wa bidhaa Li & Fung, Victor Fung, pia hayupo tena miongoni mwa mabilionea wa jarida la Forbes, baada ya kuwepo kwenye ododha hiyo kwa miaka 18

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *