Jamaa za Msamaria Mwema ambao bado wako hai na wanazungumza lugha aliyoizungumza Yesu Kristo alipokuwa duniani

The Samaritan Torah has three crowns on it to represent their three tribes of originBORIS DIAKOVSKY/ALAMY

Watu wanapomzungumzia Msamaria Mwema huenda zaidi humfikiria Msamaria aliyeangaziwa katika Biblia aliyemuokoa mwanamume aliyepigwa na majambazi, kuvuliwa nguo na kutupwa kando ya njia kufilia mbali.

Lakini huenda hawajui kwamba kuna mamia ya Wasamaria wa zama za kale Waisraeli ambao bado wanaishi duniani hadi wa leo.

BBC ilifanya ziara nchini Israel kukutana nao.

Japo kulikuwa na hali ya taharuki kati ya Waisraeli na Wapalestina, BBC ilipatana na mwelekezi ambaye alikubali kuwatembeza kwa gari kutoka Israeli hadi kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi na kuelekea hadi milima ya Gerizim ambako kuna kijiji cha Wasamaria kinachofahamika kama Kiryat Luza.

Walipita nyumba za mawe na kufika katika barabara ya vumbi na kusimama mbele ya makavazi moja ya kale.

Ndani ya makavazi hayo kulikuwa na chumba kikubwa ambacho kilikuwa na nguo za kale zinazoaminiwa kuvaliwa na wachungaji wa kale, kipande cha mkate na mti maalum.

Vitu vyote hivi vinaaminiwa kuwepo hapo kwa maelfu ya miaka iliyopita.

Ukuta mmoja ulikuwa umefunikwa na picha za wanaume wazee wenye ndevu na ambao walikuwa wamejifunga kilemba kichwani.

Mchungaji ambaye pia ni mlinzi wa makavazi hayo ya kale alinyooshe kidole moja ya wazee hao na kusema kuwa , ”Huyu alikuwa baba yangu, kohen gadol au kuhani mkuu wa wasamaria wema.

Kizazi cha makuhani kinarudi nyuma tangu zama za Haruni, ndugu wa Musa.”

Amini usiamini Musa huyo ni yule aliyetoa amri kumi za Mungu.

Wageni wengi wanaozuru mlima mtakatifu wa Gerizim ni waumini wa dini ya Kikristo ambao wamevutiwa na mifano iliyotolewa katika Kitabu cha Agano Jipya na ukweli kwamba wasamaria ambao bado wanazungumza lugha ya Kiebrania ambayo ilikuwa ikizungumzwa na Yesu.

Jamii ya wasamaria wema ni moja ya kundi dogo zaidi la kidini dunianiHaki miliki ya pichaEDDIE GERALD/ALAMY

Kulingana na Bibilia Waisraeli waligawanyika katika makabila 12 na Wasamaria wa Israel wanasemekana kutokana na makabila ya: Menasseh, Ephraim na Levi ambayo ni miongoni mwazo.

Baada ya kuhama kutoka Misri na miaka 40 ya kutafuta makaazi, Joshua aliwaongoza wana wa Israel hadi mlima wa Gerizim.

Hapo walijumuika na makabila mengine kwa sherehe iliyohusisha kubariki mlima Gerizim (ambao sasa unafahamika kama Mlima wa Baraka) na kulaani mlima Ebal (Mlima wa Laana).

“Kuna falme mbili za kale: Judea (Yuda/Wayahudi) kutoka kusini, na sisi tulikua kabila kutoka kaskazini. Baadae tulitengana lakini asili yetu ni moja,” alisema, Benyamim (Benny) Tsedaka, mwanazuoni wa Historia na balozi wa wasamaria wa Israel.

Aliongeza kuwa mnamo karne ya sita CE (Baada ya kuzaliwa kwa Yesu), Wasamaria wa Israel walikuwa takriban 1,500,000.

Waliteswa na kuawa kwa sababu ya kufuata imani za kale zilizokuwa zikifuatwa na Wagiriki, Waroma, Byzantine, Waarabu, Wapiganaji wa Kikristo maarufu kama Crusaders, Mamluki na utawala wa Ottoman.

Kufikia mwaka 1919, ni Wasamaria 141 waliyoponea kifo.

Hadi wa leo idadi yao imeongezeka zaidi ya 800, nusu yao wanaishi eneo la Holon (kusini mwa Tel Aviv) na wengine wao wanaishi milimani.

Wao ni moja ya kundi dogo zaidi la dini ya kale na nyimbo zao ni za kale zaidi duniani.

Mlima Gerizim ni makaazi ya Wasmaria wema wanaoishi katika kijiji cha Kiryat LuzaHaki miliki ya pichaHANAN ISACHAR/ALAMY)

Miaka kadhaa baadae BBC ilizuru eneo hilo kwa mara ya pili, na ilipiga kambi katika mji wa Holon uliyopo kusini mwa Tel Aviv, kukutana na Tsedaka.

Tsedaka alikuwa mwenye furaha na bashasha kusimulia hadithi ya watu wake.

Alimzungusha mwandishi wa BBC katika eneo la Holon, ambako karibu familia 80 ya Wasamaria zinaishi na kufanya kazi kama mawakili, waalimu, wahudumu wa benki na wahandisi.

“Hakuna daktari hapa,” alisema Tsedaka, “kwasababu hiyo itamaanisha kufanya kazi siku ya sabato, ambayo imepigwa marufuku.”

Ziara hiyo iliwafikisha katika Sinagogi la Wasmaria, ambalo ni nyumba ndogo ya mawe iliyo na vyumba vingine vidogo.

Juu ya lango kuna maandishi ya Kiebrania. Ndani kuna vitabu vingi vya ibada lakini hakuna viti.

Tsedaka anasema kuwa wanaume wanaoingia humo hupiga magoti au kukaa chini kwenye sakafu na vitabu vyo vitakatifu vinavyo fahamika kama Torah.

Vitabu hivyo vina mataji matatu juu yake, ambayo inawakilisha kabila zao tatu za asili.

Wanaume wanalazimika kuomba katika Sinagogi hilo siku ya Sabato lakini kwa wanawake agizo hilo nila hiari.

Siku ya Ijumaa kabla ya Sabato kuanza, Tsedaka aliitembeza timu ya kwa gari BBC kutoka nyumbani kwake Holon hadi ukanda wa Magharibi, na kuenda hadi makaazi yake ya pili yaliyopo Kiryat Luza bila visa vyovyote vya ghasia japo waandamanaji wa Palestina walikuwa katika eneo hilo.

Wasamaria wanaoishi katika mlima mtakatifu kati ya Palestina na Ukanda wa Magharibi na Wayahudi wa Israel, hujaribu kuwa daraja la kuleta amani kati ya jamii hizo mbili.

Wasamaria wengi huzungumza lugha ya kiarabu, wana majina ya kiarabu na yale ya kiebrania.

Mlima Gerizim umengaziwa sana katika Bibilia na eneo hilo leo ni mbuga ya kitaifaHaki miliki ya pichaHANAN ISACHAR/ALAMY

Kando na kuzungumza lugha ya kala na ya kisasa ya waebrania, baadhi yao wanawezo kuzungumza lugha ya kiingereza.

Tsedaka aidha aliipeleka BBC katika makaazi tatu ya Wasamaria ambayo inatajwa kuwa takatifu zaidi katika mlima wa Gerizim:

  • Mtume Abraham alimtoa mwanawe Issaka kama sadaka;
  • Eneo la Jiwe 12 ambako Joshua aliunganisha makabila baada ya kuhama kutoka Misri
  • Eneo la nguzo kubwa, lenye jiwe la rangi ya-kijivu ambapo Waisraeli waliijenga hema walipofika Israeli.

“Huu unaitwa Milima wa Milele,” Tsedaka alisema “hapa ni mahali patakatifu kushinda yote. Najua Wayahudi wana sehemu nyingine ya matukio hayo yaliyotokea, lakini historia yetu inasema yaliyotokea hapa.”

Jua lilipotua Tsedaka alianza kujiandaa kwa ajili ya kukaribisha siku ya Sabato.

Aliingia chumbani kwake na alipotoka nje alikuwa amebadilisha mavazi yake na kuvalia nguo za kale za maombi kwa waisraeli.

Aliungana na wanaume wenzake waliyokuwa wamevalia kama yeye na kuelekea upande iliyopo Sinagogi.

Walipofika walivua palapa yao na kuziacha mlangoni na kuingia ndani ambako wengine wao walikaa chini, wengine wakapiga magoti na wale waliyokosa nafasi wakasimama pempeni juu ya gunia.

Wakati mwingine wanainama vichwa vyao kuelekea upande wa kanisa lao zamani.

Sauti ya sala zao ilikuwa ya kina na ya kupoteza. Walipoita jina la Musa, walifunika nyuso zao kwa mikono kama Musa alivyofanya wakati Mungu aliposema nae.

Tsedaka, sawa na wanaume wengine huenda kusali katika Sinagogi hilo mara tatu siku ya Sabato kuanzia saa tisa na nusu.

Scholars and tourists come from around the world to witness the Paschal sacrifice, which is performed as it's described in the Book of ExodusHaki miliki ya pichaNIR ALON/ALAMY

Kila mwaka wasomi na watalii kutoka kila pembe ya dunia huzuru mlima huo kutoa sadaka au kushuhudia matambiko ya kidini ambayo imeelezewa katika kitabu cha kutoka.

Kuhani mkuu hukagua kondoo wa kila familia ili kuhakikikisha hawaina matatizo ya kiafya.

Wanyama wote huchinjwa kwa wakati mmoja na kuchomwa pamoja.

Ni ibada ya damu, na washiriki, waliyovalia nguo nyeupe, hupaka damu kwenye vipaji vyao vya uso ili kujikinga na malaika wa kifo.

Usiku wa manane, kondoo waliochijwa huliwa kwa na mboga chungu za kienyeji.

Mara ya tatu BBC ilipozuru eneo hilo miaka kadhaa baadae, Tsedaka alimtembeza mwanahabari wetu katika mji wa Nablus uliyopo katika ukingo wa magharibi kujionea kisima cha Yakubu.

Kisima hicho kimehusishwa na baba yake Yakubu ambaye alizaa makabila 12 ya Israel na inaaminiwa kuwa ni hapo Yesu alipozungumza na mwanamke msamaria.

Ziara hiyo pia iliwapeleka katika kaburi la Yusufu ambalo limekuwa katika mji wa Nablus ambao kwa miaka mingi Waislamu, Wakristo na Wayahudi wamekuwa wakizozania udhibiti wake.

The Samaritans are said to be descended from three of the 12 tribes of Israel: Menasseh, Ephraim and LeviHaki miliki ya pichaYAACOV DAGAN/ALAMY

Siku ya mwisho ya ziara hiyo ya mlima Gerizim mwaka 2012, Tsedaka alipata ruhusa ya kukutana na kuhani mkuu ambaye ni kiongozi wa kidini wa wasamaria wa Israel ambao wanasemekana kizazi chao kinajumuisha makuhani wakuu 130 wanaofikia mwana wa pili wa kiume wa Haruni ndugu wa Musa.

Mazungumzo kati ya BBC na kuhani yalifanyika vyema hadi pale mwandishi wetu alipogusia kuwa amewahi kula nyama ya ngamia.

Kuhani mkuu aligeuza uso wake na kuangalia kando kuonesha ishara ya kuambiwa kitu cha kuaibisha.

“Kula nyama ya ngamia ni vibaya zaidi ya kula nyama ya nguruwe!”

Tsedaka baadae alisema kuwa Kuhani mkuu alimuuliza, ”Vipi yule mgeni wako mlaji wa nyama ya ngamia, alifika nyumbani kwao salama?”

Leo,wasamaria wnaoishi juu ya mlima Gerizim wanajaribu kuwa daraja la kuleta amani kati ya wapalestina na wayahudiHaki miliki ya pichaBORIS DIAKOVSKY/ALAMY

Hiyo bila shaka ni ishara kuwa Wasamaria ambao wanajivunia utamaduni wa jadi wa kidini pia ni wacheshi na kwamba wanajenga urafiki na wageni wanaokuja kujifunza mawili matatu kuwahusu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *