Emile Ratelband: “Tunaishi katika wakati ambao unaweza kubadili jina lako na kubadili jinsia yako’

Juhudi za kisheria za mwanamume wa Uholanzi anayetaka kubadilisha tarehe yake ya kuzaliwa ili kuongeza uwezo wake wa kupata mchumba zimegonga mwamba.

Emile Ratelband mwenye umri wa miaka 69, anataka kubadilisha siku yake ya kuzaliwa kutoka mwezi Machi 1949 mpaka kuwa Machi 1969, akilinganisha na mabadiliko ya kubadilisha jinsia.

“Tunaishi katika wakati ambao unaweza kubadili jina lako na kubadili jinsia yako”.

Kwa nini siwezi kuwa na maamuzi ya umri wangu?” Ratelband alisema.

Hata hivyo mahakama inapinga hilo, ikisema kuwa haki nyingi katika sheria zinategemea miaka ya mtu, kwa kubadilisha hilo huenda shida nyingi zikajitokeza.

Hakuna msingi wa kisheria wa unao ongoza mabadiliko hayo, ilisema mahakama hiyo.

“Bwana Ratelband ana uhuru wa kujihisi kijana wa miaka 20 tofauti na miaka yake halisi na vile vile kubadili mienendo yake kuendana na miaka hiyo anayopendekeza,” majaji walisema, lakini hatua ya kubadilisha stakabadhi zake rasmi huenda “ikawa na athari ya kijamii”.

Bwana Ratelband, ambaye anajiita “Mkufuzi mahiri kutoka Uholanzi “, aligonga vichwa vya habari duniani kutokana na pendekezo lake hilo la kiajabu.

Kabla ya kisikilizwa kwa kesi yake, alifanya mahojiano na vyombo tofauti vya habari ambapo alisema kuwa anahisi kubaguliwa katika sekta ya ajira pamoja na mtandao maarufu ya wapendano inayofahamika kama Tinder.

Ratelband amesema kwamba kwa mujibu wa daktari wake, mwili wake ni wa mtu mwenye umri wa miaka 40 na kujielezea mwenyewe kuwa yeye ni mungu mdogo.

Aliandika kwenye ukurasa wa Facebook mwaka jana na kuelezea namna ambavyo aliamua kuchukua uamuzi huo.

“ikiwa nina miaka 49, ina maana naweza kununua nyumba mpya, kuendesha gari jipya. Naweza pia kufanya kazi zaidi,”alisema . “Nikiingia katika matandao wa Tinder unasema nina miaka 69, siwezi kupata jibu. Nikiwa na miaka 49, na muonekano niliyo nao nitakuwa katika nafasi ya kifahari.

matandao wa TinderHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Licha ya umaarufu aliyopata kupitia vyombo vya habari amekosolewa kwa kutumia pendekezo lake kupewa nafasi ya watu waliyo na mahitaji maalum ya kijinsia katika jamii

Akijitetea mahakamani bwana Ratelband alisema tarehe yake ya kuzaliwa ilikuwa makosa – japo stakabadhi hiyo haina dosari kuhusu siku aliyozaliwa, Machi 11 mwaka 1949.

Mahakama ilikubaliana naye kuwa umri ni sehemu ya utambulisho wa mtu. Lakini tofauti na jinsia ya mtu au jina, ambayo Ratelband anataka kutumia kutetea pendekezo lake ,kuna changamoto ambayo huenda ikajitokeza.

“Haki na wajibu wa mtu pia huunganishwa na miaka… kwa mfano, haki ya kupiga kura, haki ya kuoa au kuolewa,au kuendesha gari,” mahakama ilisema.

Ilibaini kuwa hatua ya kujitambulisha kama mtu mdogo kuliko umri wako halisi huenda ikaleta utatahue..

Katika uamuzi wake mahakama ilisema kuwa kuidhinisha ombi la bwana Ratelband huenda kukasababisha “kila aina ya matatizo”.

Mahakama hiyo pia ilisema kuwa japo mabadiliko ya sheria ya kumruhusu mtu kubadilisha jinsia yake imekuwa ikifanyika katika maeneo tofauti duniani bado kuna mjadala ambao unaozunguka suala hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *