Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi tarehe 01.08.2019: Dybala, Pepe, Coutinho, Rugani, Koscielny, Sane

Manchester United bado hawajaamua kuhusu suala la kuhama kwa Paulo Dybala
Image captionManchester United bado hawajaamua kuhusu suala la kuhama kwa Paulo Dybala

Manchester United bado hawajaamua kuhusu suala la kuhama kwa Paulo Dybala, huku mshambuliaji huyo wa Argentina , 25, akitarajia kujadili na Juventus juu ya hali yake ya baadae wiki hii . (Manchester Evening News)

Dybala ameiambia klabu ya United kuwa itatakiwa kumpa mkataba wenye thamani ya pauni £350,000 kila wiki ikiwa atakiunga nao. (Mail)

Rais wa kblabu ya Lille Gerard Lopez amethibitisha kuwa winga wa Ivory Coast Nicolas Pepe mwenye umri wa miaka 24 atauzwa kwa Arsenal kwa euro milioni 80. (RMC Sport – in French)

Winga wa Ivory Coast Nicolas Pepe mwenye umri wa miaka 24 atauzwa kwa ArsenalHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionWinga wa Ivory Coast Nicolas Pepe mwenye umri wa miaka 24 atauzwa kwa Arsenal

Napoli wamejipanga kwa dau la Euro milioni 60 kwa ajili ya winga wa Crystal Palace na mchezaji wa kimataifa wa Ivory Coast Wilfried Zaha baada ya kumkosa Pepe. (Mail)

Barcelona wanataka kumuuza Mbrazili Philippe Coutinho, lakini wanahofia kuwa kuwa hawajapata ofa yoyote kumuhusu mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 . (ESPN)

Arsenal imetengeneza dau la deni la mlinzi wa Juventus na Italia Daniele Rugani mwenye umri wa miaka 25 kwa ajili ya kuwa nae kwa misimu miwili. (Gazzetta dello Sport, via Sun)

Nahodha Laurent Koscielny, mwenye umri wa miaka 33, bado ameazimia kuondoka Arsenal msimu huu licha ya mazungumzo yanayoendelea baina yake na klabu hiyo.(Independent)

Arsenal imetengeneza dau la deni la mlinzi wa Juventus na Italia Daniele Rugani
Image captionArsenal imetengeneza dau la deni la mlinzi wa Juventus na Italia Daniele Rugani

Arsenal wamejiandaa kumuacha mlinzi wao Mjerumani Shkodran Mustafi aondoke msimu huu, lakini Roma abado hawaweka dau kwa ajili yake licha ya kwamba wanahusishwa na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27.(Romanews, via Star)

Mkurugenzi wa michezo wa Bayern Munich Hasan Salihamidzic anasema kuwa Manchester City wanapaswa kuombwa msamaha baada ya meneja wa klabu Niko Kovac kusema kuwa timu hiyo ya Ligi ya Bundesliga imejipanga kusaini mkataba na winga wa Mjerumani Leroy Sanes mwanye umri wa miaka 23. (Sport Bild – in German)

Zenit St Petersburg wanatarajia kutangaza kusaini mkataba wa winga wa Barcelona Malcolm, mwenye umri wa miaka 22,baada ya klabu mbili kukubaliana kuhusu garamakatika kanda hiyo ya £36.5m na zaidi kwa ajili ya Mbrazili huyo. (Goal)

Aston Villa ya wanamsaka mshambuliaji wa Brentford Mfaransa Neal MaupayHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionAston Villa ya wanamsaka mshambuliaji wa Brentford Mfaransa Neal Maupay

Manchester United wako tayari kukabiliana na Barcelona katika kumpata mshambuliaji wa klabu ya Marseille mwenye umri wa miaka 17 Mfaransa Lihadji msimu huu. (La Provence, via Mail)

Nia ya Aston Villa ya kumsaka mshambuliaji wa Brentford Mfaransa Neal Maupay imeongezeka zaidi baada ya Sheffield United kutafuta katika timu nyingine . (Birmingham Mail)

Sunderland watamrugusu kiungo wao wa kati na nahodha captain George Honeyman, mwenye umri wa miaka 24, kujiunga na kikosi cha Hull Citybadala ya kumkosa mhitimu wa shule ya soka kwa uhamisho wa bure msimu ujao. (Northern Echo)

Mchezaji mwenza wa Neymar katika kikosi cha Paris St-Germain Marco Verratti anakiri kuwa klabu hiyo lazima imuuze mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27- raia wa Brazil ikiwa hana raha katika Parc des Princes, licha ya kocha Thomas Tuchel wa kutaka mchezaji huyo abaki kikosini. (Express)

Real Madrid wamemuambia mshambuliaji wa safu ya kati wa MColombia James Rodriguez kuwa atabaki BernabeuHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionReal Madrid wamemuambia mshambuliaji wa safu ya kati wa MColombia James Rodriguez kuwa atabaki Bernabeu

Juventus amethibitisha kuwa kumekuwa na ofa kwa ajili ya mshambuliaji wake raia wa Argentina Paulo Dybala, huku kukiwa na nia ya kumnunua mchezaji huyo kutoka kwa Manchester United na Tottenham ya kumnunua . (Mirror)

Mlinzi wa zamani wa Barcelona Carles Puyol, mwenye umri wa miaka 41, amesema kuwa alikataa mara mbili ombi la Real Madrid la kutaka ajiunge nao. (AS in Spanish)

Meneja wa Rangers Steven Gerrard amethibitisha kuwa uhamisho wa winga wa Liverpool Muingereza Ryan Kent, ambaye ana umri wa miaka 22, haupo na kwamba hawawezi kumudu uhamisho wake kudumu . (Daily Record)

Tetesi za soka Ulaya Jumanne 05.02.2019: Insigne, Pogba, Rashford, Hudson-Odoi

Lorenzo InsigneHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Liverpool imewasilisha ombi la takriban Euro milioni 70 kwa mshambulaiji wa Napoli Lorenzo Insigne, mwenye umri wa miaka 27. (La Repubblica kupitia Sport Witness)

Bayern Munich itarudi na ombi la £ milioni 35 kwa winga wa Chelsea Callum Hudson-Odoi, mwenye umri wa miaka 18, katika msimu wa joto baada ya kushindwa kumsajili mchezaji huyo wa timu ya England ya wachezaji wa chini ya miaka 19 mwezi Januari. (Mail)

Mshambuliaji wa Manchester United Marcus Rashford, mwenye umri wa miaka 21, anafanya mazungumzo kuhusu mkataba mpya katika klabu hiyo ambayo huenda yakaongeza mshahara wake kwa mara mbili hadi zaidi ya £150,000 kwa wiki. (Telegraph)

Mchezaji wa kiungo cha kati wa United Paul Pogba aliwahi kutafakari kuondoka katika klabu chini ya mkufunzi wa zamani Jose Mourinho, kwa mujibu wa kakake, Mathias. (Telefoot kupitia Mirror)

Mshambuliaji wa Tottenham Vincent Janssen, mwenye umri wa 24, ameambiwa na meneja Mauricio Pochettino kwamba atajumuishwa katika kikosi cha timu hiyo katika ligi kuu ya England, licha ya kutojumuishwa katika timu ya Spurs tangu Agosti 2017. (Evening Standard)

PogbaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Meneja wa Arsenal, Unai Emery atakuwa na £40 milioni pekee kutumia msimu wa joto, baada ya kushindwa kusajili mchezaji kwa mkataba wa kudumu mwezi Januari. (Mirror)

Emery anataka kusaini angalau wachezaji watatu wapya msimu wa joto, akiwemo beki wa kushoto. (Mail)

Gunners wamekuwa wakimsaka beki wa kati wa Red Bull Leipzig raia wa Ufaransa Ibrahima Konate, mwenye umri wa miaka 19. (Bild – kupitia ESPN)

Mkataba wa mkopo wa mchezaji wa kiungo cha mbele wa Fulham Andre Schurrle kutoka Borussia Dortmund utamalizika msimu wa joto – mwaka mmoja mapema kuliko ilivyopangwa – iwapo timu hiyo ya Cottagers itashushwa daraja kutoka ligi kuu ya England. (Kicker – Kijerumani)

Hertha Berlin inataka kuendelea kuwa na mchezaji wa kiungo cha kati wa Liverpool Marko Grujic, mwenye umri wa miaka 22, kwa mkopo kupita hata baada ya mwisho wa msimu. (Liverpool Echo)

Mkataba wa mkopo wa Andre Schurrle kutoka Borussia Dortmund utamalizika msimu wa jotoHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMkataba wa mkopo wa Andre Schurrle kutoka Borussia Dortmund utamalizika msimu wa joto

Barcelona inataka kumsajili mchezaji wa Ajax mwenye umri wa miaka 19 Matthijs de Ligt katika msimu wa joto na itabidi ilipe euro milioni 75. (Mundo Deportivo Kihispania)

Cristiano Ronaldo amemeuita aliyekuwa mchezaji mwenzake wa Real Madrid James Rodriguez, ambaye kwa sasa anacheza kwa mkopo Bayern Munich, katika jitihada za kumshawishi mchezaji huyo raia wa Colombia mwenye miaka 27, ajumuike naye Juventus. (Marca)

Bora kutoka Jumatatu

Mario BaloteliHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Mshambuliaji wa Marseille Mario Balotelli, 28, anasema kuwa anataka kumaliza kazi yake ya kusakata soka kwa kuichezea timu yake ya nyumbani ya Brescia nchini Itali. (goal)

Mkufunzi wa Everton Marco Silva anasema kuwa anajua kwamba yuko chini ya shinikizo baada ya kikosi chake kushindwa na klabu ya Wolves na kusalia katika nafasi ya tisa katika jedwali la ligi ya Uingereza. (mirror)

Klabu ya Leeds inataka kumnunua winga wake wa zamani Aaron lennon, 31, kurudi katika klabu hiyo kwa kupitia kumsajili kutoka klabu ya Burnley mwisho wa msimu huu. (sun)

Ibrahim DiazHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Mshambuliaji wa Stoke City Bojan Krkic ,28, huenda akahamia katika klabu ya ligi ya Marekani New England Revolution ambayo imejitolea kumlipa mara mbili marupurupu yake huku dirisha la uhamisho nchini Marekani likiendelea kuwa wazi hadi tarehe mosi mwezi Mei. (sun)

Real Madrid haitamuuza kwa mkopo mwisho wa msimu huu kiungo wa kati wa Uhispania mwenye umri wa miaka 19 kinda Ibrahim Diaz ambaye walimsajili kutoka Manchester City. (AS)

Aaron lenon

Shirikisho la soka la Uingereza FA linataka kuanzisha refa wa kwanza atakayesimamia mechi za ligi ya wanawake ya.. (telegraph).

Kiungo wa kati wa Newcastle Sean Longstaff, 21, huenda akaitwa na timu ya Uingereza ilio na wachezaji wasiozidi umri wa miaka 21 baada ya kushirikishwa katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo.(Chronicle)

Mohamed Salah: Mshambuliaji wa Liverpool na Misri atawazwa mchezaji bora wa mwaka Afrika wa Caf kwa mwaka 2018

Mohamed Salah alikabidhiwa tuzo hiyo na rais wa Caf Ahmad Ahmad (kushoto) na rais wa Liberia George Weah (kulia)
Mohamed Salah alikabidhiwa tuzo hiyo na rais wa Caf Ahmad Ahmad (kushoto) na rais wa Liberia George Weah (kulia)

Mshambuliaji wa Misri na klabu ya Liverpool ya England Mohamed Salah ndiye Mchezaji Bora wa Mwaka wa Shirikisho la Soka Barani Afrika kwa mwaka 2018 – hii ikiwa ni mara yake ya pili kushinda tuzo hiyo.

Salah, 26, alimshinda mwenzake wa Liverpool Sadio Mane kutoka Senegal na mshambuliaji wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang.

Alikabidhiwa tuzo hiyo katika sherehe iliyofanyika nchini Senegal Jumanne.

“Nimekuwa na ndoto ya kushinda tuzo hii tangu nilipokuwa mdogo na sasa nimefanya hivyo mara mbili mtawalia,” Salah alisema.

Mshambuliaji wa Houston Dash kutoka Afrika Kusini Thembi Kgatlana alitawazwa Mchezaji Bora wa Mwaka wa kike.

Salah pia alitawazwa Mwanakandanda Bora wa Mwaka wa Afrika wa BBC kwa mara ya pili mtawalia Desemba.

Aliwafungia Liverpool mabao 44 msimu wa 2017-18 na kuisaidia klabu hiyo kufika fainali Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya ingawa walishindwa na Real Madrid.

Aidha, alifunga mabao mawili akichezea Misri katika Kombe la Dunia nchini Urusi.

Amefunga mabao 16 katika mechi 29 alizoichezea Liverpool mashindano yote msimu huu.

Salah, Mane na Aubameyang wamo kwenye Kikosi Bora cha Mwaka Afrika pamoja na beki wa Manchester United Eric Bailly, kiungo wa kati wa Manchester City Riyad Mahrez, kiungo wa kati wa Liverpool Naby Keita na beki wa kushoto wa Tottenham Serge Aurier.

Jumanne, Caf ilitangaza pia kwamba Misri itakuwa mwenyeji wa michuano ya Kombe la Taifa Bingwa Afrika mwaka 2019 baada ya Cameroon kushindwa kujiandaa kwa wakati.

Kikosi Bora cha Afrika XI: Denis Onyango (Mamelodi Sundowns/Uganda), Serge Aurier (Tottenham/Ivory Coast), Medhi Benatia (Juventus/Morocco), Eric Bailly (Manchester United/Ivory Coast), Kalidou Koulibaly (Napoli/Senegal); Naby Keita (Liverpool/Guinea), Thomas Partey (Atletico Madrid/Ghana), Riyad Mahrez (Manchester City/Algeria); Mohamed Salah (Liverpool/Misri), Pierre-Emerick Aubameyang (Arsenal/Gabon), Sadio Mane (Liverpool/Senegal)

Africa Best XI graphic

Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 28.12.2018: Ramsey, Hazard, Nasri, Higuain, Pogba

Paris St-Germain wamefanya mazungumzo na kiungo wa kati wa Arsenal Aaron Ramsey, 28, kuhusu kuhama mwezi Januari. Mchezaji huyo kutoka Wales hana mkataba mwisho wa msimu. (L’Equipe – in French)

Na klabu hiyo ya Ufaransa anaweka tayari pauni milioni 9 kwa ofa ya Ramsy kuwazuia Bayern Munich na Juventus. (Mirror)

PSG pia wanamfuatilia mchezaji mwenye miaka 29 kiungo wa kati wa Everton na Senegal Idrissa Gueye. (L’Equipe – in French)

HazardHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionHazard

Manchester United watamfikiria meneja wa Juventus Massimiliano Allegri wanapomsaka meneja mpya wa kudumu. (ESPN)

Tottenham wanaamini Real Madrid ni tisho kubwa kuliko United kumchukua meneja Mauricio Pochettino. (Telegraph)

Lakini United hawatamtangza meneja wo mpya kabla ya mwisho wa msimu. (Talksport)

Eden Hazard bado hayuko tayari kuzungumzia mkataba mapya huko Chelsea hadi msimu ujao licha ya Real Madrid kuonyesha dalili za kumwinda mchezaji huyto wa miak 27. (Sun)

Samir NasriHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionSamir Nasri

West Ham wamempa Samir Nasri, 31, ofa ya mshahara wa paunia 80,000 kwa wiki hadi mwisho wa msimu huku marufuku yake ya kutumia dawa iiliyopigwa marufuku ikitarajiwa kuisha Desemba 31. (Mirror)

Mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane amesema mafanikio ya timu yake msimu huu yanamaanisha hawatamsaini mechezaji yeyote msimu ujao. (ESPN)

Beki wa Liverpool Alberto Moreno anasema hana furaha jinsi ametendewa na meneja Jurgen Klopp na anataka kurudi Uhispania wakati mkataba wake unatarajiwa kumamilika mwezi Juni. (Onda Cero, via AS)

Alberto MorenoHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionAlberto Moreno

Meneja wa Everton Marco Silva anasisitiza kuwa mshambuliaji mturuki Cenk Tosun, 27, bado ana matumaini katika klabu nhiyo. (Guardian)

Real Madrid wanataka kumsaini beki wa Real Betis Junior Firpo, 22, kama mrithi wa Marcelo lakini anakabiliwa na ushindani kutoka Arsenal na Manchester City. (AS)

Kipengee cha mkataba wa mchezaji wa Arsenal Alex Oxlade-Chamberlain kinamaanisha kwa Arsenal ilihitajika kulipa klabu ya zamani ya Southampton pauni 10,000 kwa kiungo huyo wa kati wa England kwa kila zaidi ya dakika 20 alizocheza (Mail)

Paul PogbaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionPaul Pogba

Beki wa Colombia Jeison Murillo, 26, anataka kuhamia kabisa Barcelona baada ya kujiunga kwa mkopo kutoka Valencia hadi mwisho wa msimu na anaweza kusainiwa kwa pauni milioni 22.6. (Marca)

Thorgan Hazard ndugu mdogo wa Eden hataruhusiwa kuondoka Borussia Monchengladbach mwezi Januari licha kuwa vilabu kadhaa vimeonyesha ni ikiwemo Tottenham, huku Chelsea ikiwa na kipengee cha kununua tena msimu huu. Bild – in German)

Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 11.12.2018: Hazard, Fabregas, Man, Slimani, Neves, Almiron

Eden Hazard
Image captionEden Hazard

Mchezaji wa Chelsea Eden Hazard, 27, tena amezungumzia kuhama kwenda Real Madrid na anasema kuwa hajui ni lini ataamua hatma yake. Lakini Mbelgiji huyo amekiri kuwa mazungumzo kuhusu mkataba mpya huko Stamford Bridge yamekwama. (RMC Sport via Express)

Mkurugenbzi wa michezo wa AC Milan Leonardo amethibitisha kuwa klabu hiyo ya Serie A imezungumza Chelsea kuhusu uwezekano wa kumsaini kiungo wa kati Cesc Fabregas, 31. (London Evening Standard)

Tottenham wamejiunga na Manchester United katika kumwinda mshambuliaji raia wa Romania Dennis Man, mchezaji huyo mwenye miaka 20 aiyechezea FCSB ambayo awali ilikuwa inajulikana kama Steaua Bucharest. (Sun)

Cesc FabregasHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionCesc Fabregas

Spurs wanachelewa zaidi kuufungua uwanja wao mpya kutokana na ugumu wa kuandaa warsha wakati huu wa msimu wa krismasi. (Times)

Meneja wa Fulham Claudio Ranieri yuko tayari kumsaini mchezaji wa pili Islam Slimani mwezi Januari. Ranieri alimsaini mchezaji huyo wa miaka 30 raia wa Algeria wakati akiwa meneia wa Foxes. (Telegraph)

Ajenti wa kiungo wa kati wa Wolves mreno Ruben Neves anatakana mchenzia huyo mwenye miaka 21 kuhamia Juventus. (Calciomercato – in Italian)

Ruben NevesHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionRuben Neves

Baba yake Miguel Almiron amesema Newcastle wako nafasi nzuri ya kumsaini mtoto wake huyo mwenye miaka 24 kutoka Atlanta United mwezi Januari. (Newcastle Chronicle)

Leeds na Aston Villa watajaribu kumsaini kipa Karl Darlow mwezi ujao. Mchezaji huyo mwenye miaka 28 alipoteza nafasi yake huko Newcastle na amecheza mechi moja peke yake msimu huu. (Sun)

Mlinzi wa zamani wa England na BT Sport pundit Rio Ferdinand alimtaja mlinzi wa Manchester City mwenye miaka 28 Kyle Walker kuwa tegemeo kubwa wakati City walishindwa na Chelsea siku ya Jumamozi kwa mabao 2-0. (Independent)

Kyle WalkerHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionKyle Walker

Mlinzi wa zamani wa Cardiff Greg Halford, 34, amekuwa akifanya mazoezi na West Brom na atapewa mkataba wa muda mfupi na klabu hiyo. (WalesOnline)

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amethibitisha kuwa hataifunza Italia hivi karibuni na kupuuza maswali kuwa Nopoli wanataka huduma zake wakati akiwa huko Dortmund. (Liverpool Echo)

Wing’a wa Bayern Munich Mholanzi Arjen Robben, 34, anasema atastaafu ikiwa ofa ya sasa haitafanikiwa wakati mkataba wake utamalizika msimu huu. (Goal)

West Bromwich Albion wanataka kumsaini kuiungo wa kati wa Leicester na Wales Andy King, 30, kwa mkopo mwezi Januari. (Mail)

Victor MosesHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionVictor Moses

Chelsea watamuuza Victor Moses mwezi ujao huku Crystal Palace na Fulham wakitaka kutoa ofa zao kwa mchezaji huyo anayewekewa thamani ya pauni milioni 12 mwenye miaka 27 ambaye mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Nigeria. (Sun)

Barcelona wanamfuatilia mshambualjia wa Everton raia Brazil Richarlison, 21. (Star)

Kiungo wa kati wa kisosi cha Manchester City cha chini ya miaka 21 Phil Foden, 18, anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka sita. (Telegraph)

Phil FodenHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionPhil Foden

Chelsea wanataka kumuongezea mkataba wa miaka 12 mlinzi raia wa Brazil David Luiz, 31, baada ya msimu huu ambao utamwezesha kutafuta kwingine. (Mirror)

Mlinzi wa kikosi cha chini ya miaka 21 wa Everton raia wa England Mason Holgate, 22, ameambiwa kuwa anaweza kuondoka kwa mkopo mwezi Januari. (Mirror)

Marseille wanawatafuta mabeki wawili – Nacho Monreal, 32, wa Arsenal na Alberto Moreno, 26 wa Liverpool wakati wanapanga kuboresha kikosi chao mwezi Januari. (France Football, via Mirror)

Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 15.11.2018: De Gea, Wenger, Foden, Neymar, Mbappe, Smalling

Meneja wa zamani wa Arsenal, Arsene Wenger
Image captionMeneja wa zamani wa Arsenal, Arsene Wenger

Meneja wa zamani wa Arsenal, Arsene Wenger amekataa kuchukua nafasi ya Slavisa Jokanovic kuwa kocha wa Fulham ingawa tayari Claudio Ranieri alikuwa amepewa. (Daily Mirror)

Huku meneja wa zamani wa Chelsea na Tottenham, Andre Villas-Boas pamoja na kocha wa zamani wa Monaco Leonardo Jardim wote wameikataa nafasi ya kuiongoza Fulham. (Telegraph)

Meneja mpya wa Fulham Ranieri, anataka kumsajili mlinzi wa Liverpool Joel Matip, 27 mwezi Januari. (A Spor, via Talksport)

Real Madrid iko tayari kumchukua mmoja wa washambuliaji wa Paris St-Germain kama klabu ya Ufaransa itawauza wachezaji wake kutokana na sababu za matumizi zaidi ya kifedha. Wachezaji hao ni Neymar, 26, na Kylian Mbappe, 19. (AS – in Spanish)

Fifa inavichunguza vilabu vitano vya ligi ya England kuhusu uvunjwaji wa kanuni za usajili wa wachezaji wa kigeni ambao wako chini ya umri wa miaka 18.

Timu hizo zitafugiwa kufanya usajili ikiwa zitakutwa na hatia ya kukiukwa na kanuni za usajili. (Daily Telegraph)

Kipa wa Manchester United David de Gea, 28
Image captionKipa wa Manchester United David de Gea, 28

Kipa wa Manchester United David de Gea, 28, anaendelea na majadiliano kuhusu kusaini mkataba mpya. Mkataba wa sasa wa de Gea utaisha muda wake katika kipindi cha kiangazi lakini klabu inataka kumuongezea miezi 12. (London Evening Standard)

Everton inataka kumsajili mlinzi wa kati Chris Smalling, 28,mwishoni mwa msimu huu wakati ambao mkataba wake utakuwa umeisha. (The Sun)

Kiungo wa kati wa Manchester City na England Phil Foden,18 anakaribia kusaini mkataba mpya wa miaka sita. (Daily Telegraph)

kipa wa Southampton Alex McCarthyHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionKipa wa Southampton Alex McCarthy

Meneja wa England Gareth Southgate atamtumia kwa mara ya kwanza goli kipa wa Southampton Alex McCarthy, mlinzi wa Brighton Lewis Dunk na mshambuliaji wa Bournemouth Callum Wilson katika mechi ya kirafiki dhidi ya Marekani itakayofanyika siku ya alhamisi. (Daily Mirror)

Chelsea wanavutiwa kumsajili mchezaji wa Borussia Dortmund Christian Pulisic, 20, katika msimu wa kiangazi. (The Guardian)

Chelsea wako tayari kusikiliza ofa ya mkopo ya mlinzi wa kati na nahodha Gary Cahill, 32, ambaye mkataba wake unaisha mwisho wa msimu. (Daily Mail)

Gary Cahill, 32Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionGary Cahill, 32

Roma inajiandaa kumsajili mchezaji wa Manchester United Ashley Young, 33 mwezi Januari. (The Sun)

Wolves inatamani kumsajili mlinzi wa Argentina Marcos Rojo, 28, ambaye atakuwa huru kuondoka Manchester United mwezi Januari. (Birmingham Mail)

Newcastle inavutiwa na Miguel Almiron mwenye umri wa miaka 24 ambaye ni kiungo wa kati wa Paraguay anayecheza ligi ya nchini Marekani. (The Chronicle)

Zlatan Ibrahimovic, 37Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionZlatan Ibrahimovic, 37

AC Milan inataka kumsajiri kwa mara nyingine mshambuliaji wa Sweden Zlatan Ibrahimovic, 37. (Calciomercato).

Tetesi za soka Ulaya Ijumaa 02.11.2018: Ramsey, Fabregas, Suarez, Gomez, Fabinho

Aaron Ramsey(kulia) alijiunga na Arsenal mwaka 2008 Ramsey(kulia) alijiunga na Arsenal mwaka 2008

Chelsea huenda ikabadili msimamo kuhusu mpango wake wa kumnunua kiungo wa kati wa Arsenal Aaron Ramsey, 27,kutokana na kuimarika kwa mchezo wa Ross Barkley, 24, na Ruben Loftus-Cheek, 22. (Star)

Huku hayo yakijiri, Liverpool imefutilia mbali uwezekano wa kiungo huyo wa kimaatifa wa Wales ambaye yuko tayari kuondoka Gunners bila malipo msimu wa joto kujiunga nayo. (Sky Sports)

Kiungo wa kati wa Mhispania Cesc Fabregas, 31, atalazimika kusubiri hadi mwaka mpya kabla ya kuanza mazungumzo ya kandarasi mpya na Cheasea . (Evening Standard)

Suarez amefunga mabao tisa dhidi ya Real MadridHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionSuarez amefunga mabao tisa dhidi ya Real Madrid

Mshambuliaji wa Uruguay Luis Suarez, 31, anasema Barcelona hivi karibuni itaanza kumtafuta mtu atakaechukua nafasi yake licha ya kufunga hat-trick katika mechi ya El Clasico. (Sport 890, via Sun)

Liverpool inajiandaa kumpatia kandarasi mpya mlinzi wa England defender Joe Gomez, 21, miaka tatu na nusu hata kabla ya kumalizika kwa mkataba wake wa sasa. (Mirror)

Kiungo wa kati wa Brazil Fabinho huenda akaondoka Liverpool miezi sita tu baada ya kuhamia Anfield kwasababu ”ameboeka”. (Le Parisien – in French)

Meneja wa timu ya taifa ya Ubelgiji Roberto Martinez amesema “Hatutapoteza muda wetu kujadili hilo” alipoulizwa kuhusu tetesi za Real Madrid kutaka kumpatia kazi kama meneja wake mpya. (AS, via VTM Nieuws)

Wigan manager Roberto Martinez

Tottenham inapania kumnunua kiungo wa kati wa Watford, mfaransa Abdoulaye Doucoure, 25. (Mirror)

Meneja wa Manchester United boss Jose Mourinho ana mpango wa kufanya usajili zaidi ya moja wakatu dirisha la uhamisho litakapo funguliwa mwezi Januari- Ni mara ya kwanza klabu hiyo itafanya hivyo katika kipindi cha miaka 10. (Manchester Evening News).

Borussia Dortmund inataka kumsajili kiungo wa kati wa Manchester City na Uhispania Brahim Diaz, 19. (Metro)

Lakini meneja wa Manchester City Pep Guardiola anasema klabu hiyo “itafanya kila iwezalo” kumshawishi asiondoke. (Manchester Evening News)

Dele Alli kusalia Spurs hadi 2024 baada ya kutia saini mkataba mpyaHaki miliki ya pichaAFP
Image captionDele Alli kusalia Spurs hadi 2024 baada ya kutia saini mkataba mpya

Kiungo wa kati wa Tottenham Dele Alli, 22, anasema “kushinda kombe sio kila kitu ukizingatia umri wangu” baada ya kutia saini mkataba mpya wa miaka sita na Spurs mapema wiki hii. (Telegraph)

Wanaotunga sheria za kandanda huenda wakajadili mabadiliko yatakayo fafanua sheria ya kugusa mprira kwa mkono na kuondoa “makusudi”. (Telegraph)

Wachezaji wa Fulham watalazimika kukubali kupunguziwa mshahara endapo wataondolewa wakatika ligi ya Primia. (Mail)

Bora kutoka Alhamisi

Raheem SterlingHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionRaheem Sterling

Mshambuliaji wa Manchester City Raheem Sterling, 23, ambaye kandarasi yake inamalizika mwisho wa msimu huu, anatarajiwa kutia saini mkataba mpya.

Hatua hiyo huenda ikatia kikomo shinikizo za mashabiki kutaka kiungo huyo kuondoka klabu hiyo kutokana na utenda kazi wake duni uwanjanani. (Manchester Evening News)

Aaron Ramsey, 27, kiungo wa kati wa Wales, ameambiwa na Arsenal anaweza kuihama klabu hiyo msimu ujao wa joto. (Mail)

Antonio Conte aliongoza Chelsea kushinda kombe la FA mwezi MeiHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionAntonio Conte aliongoza Chelsea kushinda kombe la FA mwezi Mei

Aliyekuwa meneja wa klabu ya Chelsea Antonio Conte bado anapigiwa upatu kuchukua wadhifa wa kuwa mkufunzi mkuu katika klabu ya Real Madrid licha ya tetesi za mapema wiki hii kwamba hakuna uwezekano huo. (AS)

Juventus inatarajiwa kumwinda kiungo wa kati wa Manchester United kutoka Uhispania Juan Mata, 30 mwezi Januari.

Mata anahudumia mkondo wa mwisho wa kandarasi yake katika uga wa Old Trafford. (Evening Standard)

Tetesi za Soka Ulaya Jumapili 21.10.2018: Hazard, Sterling, Ake, Rooney, Malcom, Barella

Eden Hazard

Chelsea wanataka kumfanya Eden Hazard kuwa mchezaji anayelipwa kitita cha juu zaidi katika Ligi ya Premier kwa kumpa ofa ya mshahara wa dola 350.000 kwa wiki. (Express)

Mwanamfalme wa Saudi Arabia Prince Mohammed bin Salman anatarajiwa kukutana na wamiliki wa Manchester United familia ya Glazer wiki chache zinazokuja, kuwasilisha ofa ya dola bilioni 4 kuinunua klabu hiyo. (Mirror)

Manchester City wanakataa kubadilisha msimamo wao kuhusu masharti ya mkataba wake na Raheen Sterling, na kuongeza hofu kuwa mchezaji huyo wa miaka 23 wa England anaweza kuondoka msimu ujao. (Mirror)

Raheen SterlingHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionRaheen Sterling

Real Madrid wako tayari kumpa ofa Sterling mwezi Januari. (Express)

Manchester City wanatathmini ofa ya pauni milioni 40 kwa mchezaji wa Bournemouth Nathan Ake mwezi Januari. Mchezaji huyo mwenye miaka 23 wa Uholanzi pia amehusishwa na Manchester United na Tottenham. (Sun)

Tottenham wanapanga kumuendea kiungo wa kati wa Blackburn Bradley Dack, 24, kutokana na ripoti nzuri za majenti. (Express)

Meneja Manchester United Jose Mourinho anataka kumleta mlinzi wa Fiorentina Nikola Milenkovic. Mchezaji huyo wa kimataifa raia wa Serbia anawekewa thamani ya dola milioni 40 na klabu ya Italia kwa kuwa wanajua anawindwa na United, Tottenham, Chelsea, Arsenal na Juventus. (Star)

Jose MourinhoHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionJose Mourinho

Arsenal wanataka kumsaini wing’a wa Barcelona raia wa Brazil Malcom, 21, mwezi Januari kwa mkopo. (Star)

Meneja wa Arsenal Unai Emery amekiri kuwa alikuwa anataka kumsaini mshambuliaji wa sasa wa Arsenal na Ufaransa Alexandre Lacazette mwanzo wa msimu wa mwaka 2016 – 2017 wakati akiwa meneja wa Paris St-Germain. (Mirror)

Kiungo wa kati wa Cagliari mwenye miaka 21 raia wa Italia Nicolo Barella, ambaye analengwa na Arsenal na Liverpool hatajiunga na klabu nyingine kwa sababu za pesa bali kwa sababu za ndoto. (Calciomercato)

Nicolo BarellaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionNicolo Barella

Meneja Mauricio Pochettino anasema Tottenham inataka kuwasaini wachezaji Januari, baada ya kutomsaini mchezaji yeyote wakati wa msimu wa joto. (Enfield Independent)

Mlinzi wa Real Madrid Marcelo, 30, anasema wachwzaji wako chini ya shinikizo kutoka kwa meneja Julen Lopetegui baada ya kupata pigo lingine siku ya Jumamosi (Marca)

Bora Zaidi Kutoka Jumamosi

Mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho anaamini kwamba Hazard ataisaidia Chelsea kushinda taji la ligi ya Uingereza msimu huu. (Daily Star)

Mshambuliaji wa man United Anthony Martial ,22, ambaye hana kandarasi na klabu hiyo mwisho wa msimu huu analenga kuondoka katika klabu hiyo. (Mirror)

Anthony MartialHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionAnthony Martial

Mchezaji anayelengwa na Tottenham na Juventus Anthony Martial amekataa ofa kadhaa za kuandikisha kandarasi mpya na United. (RMC Sport via Calciomercato)

Nahodha wa klabu ya Juventus Giorgio Chiellini, 34, amemwambia kiungo wa kati wa Manchester United Paul Pogba, 25, kwamba anakaribishwa tena katika klabu hiyo ya Itali.. (Mirror)

Chelsea itajaribu kumsaini mshambuliaji mpya mnamo mwezi Januari baada ya kupoteza subira na mshambuliaji Alvaro Morata, 25. (Sun)

Pep GuardiolaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionPep Guardiola

Mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola amesema kuwa mchezaji wa Borussia Dortmund na Uingereza kinda Jadon Sancho huenda asirejee katika klabu hiyo katika kipindi chake cha ukufunzi. (Manchester Evening News)

Manchester City imeanza mazungumzo na winga Leroy Sane, 22, kuhusu kumuongezea kandarasi yake , licha ya kwamba raia huyo wa Ujerumani ana takriban miaka miwili na nusu iliosalia katika kandarasi (Telegraph