Benki ya Dunia yaridhia kuikopesha Tanzania dola milioni 300

Dkt Hafez Ghanem
Rais Magufuli na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Dkt Hafez Ghanem wamefanya mazungumzo Ikulu, Dar es Salaam

Benki ya Dunia imeridhia kutoa Dola za Marekani Milioni 300 sawa na shilingi bilioni 680.5 kwa Tanzania kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa kuongeza ubora wa elimu ya sekondari, Ikulu ya Tanzania imeeleza.

Fedha hizo zinaokusudiwa kujenga vyumba vya madarasa, mabweni, maabara, nyumba za watumishi na kununua vifaa vya kufundishia.

Makubaliano hayo yamefikiwa hii leo baada mkutano wa Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Dkt. Hafez Ghanem na Rais John Magufuli yaliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Ghanem amesema pamoja na kuridhia kutoa fedha za mradi huo, Benki hiyo inaendelea kufadhili miradi mbalimbali ya maendeleo nchini Tanzania yenye thamani ya Dola za Marekani Bilioni 5.2 sawa na zaidi ya shilingi Trilioni 13.

Makubaliano hayo yanafuta maamuzi ya awali ya uongozi wa benki hiyo ya kuzuia mkopo huo.

Chanzo cha kuaminika kutoka benki hiyo kiliiambia BBC Swahili Jamatano, Novemba 14 kuwa mkopo huo ulisitishwa kutokana na ukiukwaji wa haki za binaadamu nchini Tanzania.

Sababu kuu mbili za zuio hilo zilikuwa ni mosi, uamuzi wa Rais John Magufuli wa kuzuia wanafunzi wanaopata ujauzito kuendelea na masomo mara baada ya kujifungua.

Pili, maboresho ya Sheria ya Takwimu yaliyopitishwa na Bunge la Tanzania Septemba 10 ambapo pamoja na mengine, inakataza usambazaji wa takwimu zinazolenga kupinga, kupotosha au kukinzana na takwimu rasmi za serikali.

Adhabu ya kufanya hivyo ni faini ya Dola 6,000 au kwenda jela miaka mitatu.

Afisa huyo wa Benki hiyo pia aliithibitisha BBC kuwa safari zote rasmi za wafanyakazi wa Benki ya Dunia zimesitishwa kutokana na hofu ya kukamatwa na kushtakiwa watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja.

KikaoHaki miliki ya pichaIKULU TZ

Hata hivyo, benki hiyo ilisema itaendelea na majadiliano na serikali ya Tanzania.

“Tukishirikiana na wadau wengine tutaendelea kupigania haki ya wasichana kupata elimu kwa kujadiliana na serikali ya Tanzania,” ilisema sehemu ya barua pepe ya Benki ya Dunia kwa BBC Swahili.

Haijafahamika ni makubaliano gani yaliyofikiwa mpaka sasa mkopo huo umekubaliwa kutoka. Hata hivyo, Rais Magufulia amesema pesa hizo “hazijafyekelewa mbali” kama baadhi ya watu “wasiotutakia mema walivyosema.”

Rais Magufuli amenukuliwa akisema kuwa Ghanem amekwenda Tanzania kuthibitisha kuwa Benki ya Dunia haitaiacha nchi hiyo.

Wote

“Namshukuru Dkt. Hafez Ghanem na Benki ya Dunia kwa kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya miradi ya Tanzania, hizo Dola Milioni 300 ambazo baadhi ya watu wasiotutakia mema walisema zimefyekelewa mbali, anasema zitaletwa, na pia Benki ya Dunia imetoa Dola Bilioni 5.2 ambazo zinafadhili miradi mbalimbali ya elimu, nishati, barabara, kilimo, afya na maji, ni miradi mikubwa na mingi.

Kwa hiyo amekuja kututhibitishia kuwa Benki ya Dunia haitatuacha.” amesema Rais Magufuli.

Mazungumzo kati ya Magufuli na Ghanem yamehudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Nje Dkt. Augustine Mahiga, Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako, Waziri wa Afya Ummy Mwalimu na Mwakilishi wa Benki ya Dunia Tanzania Bi. Bella Bird.

Ninajizuia kuwabusu wasichana kwa sababu ni hatari kwa maisha yangu

22-year-old Oli Weatherall who has a severe peanut allergy pichaOLI WEATHERALL
Image captionOli Weatherall

Kuna sababu kadhaa zinazoweza kumzuia mtu kubusu – kufa kawaida sio moja ya sababu hizo.

Lakini kwa Oli Weatherall ni kitu cha kumtia wasi wasi mkubwa pamoja na safari za saa nyingi na kula hotelini.

Mwanmume huyo wa miaka 22 kutoka Surrey hukumbwa na madhara mabaya sana mara alapo njugu.

Wakati akiwa mtoto madhara yatokanayo na njugu yalisababisha alazwe hospitalini. Alisema mate yake yaliganda hadi kusababisha asipumue vizuri.

Tangu wakati huo maisha yake yamebadilika kabisa.

Oli's allergy means simply taking medication after coming in to contact with nuts might not be enough to save his life.Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionHata matibabu baada ya kula njugu haitoshi kuokoa maisha yake

Oli anakumbuka wakati wa kwanza alikimbizwa hospitalini baada ya kula mafuta ya njugu kama kisa kibaya zaidi katika maisha yake.

Hakufahamu kile kilikuwa kinaendelea kwenye mwili wake na ngozi yake ilipata madhara mabaya sana.

Sio tu kitu rahisi kujiuzuia kula mafuta ya njugu. Hata kumbusu msichana ni kitu kinaweza kuwa hatari sana kwake.

Kama msichana amekula njugu au amekula chakula kina njugu inawez kuwa hatari.

“Watu washakufa kutokana na hilo,” Oli anasema.

“Ni hatari sana ambacho hata watu hawataamini kama hawana madhara kama hayo.

Oli makes his own food from scratch to avoid nuts and has started an Instagram page with allergy friendly, vegan recipes.Haki miliki ya pichaOLI WEATHERALL
Image captionOli hupika chakula chake mwenyewe kujizuia na njugu

Kula sehemu yoyote isipokuwa nyumbani ni tatizo.

Huku mikahawa ikiwa inahitaji kufahamu kuhusu madhara ya vyakula ni kipi kilicho kwenye chakula chao, Oli anasema mameneja wasio na ujuzia na wahudumu wanaweza kuyafanya maisha kuwa magumu.

Inamaanisha kuwa kila mara akiwa nje kwa saa chache ni lazima apange mlo wake vilivyo.

Maisha yake mengi ni lazima yapangwe kuweza kula kwa njia salama.

Oli finds going on holiday with an allergy exhausting and isn't planning on doing it again any time soon.Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionOli hupata safari za kigeni kuwa zenye changamoto sana

Safari za nje ya nchi hazifanyiki kwa sasa pia. Mwanamume huyu anasema kuwa hilo pia linaweza kuwa hatari sana.

Sio tu chakula kwenye ndege. Lakini pia kutoelewa vizuri lugha ya sehemu fulani inaweza kuwa hatari sana kwa maisha.

Mashirika ya ndege yana vifaa vya matibabu na wahaudumu wamepewa mafunzo ya huduma za kwanza lakini Oli ana hofu kuwa hilo halitoshi.

Jamal Khashoggi: Mwendesha Mashtaka Saudia ataka waliomuua mwanahabari wapatiwe adhabu ya kifo

Khashoggi

Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu nchini Saudi Arabia imemaliza uchunguzi wake juu ya nani aliyeamuru kuuawa kwa mwanahabari Jamal Khashoggi na kufikia kikomo kuwa haikuwa Mwanamfalme Mohammed bin Salman.

Uchunguzi huo umebaini kuwa mauaji hayo yaliamuriwa na afisa mwandawizi wa idara ya usalama wa taifa ya Saudia ambaye alipewa kazi ya kumshawishi Khashoggi kurejea Saudia. Mwanahabari huyo ambaye alikuwa kinara wa kumkosoa Bin Salman alikimbia Saudia mwaka 2017 na kuhamia Marekani.

Kwa mujibu wa msemaji wa ofisi hiyo, Khashoggi alidungwa sindano ya sumu baada ya purukushani kuibuka ndani ya ofisi ndogo za ubalozi wa nchi hiyo jijini Istanbul, Oktoba 2, 2018.

Watu 11 tayari wameshafunguliwa mashtaka kutokana na mkasa huo na waendesha mashtaka wanataka watano kati yao kupatiwa adhabu ya kifo. Uchunguzi unaendelea kwa watu wengine 10 ambao wanshukiwa kushiriki mauaji hayo.

Katika mkutano na waandishi wa habari, Naibu Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Saudia Shalaan bin Rajih Shalaan amesema mwili wa Khashoggi ulikatwa katwa ndani ya ubalozi baada ya kuuawa.

Vipande hivyo vya mwili vilikabidhiwa kwa mshirika wao ambaye ni raia wa Uturuki nje ya ubalozi. Tayari picha ya kuchora ya mshirika huyo imetolewa na uchunguzi unaendelea kujua vipande hivyo vya mwili vilipelekwa wapi.

Bwana Shalaan hata hivyo hakuwataja wale ambao wamefunguliwa mashtaka juu ya tukio hilo.

A man wearing a mask of Saudi Crown Prince Mohammed bin Salman at a protest outside the Saudi consulate in Istanbul, Turkey (25 October 2018)Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionWaandamanaji wakionesha hisia kali kuwa Mwanamfalme Mohammed bin Salman anahusika na mauaji

“Uchunguzi wetu umebaini kuwa aliyeamuru mauaji ni kiongozi wa timu ya ushawishi aliyetumwa Istanbul na Naibu Mkurugenzi wa Usalama Generali Ahmed al-Assiri kumtaka Khashoggi kurudi nyumbani,” amesema Shalaan.

“Mwanamfalme bin Salman hakuwa na taarifa yeyote ya kilichokuwa kinaendelea,” alisisitiza.

Mwanamfalme Mohammed, ambaye ni mtoto wa Mfalme Salman ndiye anayetawala nchi ya Saudia kutokana na baba yake kuwa mgonjwa amejitetea kuwa hakushiriki kwa namna yeyote ile. Na pia amesema mauaji hayo ni “kosa kubwa la jinai ambalo halina utetezi”.

Wakosoaji wake hata hivyo wanasema kuwa uwezekano ni mdogo sana kuwa hakuwa na taarifa juu ya operesheni hiyo.

KhashoggiHaki miliki ya pichaEPA
Image captionPicha za watu wanaoaminika kushiriki operesheni ya kumuua Khashoggi

Watu 21 waliokamatwa kutokana na tukio hilo wamekuwa wakionekana katika shughuli mbali mbali za kiusalama za Saudia. General Assiri na kigogo mwengine Saud al-Qahtani wamefutwa kazi kutokana na tukio hilo.

Shalaan amesema Qahtani amezuiwa kutoka nje ya Saudia na anaendelea kuchunguzwa. Hata hivyo hakusema chochote kuhusu Generali Assiri.

Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan amesema “amri ya kumuua Khashoggi imetoka kwenye mamlaka za juu kabisa za serikali ya Saudia” lakini haamini kuwa ilitolewa na Mfalme Salman.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Mevlut Cavusoglu hata hivyo amesema baadhi ya kauli za Shalaan haziridhishi.

“Wanasema mtu huyu aliuawa sababu alipambana, lakini mauaji hayo yalipangwa kabla,” aliwaambia waandishi.

KhashoggiHaki miliki ya pichaAFP/GETTY

“Tena,wanasema mwili wake ulikatwa katwa…lakini hili si jambo la kukurupuka. Vifaa vya kutekeleza hilo na watu wa kulifanya waliingizwa nchini na baadaye kutekeleza.”

Maafisa wa Uturuki awali walisema kuwa mmoja wa maafisa usalama 15 wa Saudia walioingia Uturuki kumuua Khashoggi alikuwemo mtaalamu wa kuchunguza sababu ya vifo ambaye aliingia nchini humo na msumeno.

“Wale ambao walitoa amri na kuchochea watajwe na mchakato huu usizibwe,” amesema Cavusoglu na kuongeza kuwa Uturuki “itatoa mwangaza wa mauaji haya katika hatua zote.”

Denmark yasitisha msaada Tanzania kutokana na kauli dhidi ya wapenzi wa jinsia moja

Danish Minister for Development Cooperation Ulla Tornaes addresses the media in Dhaka, Bangladesh 31 October 2018.
Image captionWaziri wa Ushirikiano wa Maendelo wa Denmark Ulla Tornaes amesitisha ziara yake nchini Tanzania

Nchi ya Denmark imezuia krone milioni 65 ($9.8 milioni) ambazo zilikuwa ni msaada kwa Tanzania baada ya kutolewa “kauli zisizokubalika dhidi ya wapenzi wa jinsia moja” kutoka kwa mwanasiasa mwandamizi.

Hatua hiyo ya Denmark imetangazwa na waziri wake wa Ushirikiano wa Maendeleo Ulla Tornaes. Bi Tornaes hata hivyo hakumtaja kwa jina mwanasiasa mwandamizi wa Tanzania aliyetoa kauli hiyo ambayo wanasema haikubaliki na kushtusha.

Mwezi uliopita, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, alitangaza operesheni dhidi ya wapenzi wa jinsia moja kwa kutaka watu wawaripoti polisi watu wote wanaojihusisha na vitendo hivyo.

Makonda pia alitangaza kamati maalum ambayo pamoja na shughuli nyengine ingeliangazia suala hilo la wapenzi wa jinsia moja.

Serikali hata hivyo ilijitenga na kauli hiyo ya Makonda kwa kudai alikuwa akitoa mtazamo wake na si sera rasmi ya nchi.

Kufanya ngono kinyume cha maumbile ni kosa la jinai nchini Tanzania na mtu akipatikana na hatia anaweza kuadhibiwa kifungo cha miaka 30 ama maisha jela. Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na kukazwa kamba dhidi ya watu wanaojihusisha na matendo hayo.

Mwaka 2017, aliyekuwa Naibu Waziri wa Afya alitetea tishio la kutaja listi ya wapenzi wa jinsia moja.

“Nimeshtushwa na mambo hasi yanayoendelea Tanzania. Hivi karibuni ni kauli imetolewa kauli isiyokubalika dhidi ya wapenzi wa jinsia moja na kamishna,” ameandika Bi Tornaes kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Twitter.

“Kutokana na hilo nimezuia msaada wa DKK 65m kuelekea nchi hiyo. Kuheshimu haki za binaadamu ni jambo kubwa kwa Denmark.”

Denmark ni nchi ya pili kwa kutoa misaada kwa Tanzania.

Waziri huyo pia amesitisha ziara yake nchini Tanzania, shirika la habari la nchi hiyo DR limeripoti.

Image captionMwezi uliopita Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam alitangaza kampeni dhidi ya wapenzi wa jinsia moja

Seeikali ya Tanzania bado haijatoa tamko lolote kuhusu hatua hiyo ya Denmark.

Makonda – ambaye ni mtu wa karibu na rais Magufuli- pia amesema alitaraji kuandamwa na nchi za magharibi kwa kauli yake na kuongeza: “Ni bora kuzikasirisha nchi za magharibi kuliko kumkasirisha Mungu.”

Wakati ikijitenga na kauli ya Makonda serikali ilisema “itaendelea kuheshimu haki zote za binaadamu kwa mujibu wa katiba na mikataba ya kimataifa.”

Awali mwanzoni mwa mwezi huu, watu 10 walikamatwa kwa kuandaa harusi ya wapenzi wa jinsia moja visiwani Zanzibar. Hatua hiyo ilipingwa vikali na mashirika ya haki za kibinaadamu

Mwanamke ajifungua mtoto baada ya kupandikizwa mfuko wa uzazi India

Meenakshi Valand mwananamke wa 12 duniani kujifungua mtoto baada ya kupandikizwa mfuko wa uzaziHaki miliki ya pichaGALAXY CARE HOSPITAL
Image captionMeenakshi Valand ni mwananamke wa 12 duniani kujifungua mtoto baada ya kupandikizwa mfuko wa uzazi

Meenakshi Valand ni mmoja kati ya watu wachache duniani ambao wamejaaliwa kupata watoto baada ya kupandikizwa mfuko wa uzazi.

Alikuwa na furaha isiyokuwa na kifani.

“Sikuweza kujizuia kulia baada ya kusikia sauti ya mwanangu akilia. Haya ni machozi ya furaha – Nimepoteza watoto sita katika kipindi cha miaka kadhaa iliyopita,” aliiambia BBC.

Mama huyo wa miaka 28-alijifungua mwezi uliyopita nchini India baada ya kupandikizwa mfuko wa uzazi wa mamake mzazi.

Katika miaka tisa ya ndoa yake, Meenakshi alizaa watoto wawili waliofariki, alipoteza wengine wanne katika uja uzito, hatua iliyomsababisha kukatika kwa mfuko wake wa uzazi.

Hali hiyo inajulikana kama Ashermans syndrome.

Lakini hakukata tamaa. “Nilitaka kuwa na mtoto wangu mwenyewe. Sikutaka kutumia mbinu nyingine yoyote.”

Kwa mujibu wa jarida la kimataifa la utafiti wa kisayansi, 15% ya watu hawana uwezo wa kuzaa na 3 kati ya 5% ya visa hivi husababishwa na matatizo ya mfuko wa uzazi.

Radha alizaliwa Oktoba kabla ya kufikisha wakati wa kuzaliwa akiwa na kilo 1.45Haki miliki ya pichaGALAXY CARE HOSPITAL
Image captionRadha alizaliwa Oktoba kabla ya kufikisha wakati wa kuzaliwa akiwa na kilo 1.45

Alimtembelea Dkt Shailesh Putambekar, mtaalamu wa upasuaji na upandikizaji wa mfuko wa uzazi katika hospitali ya Galaxy Care mjini Pune.

Wakati huo mama yake Sushila Ben alikuwa amejitolea kumpatia mfuko wake wa uzazi ili kumuezesha kupata mtoto.

Upandikizaji huo ulifanywa na kundi la wataalam 12 mwezi Mei mwaka 2017 na ulifanikiwa.

Lakini Januari mwaka huu alikabiliwa na changamoto nyingine baada ya hatua ya kuhamisha kijusi kukwama.

Hata hivyo utaratibu huo ulifanywa tena mwezi Aprili.

Wiki 20 baadae mwanawe Radha alizaliwa kabla ya kufikisha wakati wa kuzaliwa akiwa na kilo 1.45.

Dkt Putambekar alisema , “Meenakshi alianza kupata matatizo mengine ikiwa ni pamoja na shinikizo la damu hali ambayo ilitulazimu kumfanyia upasuaji wa dharura ili kumuokoa mama na mtoto.

Mtoto alizaliwa salama lakini kabla ya wakati na alikuwa na kilo 1.45 ”Lakini anaendelea vizuri hana neno”

Huu ilikuwa mfumu wa kwanza wa kuzalisha ambao ni wa 12 kote duniani.

Upandikizaji wa mfuko wa uzazi enzi hizi:

Kisa cha kwanza mtoto kuzaliwa kupitia upandikizaji wa kizazi kilifanyika nchini Uswidi mwaka 2014Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionKisa cha kwanza mtoto kuzaliwa kupitia upandikizaji wa kizazi kilifanyika nchini Sweden mwaka 2014

Upandikizaji wa mfuko wa uzazi umefanywa katika mataifa 10 ikiewemo: Sweden, Saudi Arabia, Uturuki, Marakani, Uchina na Jamhuri ya Czech, Brazil, Ujerumani, Serbia na India.

 • 2014 – Mwanamke kutoka mji wa Gothenburg, nchini Sweden alijifungua mtoto wa kiume kupitia utaratibu wa kupandikizwa mfuko wa uzazi.
 • Mwanamke huyo wa miaka 36 alipata mhisani wa miaka 60 aliyempatia kizazi.
 • 2017 – Mwanamke katika mji wa Dallas, Texas, alizaa mtoto kupitia mfumo wa upandikizaji wa mfuko uzazi nchini Marekani.
 • 2018 – Mwanamke alifanikiwa kujifungua mtoto wa kisichana kupitia upandikizaji wa mfuko wa uzazi kwa mara ya kwanza nchini India.
 • Watoto 12 wamezaliwa kupitia mfumo huo nane kati ya watoto hao wamezaliwa nchini Sweden.
 • Ni mwanamke mmoja tu kati ya 12 aliyepandikizwa kizazi cha mtu aliyekufa.

Mfumo huu unafanya kazi vipi?

Wakati wa upandikizaji wa mfuko wa uzazi mfumo wa neva haupandikizwi kwa hivyo mwanamke hapati uchungu wakati wa kujifungua mtoto.

Mfumo huu maalum ulipoanza ulikuwa ukichukua hadi saa 13 kufanywa. “Lakini sasa upandikizaji wa mfuko wa uzazi unachukua saa sita anasema Dkt Shailesh Puntambekar.

Mfumo wa upandikizaji wa kizazi umefanyika katika mataifa 10 kufikia sasaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMfumo wa upandikizaji wa kizazi umefanyika katika mataifa 10 kufikia sasa

Kwa mujibu wa kundi la wataalamu katika hospitali ya Galaxy Care, mfumo wa upandikizaji wa mfuko wa uzazi unagharimu karibu dola 11000.

Lakini katika kesi ya Meenakshi Wayanad ambayo ni ya kwanza na aina yake nchini India, hakutakiwa kulipa chochote.

Alipewa dawa za kudhibiti mfumo wa kinga mwilini ili kuzuia mfuko mpya wa uzazi kukataliwa.

Mwaka mmoja baada ya upandikizaji, madkatari waliamua kukipandikiza kijusi kilichokuwa kimegandishwa.

Wanasema upandikizaji unadhaniwa kuwa salama kwa mama na mtoto licha ya kutumiwa kwa dawa inayofahamika kama (immuno-suppressants) pamoja na kuhusishwa kwa upasuaji wa aina tofauti.

Nchini India pekee karibu wanawake 600 wamewekwa katika orodha ya watu wanaotaka kufanyika upandikizaji wa kizazi kipya

Awali njia ya pekee ambayo mwanamke aliye na tatizo la kizazi kupata mtoto ni kupitia mfumo wa kibiologia ambapo mwanamke mwingine anatumiwa kubeba mimba kwa niaba ya yule aliye na tatizo la kushika mimbaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionNjia ya pekee ya kupata kupata mtoto kwa walio na shida ni kupitia mwanamke mwingine anayebeba mimba kwa niaba ya yule aliye na tatizo la kushika mimba

Uchunguzi wa kimataifa kuhusiana na utaratibu wa kupandikiza mfuko wa uzazi umebaini kuwa utaratibu huo umepata ufanisi mkubwa lakini unahitaji majaribio ya kliniki ya kudhibiti kisaikolojia na ukaguzi katika ngazi kadhaa.

Wakichangia katika jarida la kimataifa la masuala ya uzazi kundi la madaktari kutoka Japan limesema huku utaratibu wa kupandikiza mfuko wa uzazi ukisifiwa kwa kuwapa faraja wanawake waliyo na tatizo la mfuko wa uzazi bado utaratibu huo unaendelea kufanyiwa majaribio.

Matumaini ndiyo kitu Meenakshi alikuwa akijipatia: “Nimeteseka sana lakini sasa nina furaha kupita maelezo.”

Utafiti umebaini kuwa wazazi hawana ufahamu kuhusu uwezekano wa watoto wao kuugua ugonjwa wa kisukari.

Mwanamke wa kisomali akimshikilia mtoto wake anayeugua kisukari Kaskazini Mashariki mwa KenyaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMwanamke wa kisomali akimshikilia mtoto wake anayeugua kisukari Kaskazini Mashariki mwa Kenya

Ulimwengu unapoadhimisha siku ya ugonjwa wa kisukari, utafiti uliyofanywa na shirikisho la kimataifa la ugonjwa wa kisukari (IDF) umebaini kuwa wanne kati ya wazazi watano hawana uwezo kung’amua dalili za mapema za ugonjwa huo kwa watoto wao.

Awali ugonjwa wa kisukari ulihusishwa na watu wanene na wazee lakini miaka ya hivi karibuni watoto wachanga pia wamejikuta wakikabiliwa na maradhi hayo.

Ili kufahamu kwanini watoto pia wanakabiliwa na ugonjwa huu BBC imezungumza na Farhia Mohammed kutoka mtaa wa Eastleigh jijini Nairobi, anayemuuguza mtoto wake wa miaka minane ambaye alipatikana na ugojwa wa kisukari akiwa mdogo.

Farhia anasema hana budi kumpikia chakula maalum mwanawe ili aweze kudhibiti kiwango cha sukari mwilini mwake.

”Nikiamka nafikiria kile kitu nitampatia, lazima iwe chakula asili, kama anaenda shule lazima apate mlo kamili”

Mtoto huyo aligunduliwa kuwa anaugua kisukari alipokuwa na miaka minne. Mama Farhia anasema hakuwa na ufahamu mwanawe anaugua kisukari

”Niliona mtoto anaenda msalani mara kwa mara hali ambayo nilihisi si ya kawaida”

Anasema alipompeleka hospitali hawakuruhusiwa kurudi nyumbani kwa sababu mtoto alihitajika kupewa matibabu ya dharura.

Vipimo vya sukari mwiliniHaki miliki ya pichaREUTERS

Lakini swali ni je ni kwanini watoto wanapatikana na maradhi ya kisukari wakiwa wadogo?

Abdisalan Mohammed ambaye ni daktari wa watoto anasema ugonjwa wa kisukari umekuwepo tangu zamani.

Anaongeza kuwa tofauti na miaka ya nyuma siku hizi kuna maabara ambayo wataalamu wanatumia kufanya utafiti ili kubaini ikiwa mtoto anaugua ugonjwa huo.

Dkt Abdisalan anasema”kwa kweli 10% ya ugonjwa wa kisukari unapatikana kwa watoto wachanga kwa hivyo watu wasifikirie kuwa huu ni ugonjwa wa watu wazima pekee”

Watoto hususan hupatikana na aina ya kwanza ya kisukari ambayo inahitaji mgonjwa kudungwa dawa ya insulin ili kudhibiti kiwango cha sukari mwilini.

Kisukari ni ugonjwa gani?

Kwa mujibu wa ripoti ya mwaka 2017 ya shirikisho la kimataifa la ugonjwa wa kisukari karibu watu milioni 15.5 waliyo na umri kati ya miaka 20-79 wanaishi na ugonjwa huo barani Afrika.

Ugonjwa wa kisukari hutokea pale kongosho (pancrease) inaposhindwa kutengeneza homoni au kichocheo aina ya Insulin, au pale mwili unaposhindwa kutumia vizuri kichocheo hicho.

Hali hiyo husababisha ongezeko la kiwango cha sukari kwenye damu (hyperglycemia).

Kazi ya Insulin ni kuondoa glucosei katika damu na kuingiza katika misuli, seli za mafuta na ini, ambako hutumiwa kama nishati.

Dkt Abdisalan anasema kuwa chakula kinapoyeyushwa matukio kadhaa hutokea ikiwa ni pamoja na sukari inayoitwa glucose ambayo ni chanzo cha nguvu mwilini kuingia katika damu.

Mwanamke akijipima uzaniHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Tukio la pili hutokea katika kiungo kinachoitwa kongosho (pancrease) ambacho hutengeneza kichocheo cha Insulin.

Kazi ya Insulin ni kuondoa glucosei katika damu na kuingiza katika misuli, seli za mafuta na ini, ambako hutumiwa kama nishati.

Kuna aina mbili kuu ya ugunjwa wa kisukari,

Aina ya kwanza ya kisukari

Mtu hupatikana na aina hii ya kisukari ikiwa seli maalumu zinazotengeneza homoni ya insulin zinapokosekana katika tezi kongosho.

Pia kongosho zinapoharibika kutokana na sababu yeyote ile husababisha ukosefu kabisa au upungufu wa kichocheo hicho kwenye damu.

Kwa mujibu wa wataalamu wa matibabu aina hii ya kisukari ni hatari sana.

Huwaathiri zaidi watoto na vijana

Aina ya pili ya kisukari

Katika aina hii ya kisukari, insulin huzalishwa kwa kiwango cha kutosha isipokuwa tatizo lipo kwenye ufanisi na utendaji kazi wake.

Upungufu wa mazoezi ni hatari kwa afya ya mwanadamuHaki miliki ya pichaEMPICS
Image captionUpungufu wa mazoezi ni hatari kwa afya ya mwanadamu

Mara nyingi mtu hupatikana na aina hii kisukari ukubwani.

Hii inatokana na kupungua kwa utendaji kazi wa homoni ya insulin, au seli kushindwa kutumia insulin ipasavyo.

Hali hii mara nyingi husababishwa na unene uliopitiliza, au hali ya kutofanya mazoezi kabisa.

DALILI ZA UGONJWA WA KISUKARI

 • Kukojoa mara kwa mara
 • Kuhisi kiu kali na kunywa maji kwa kiwango cha kupitiliza (polydipsia).
 • Kuhisi njaa na kula mara kwa mara (polyphagia).
 • Kuchoka haraka
 • Kupungua uzito
 • Vipele mwilini
 • Kutoa harufu ya acetone inayofanana na harufu ya pombe.
 • kuhisi maumivu ya tumbo na kupoteza fahamu

Mtu anayeugua kisukari huwa na kiwango cha juu vya sukari kwenye damu kwa sababu mwili wake hauwezi kupeleka sukari kwenye seli za mafuta, ini na misuli ili ihifadhiwe kwa ajili ya kuzalisha nguvu.

Hali hali ya kuwa na kiwango cha juu cha sukari kwenye damu huenda ikaharibu moyo, macho, miguu na figo

Hata hivyo tiba maalum na uangalizi mzuri kwa watu wanaougua kisukari inaweza kuwahakikishia maisha marefu yenye afya

Rais Magufuli asema hatochoka kubadili mawaziri

Magufuli

Rais wa Tanzania John Pombe Magfuli amesema hatachoka kufanya mabadiliko ya baraza lake la mawaziri kila itakapohitajika.

Ndani ya miaka mitatu ya uongozi wake, tayari Magufuli ameshafukuza kazi mawaziri tisa kati ya 19 aliowateua Desemba 10, 2015.

Akizungumza leo Ikulu katika hafla ya kuwaapisha mawaziri wapya, Rais Magufuli amesema ataendelea kufanya mabadiliko ya baraza lae pale patakapokuwa na uhitaji wa kufanya hivyo.

“…hii ni kama safari, sio lazima wote tufike. Inawezekana hata mie kiongozi nisisfike lakini lengo letu lazima litimie,” amesema Magufuli.

Mawaziri wapya walioapishwa leo ni Japhet Hasunga kuwa Waziri wa Kilimo na Joseph Kakunda kuwa Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji.

Ambao wametimuliwa katika nafasi hizo ni Dkt. Charles Tizeba na Charles Mwijage mtawalia.

Mawaziri hao wawili wamekuwa wahanga wa sakata la korosho lakini kwamujibu wa Magufuli utendaji wao wa kazi ulikuwa unamkwaza siku nyingi.

Magufuli, Majaliwa, TizebaHaki miliki ya pichaIKULU
Image captionCharles Tizeba (kushoto) ametimuliwa katika nafasi yake ya uwaziri wa kilimo.

Magufuli ‘alipovamia’ mkutano kati ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na wanunuzi wa sekta binafsi tarehe 28 Septemba aligundua ‘madudu’ mengi ambayo yangeweza kutatuliwa na wizara hizo mbili na bodi ya korosho lakini hawakufanya hivyo mapema.

“Kwenye mkutano ule nilikuta bodi ya korosho imetoa bei elekezi ya Sh1,500, iliniumiza sana…lakini mwisho wa yote unajiuliza wizara ya kilimo ipo wapi? Au Mwijage nae alikuwa tu na viwanda akasahau wafanyabiashara ya korosho.”

Katika mkutano wa Oktoba 28, Magufuli na wafanyabiashara walikubaliana bei elekezi ya Sh3,000 lakini utekelezaji wake ulisuasua. “Sikuona tamko lolote kutoka kwa Waziri wa Kilimo au Biashara kukemea kile ambacho kilikuwa kinaendelea, mpaka ikabidi nimtume Waziri Mkuu awape wanunuzi siku nne tu wafanye maamuzi.”

‘Kila Kitu Waziri Mkuu’

Magufuli pia ameiambia hadhara iliyokuwepo ikulu kuwa alishawahi kumwambia Waziri Mkuu kuwa atamfanya kuwa Waziri wa Kilimo kutokana na kutatua changamoto nyingi za wiazara hiyo.

“Kulipokuwa na shida ya bei ya kahawa mkoani Kagera, ilibidi Waziri Mkuu aende akalimaliza ndani ya moda mfupi. Sasa najiuliza Mwijage hakuliona hili na yupo karibu, lakini kahawa nizao la kilimo hawakuchua hatua pia.”

Magufuli na MajaliwaHaki miliki ya pichaIKULU
Image captionRais Magufuli na Waziri Mkuu Majaliwa walipokutana na wanunuzi wa korosho Oktoba 28

Waziri Majaliwa alienda Kagera mwezi Oktoba na kutangaza mfumo mpya wa minanda ya kahawa na kumaliza sakata hilo.

Changamoto nyengine ilikuwa ya kiwanda cha chai cha Mponde Tanga ambacho kilikuwa hakifanyi kazi kwa zaidi ya miaka mitano lakini Majaliwa akamaliza mgogoro wake mapema mwezi huu.

“Sio kama siwapendi, nampenda Tizeba nataniana na Mwijage lakini katika hili nimeona siwezi tena kuwasukuma, nitawavunja miguu. Wacha hawa wapya waje waendane na spidi.”

Mawaziri Waliotoswa

Mwezi Mei 2016, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani Charles Kitwanga alifutwa kazi kwa tuhuma za kuingia Bungeni akiwa amelewa.

Mawaziri wawili Profesa Sospeter Muhongo (Nishati na Madini) George Simbachawene (Ofisi ya Rais) walifutwa kazi kufuatia sakata la mchanga wa madini (makinikia) wa kampuni ya Acacia.

Julai mosi mwaka huu Mwigulu Nchemba alitolewa kwenye nafasi ya uwaziri wa Mambo ya Ndani. Rais Magufuli alitaja sababu 13 kumwondoa Mwigulu ikiwemo ajali za barabarani na matumizi mabaya ya fedha za Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa.

Mwezi Machi 2017 Nape Nnauye aliyekuwa Waziri wa Habari alitimuliwa kazi. Mkuu wa Mko wa Dar es Salaam, Paul Makonda alivamia Kituo cha Televisheni cha Clouds akiwa na askari wenye silaha akitaka kipindi anachotaka yeye kirushwe hewani.

Je Paul Makonda anapendelewa na serikali Tanzania?

Nape akiwa kama waziri mwenye dhamana, akaitisha uchunguzi huru wa tukio hilo. Ripoti ya uchunguzi huo ilimtia lawani Makonda.

Nape aliahidi kuifikisha ripoti hiyo kwa Rais, lakini hatimaye alifutwa kazi, na badala yake Magufuli, mbele ya hadhara akamsihi Makonda ” piga kazi” na kusema yeye Rais hapangiwi nini cha kufanya.

Mawaziri wengine waliotimuliwa kazi ni Prof Jumanne Maghembe (Maliasili na Utalii) na Gerson Lwenge (Maji na Umwagiliaji).

Magufuli aamuru Jeshi kukusanya korosho kutoka kwa wakulima, wanunuzi wafungiwa

Wakulima wa korosho

Rais wa Tanzania John Magufuli amesema kwamba kuanzia Jumatatu wanunuzi wa korosho hawaruhusiwi tena kununua bidhaa hiyo kutoka kwa wakulima.

Serikali sasa iko tayari kununua korosho hizo kwa gharama ya shilingi 3,300 badala ya shilingi 3000 za kitanzania ambayo ni sawa na dola 1.4.

Na kukabidhi rasmi kwa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kuzichukua korosho hizo.

Mzozo huu wa korosho umekuwa gumzo kubwa Tanzania kwasababu korosho zina umuhimu mkubwa kutokana na kuwa usafirishaji wake katika nchi za nje ndio mojawapo ya kitega uchumi nchini humo.

Siku ya Jumamosi rais Magufuli alisema kuwa endapo wanunuzi binafsi hawatatii maagizo ya Serikali ifikapo Jumatatu tarehe 12 Novemba, 2018 saa 10:00 Jioni basi hawatanunua tena korosho, jambo ambalo limetimia lakini alitamka hayo majira ya saa tano na nusu asubuhi.

Pamoja na uamuzi huo, rais Magufuli amelikabidhi jeshi kiwanda kimoja cha korosho kilichokuwa kinamilikiwa na mtu binafsi kinachofahamika kama ‘Bucco’. Kiwanda hicho kilibinafsishwa miaka kadhaa iliyopita lakini muwekezaji wake hakutimiza masharti na serikali ilikitwaa wiki iliyopita.

magufuliHaki miliki ya pichaAFP

Amesema kiwanda hicho kina uwezo kwa kutengeneza korosho mpaka kilo 20 elfu kwa mwaka hivyo hizo tani hizo 70 elfu ni kidogo sana kazi za wanajeshi.

“Na kuanzia leo wanajeshi inabidi wakakizingire na wakishindwa watapewa watu wengine” Rais Magufuli amesisitiza.

Soko la Korosho Kimataifa

Rais Magufuli ameongeza kwa kusisitiza kuwa ameangalia soko la korosho na korosho za Tanzania ni za kiwango cha juu.

Na Tanzania ina uwezo wa kupata tani 210,00 kwa mwaka huu.

Tayari Rais Magufuli amewafuta kazi mawaziri wa wiwili Waziri wa Kilimo Charles Tizeba na mwenzake wa Viwanda , biashara na uwekezaji wawefutwa kazi kufuatia sakata hilo. Pia amevunja Bodi ya Korosho na kutengua uteuzi wa mwenyekiti wa bodi hiyo.

koroshoHaki miliki ya pichaISSOUF SANOGO

Kwa upande wao wakulima, BBC ilizungumza na mmoja wa mfanyabiashara na mkulima wa zao la korosho ambaye alisifu umuhimu wa korosho katika uchumi wa mkoa wa Mtwara.

Alibainisha kwamba korosho inatoa ajira za muda katika mkoa huo lakini mfumo uliokuepo ulikuwa unarudisha nyuma mauzo na kuwafanya wakulima kushindwa kupata faida.

Na kwa upande wao wanunuzi wa zao hilo walishindwa kufikia bei ambayo wangeweza hata kuuuza mwaka jana.

Korosho zaondoka na mawaziri wawili Tanzania

Mnamo mwezi Juni mjadala mkali ulizuka nchini Tanzania kuhusu mapendekezo ya bajeti ya mwaka 2018 /2019 katika zao la korosho. Mapendekezo hayo ni pamoja na kuondolewa kwa ruzuku ya asilimia 65 iliyokuwa inaenda kwenye Mfuko wa Maendeleo wa Korosho na badala yake, iende kwenye mfuko mkuu wa serikali.

Chama cha ushirika kilibainisha tatizo lililopo la teknolojia ya kunyunyizia na utegemezi wa pembejeo kutoka nje.

Kwa takribani miaka 10, korosho imekuwa zao lililoleta matokeo chanya ambapo tangu mwaka 2007/08 bei ilikuwa shilingi 250 mpaka 500 kwa kilo ila sasa hivi wastani ni shilingi 3000 mpaka 5000 kwa kilo.

Wafanyabiashara wa korosho wakimsikiliza Rais Magufuli Septemba 28
Image captionWafanyabiashara wa korosho wakimsikiliza Rais Magufuli

Msimamo wa serikali kuhusu bei ya korosho

Ingawa mwezi Oktoba tarehe 28, 2018 baada ya serikali ya Tanzania kufanya mazungumzo na wanunuzi wa zao la korosho, Serikali ililazimika kuchukua hatua ya kuwalazimisha wanunuzi kununua korosho hizo na hata kutishia kuwafutia leseni wafanyabiashara hao.

Katika mazungumzo hayo Serikali iliungana na msimamo wa wakulima wa korosho wa kukataa bei ya kati ya shilingi 1,900 hadi 2,700 kwa kilo, na hivyo kukubaliana kuwa korosho zitanunuliwa kwa bei isiyopungua shilingi 3,000 kwa kilo.

Na mtaalamu wa uchumi na biashara nchini Tanzania, Johakim Bonaventure anasema serikali imeamua kutekeleza sera ya kuweza kuhodhi ile kodi ya kuuza nje, mwanzoni ilikuwa inahozi kwa asilimia 35 ya kipato hicho lakini sasa hivi imechukua na ile asilimia 65.

‘Ni jambo jema lakini kiuchumi kuna mambo kadhaa ambayo yanaweza kuwa yameandamana nayo na mojawapo ni kupunguza uwezo wa vyombo vinavyosimamia mazao sio korosho pekee yanayolimwa katika baadhi ya maeneo.’

Mtaalamu huyo amesema kama zao la korosho likiweza kuathirika basi pato linaweza kuathirika pia.Bado kuna uwezekano wa kukaa chini kuangalia faida na hasara.

Mwaka jana zao la korosho limeweza kuleta mapato makubwa katika taifa na sasa linatangazwa kuanzishwa katika maeneo mengine 17.

Bobi Wine: Nyota wa muziki wa pop na mbunge afanya tamasha la kwanza tangu akamatwe

Bobi Wine appears on stage on the outskirts of Kampala
Image captionBobi Wine

Nyota wa muziki wa pop na mbunge wa upinzani nchini Uganda Bobi Wine amefanya tamasha lake kwanza tangu ashtakiwe na kufungwa kwa mshtaka ya uhaini.

Kulikuwa na idadi kubwa ya polisi kwenye tamasha hilo, ambalo liliruhusiwa tu kufanyika kwa sababu halikuwa la kisiasa.

Bobi Wine anadaiwa kuteswa na kupigwa akiwa kuzuizi mwezi Agosti, madai yanayokanwa na mamlaka.

Umaarufu wake miongoni mwa vijana nchini Uganda unaonekana kuwa changamoto kubwa kwa rais wa miaka mingi Yoweri Museveni.

Baadhi ya maelfu ya watu waliohudhuria tamasha walivaa nguo nyekundu, rangi inayohusishwa na vuguvugu la Bobi Wine la People Power.

“Ninashukuru polisi wa Uganda kwa kutupa ulinzi na kutotuzuia kama vile wamekuwa wakifanya awali,” Bobi Wine aliuambia umati kwa mujibu wa AFP.

“Sisi ni watu wenye amani na tunataka kusikilizwa.”

Mbunge huyo mwenye miaka 36 ambaye jina lake kamili ni Robert Kyagulanyi, aliwania na kushinda kama mgombea huru kwenye uchaguzi mdogo huko Kyadondo East kati kati mwa Uganda

Mwezi Agosti yeye pamoja na wanasiasa wengine 30 wa upinzani walishtakiwa kwa uhaini baada ya msafara wa rais kutupiwa mawe baada ya mkutano wa kampeni.

Aliondoka nchini Uganda kwenda kupata matibabu nchini Marekani kufuatia majeraha aliyoyapata akiwa kizuizini lakini akarudi nyumbani mwezi Septemba.

Idadi kubwa ya watu nchini Uganda wako chini ya miaka 35 na Wine amekuwa kama mfano wa vijana wenye ghadhabu ya ukosefu wa ajira na siasa zilizokwama.

Bobi Wine alizaliwa miaka minne kabla ya Bw Museveni kuwa rais mwaka 1986 na amekuwa akitoa wito kwa Museveni astaafu kutokana kwa siasa za mwaka 2021.

Bobi Wine appears on stage on the outskirts of KampalaHaki miliki ya pichaAFP
Image captionTamasha hilo lilifuatiliwa kwa karibu na polisi
Fans attend a Bobi Wine concert in UgandaHaki miliki ya pichaAFP
Image captionMaelfu walihudhuria tamasha katika vitongoji vya mji wa Kampala
Bobi Wine appears on stage on the outskirts of KampalaHaki miliki ya pichaAFP
Image captionBobi Wine amelkuwa mfano kuigwa na vijana wa Uganda

Mlipuko wa sasa wa Ebola ndio mbaya zaidi katika historia nchini DRC karibu 200 wafariki tangu Agosti

A health worker administers Ebola vaccine to a boy in the village of Mangina in North Kivu province, August 18, 2018
Image captionWatoa huduma za afya kwa sasa wanawachanja watu kuzuia kusambaa ugonjwa huo

Mlipuko wa saa wa Ebola nchini Jamhuri ya Demokrasi ya Congo ndio mbaya zaidi zaidi kuwai kutokea katika historia ya nchi hiyo, kwa mujibu wa wizara ya afya.

Karibu watu 200 wamefariki dunia tangu Agosti, kwa mujibu wa maafisa, huku zaidi ya 300 wakithibitishwa kuambukizwa ugonjwa huo.

Congo imekumbwa na misukosuko ya miaka mingi na jitihada za kukukabiliana ugonjwa huo zimetatizwa na mashambulizi dhidi ya watoa huduma za afya.

Wakati huu visa 319 vimeandikishwa na pia vifo 198, waziri wa afya Oly Ilunga alisema.

Karibu nusu ya waaathiriwa ni kutoka mji wa Beni, mji wenye wakaazi 800,000 eneo la Kivu Kaskazini, kwa mujibu wa halmashauri ya kitaifa ya afya.

Mlipuko wa sasa ndio wa kumi kuikumba Congo na mbaya zaidi tangu ule wa kwanza wa mwaka 1976.

Mlipuko wa mwaka 1976 kwa kile kilikuwa ugonjwa usiojulikana ulizua wasi wasi mkubwa lakini ulidhibitiwa na wataalamu walioutambua kwa haraka.

Ebola husambaaa kupitia maji maji ya mwila na mara nyingi huwa hatari sana kwa maisha