Baby Pendo: Makamanda 5 wa polisi wana kesi ya kujibu Kenya

Ghasia za uchaguzi za mwaka 2017

Makamanda watano wa polisi walioongoza operesheni ya 2017 ambapo mtoto kwa jina baby Pendo aliuawa mjini Nyalenda kaunti ya Kisumu wa nakesi ya kujibu ya kifo chake.

Uchunguzi ulioongozwa na hakimu mwandamizi Beryl Omollo ulitoa uamuzi huo siku ya Alhamisi mjini Kisumu.

Makamanda hao ni Linah Kosgei, Benjamin Koima, Christopher Mutune Maweu, Titus Yoma na John Thiringi.

Wakati wa operesheni hiyo iliokumbwa na utata Bwana Yoma alikuwa kamanda wa polisi wa kaunti ya Kisumu, Bwana Maweu alikuwa OSPD wa Kisumu Mashariki, bwana Thiringi alikuwa OSC wa kisumu ya kati huku Koima akisimamia Kisumu magharibi huku naye bi Kosgei akiongoza kituo ha polisi cha Nyalenda.

Mtoto huyo aliyekuwa na miezi sita aliuawa ndani ya nyumba ya babake na maafisa wa polisi wa kitengo cha kukabiliana na ghasia ambao walikuwa wakijaribu kuzima maandamno yalioanza kufuatia matokeo ya uchaguzi wa 2017.

Babake baby Samantha Pendo Joseph Abanja
Image captionBabake baby Samantha Pendo Joseph Abanja, ameelezea furaha yake kuhsu hukumu hiyo.

Babake baby Samantha Pendo Joseph Abanja, ameelezea furaha yake kuhusu hukumu hiyo.

“Nimefurahi mno na naskia roho imetulia. Tumepata haki tuliokuwa tukitafuta, lakini kuna watu wengine wengi nchini kenya ambao hawajapata haki yao, kwa hivyo bado safari ni ndefu. Lakini nimefurahia uamuzi huu. Tuna imani na idara ya mahakama.”

Katika uamuzi wake, hakimu pia alimuagiza mkurugenzi wa mashtaka Noordin Haji kuwachunguza maafisa 31 wa kikosi cha GSU ambao aliwataja kuwa ‘washukiwa muhimu’.

Maafisa wengine 20 wa polisi ambao walikuwa chini ya usimamizi wa Kosgei mjini Nyalenda pia watachunguzwa mahakama hiyo iliamuru.

Kifo

Wazazi wake Bwana Joseph Abanja na mkewe Lencer Achieng, walisema kuwa walikuwa wakiomba maajabu ya Valentines na ni hicho walichopata.

Na wakati wa kusikizwa kwa kesi hiyo makamanda hao walilaumiana huku hakuna hata mmoja akitaka kuchukuwa lawama.

Wakati mwengine maafisa hao walitaka kushikana mashati mahakamani.

Baby pendo alifariki mnamo mwezi Agosti 2017, baada ya kdaiwa kupigwa katika kichwa na maafisa wa polisi kufuatia ghasia zilizokumba kaunti ya Kisumu baada ya raia Uhuru Kenyatta kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais.

Maafisa wa polisi walishutumiwa kwa kuvunja na kuingia katika nyumba ya bwana Abinja katika mtaa wa mabanda wa Nyalenda.

Mtoto huyo alifairiki siku tatu baadaye wakati alipokuwa akipatiwa matibabu katika hospitali ya Aga Khan.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *