Baby Pendo: Makamanda 5 wa polisi wana kesi ya kujibu Kenya

Ghasia za uchaguzi za mwaka 2017

Makamanda watano wa polisi walioongoza operesheni ya 2017 ambapo mtoto kwa jina baby Pendo aliuawa mjini Nyalenda kaunti ya Kisumu wa nakesi ya kujibu ya kifo chake.

Uchunguzi ulioongozwa na hakimu mwandamizi Beryl Omollo ulitoa uamuzi huo siku ya Alhamisi mjini Kisumu.

Makamanda hao ni Linah Kosgei, Benjamin Koima, Christopher Mutune Maweu, Titus Yoma na John Thiringi.

Wakati wa operesheni hiyo iliokumbwa na utata Bwana Yoma alikuwa kamanda wa polisi wa kaunti ya Kisumu, Bwana Maweu alikuwa OSPD wa Kisumu Mashariki, bwana Thiringi alikuwa OSC wa kisumu ya kati huku Koima akisimamia Kisumu magharibi huku naye bi Kosgei akiongoza kituo ha polisi cha Nyalenda.

Mtoto huyo aliyekuwa na miezi sita aliuawa ndani ya nyumba ya babake na maafisa wa polisi wa kitengo cha kukabiliana na ghasia ambao walikuwa wakijaribu kuzima maandamno yalioanza kufuatia matokeo ya uchaguzi wa 2017.

Babake baby Samantha Pendo Joseph Abanja
Image captionBabake baby Samantha Pendo Joseph Abanja, ameelezea furaha yake kuhsu hukumu hiyo.

Babake baby Samantha Pendo Joseph Abanja, ameelezea furaha yake kuhusu hukumu hiyo.

“Nimefurahi mno na naskia roho imetulia. Tumepata haki tuliokuwa tukitafuta, lakini kuna watu wengine wengi nchini kenya ambao hawajapata haki yao, kwa hivyo bado safari ni ndefu. Lakini nimefurahia uamuzi huu. Tuna imani na idara ya mahakama.”

Katika uamuzi wake, hakimu pia alimuagiza mkurugenzi wa mashtaka Noordin Haji kuwachunguza maafisa 31 wa kikosi cha GSU ambao aliwataja kuwa ‘washukiwa muhimu’.

Maafisa wengine 20 wa polisi ambao walikuwa chini ya usimamizi wa Kosgei mjini Nyalenda pia watachunguzwa mahakama hiyo iliamuru.

Kifo

Wazazi wake Bwana Joseph Abanja na mkewe Lencer Achieng, walisema kuwa walikuwa wakiomba maajabu ya Valentines na ni hicho walichopata.

Na wakati wa kusikizwa kwa kesi hiyo makamanda hao walilaumiana huku hakuna hata mmoja akitaka kuchukuwa lawama.

Wakati mwengine maafisa hao walitaka kushikana mashati mahakamani.

Baby pendo alifariki mnamo mwezi Agosti 2017, baada ya kdaiwa kupigwa katika kichwa na maafisa wa polisi kufuatia ghasia zilizokumba kaunti ya Kisumu baada ya raia Uhuru Kenyatta kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais.

Maafisa wa polisi walishutumiwa kwa kuvunja na kuingia katika nyumba ya bwana Abinja katika mtaa wa mabanda wa Nyalenda.

Mtoto huyo alifairiki siku tatu baadaye wakati alipokuwa akipatiwa matibabu katika hospitali ya Aga Khan.

Tetesi za soka Ulaya Jumanne 05.02.2019: Insigne, Pogba, Rashford, Hudson-Odoi

Lorenzo InsigneHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Liverpool imewasilisha ombi la takriban Euro milioni 70 kwa mshambulaiji wa Napoli Lorenzo Insigne, mwenye umri wa miaka 27. (La Repubblica kupitia Sport Witness)

Bayern Munich itarudi na ombi la £ milioni 35 kwa winga wa Chelsea Callum Hudson-Odoi, mwenye umri wa miaka 18, katika msimu wa joto baada ya kushindwa kumsajili mchezaji huyo wa timu ya England ya wachezaji wa chini ya miaka 19 mwezi Januari. (Mail)

Mshambuliaji wa Manchester United Marcus Rashford, mwenye umri wa miaka 21, anafanya mazungumzo kuhusu mkataba mpya katika klabu hiyo ambayo huenda yakaongeza mshahara wake kwa mara mbili hadi zaidi ya £150,000 kwa wiki. (Telegraph)

Mchezaji wa kiungo cha kati wa United Paul Pogba aliwahi kutafakari kuondoka katika klabu chini ya mkufunzi wa zamani Jose Mourinho, kwa mujibu wa kakake, Mathias. (Telefoot kupitia Mirror)

Mshambuliaji wa Tottenham Vincent Janssen, mwenye umri wa 24, ameambiwa na meneja Mauricio Pochettino kwamba atajumuishwa katika kikosi cha timu hiyo katika ligi kuu ya England, licha ya kutojumuishwa katika timu ya Spurs tangu Agosti 2017. (Evening Standard)

PogbaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Meneja wa Arsenal, Unai Emery atakuwa na £40 milioni pekee kutumia msimu wa joto, baada ya kushindwa kusajili mchezaji kwa mkataba wa kudumu mwezi Januari. (Mirror)

Emery anataka kusaini angalau wachezaji watatu wapya msimu wa joto, akiwemo beki wa kushoto. (Mail)

Gunners wamekuwa wakimsaka beki wa kati wa Red Bull Leipzig raia wa Ufaransa Ibrahima Konate, mwenye umri wa miaka 19. (Bild – kupitia ESPN)

Mkataba wa mkopo wa mchezaji wa kiungo cha mbele wa Fulham Andre Schurrle kutoka Borussia Dortmund utamalizika msimu wa joto – mwaka mmoja mapema kuliko ilivyopangwa – iwapo timu hiyo ya Cottagers itashushwa daraja kutoka ligi kuu ya England. (Kicker – Kijerumani)

Hertha Berlin inataka kuendelea kuwa na mchezaji wa kiungo cha kati wa Liverpool Marko Grujic, mwenye umri wa miaka 22, kwa mkopo kupita hata baada ya mwisho wa msimu. (Liverpool Echo)

Mkataba wa mkopo wa Andre Schurrle kutoka Borussia Dortmund utamalizika msimu wa jotoHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMkataba wa mkopo wa Andre Schurrle kutoka Borussia Dortmund utamalizika msimu wa joto

Barcelona inataka kumsajili mchezaji wa Ajax mwenye umri wa miaka 19 Matthijs de Ligt katika msimu wa joto na itabidi ilipe euro milioni 75. (Mundo Deportivo Kihispania)

Cristiano Ronaldo amemeuita aliyekuwa mchezaji mwenzake wa Real Madrid James Rodriguez, ambaye kwa sasa anacheza kwa mkopo Bayern Munich, katika jitihada za kumshawishi mchezaji huyo raia wa Colombia mwenye miaka 27, ajumuike naye Juventus. (Marca)

Bora kutoka Jumatatu

Mario BaloteliHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Mshambuliaji wa Marseille Mario Balotelli, 28, anasema kuwa anataka kumaliza kazi yake ya kusakata soka kwa kuichezea timu yake ya nyumbani ya Brescia nchini Itali. (goal)

Mkufunzi wa Everton Marco Silva anasema kuwa anajua kwamba yuko chini ya shinikizo baada ya kikosi chake kushindwa na klabu ya Wolves na kusalia katika nafasi ya tisa katika jedwali la ligi ya Uingereza. (mirror)

Klabu ya Leeds inataka kumnunua winga wake wa zamani Aaron lennon, 31, kurudi katika klabu hiyo kwa kupitia kumsajili kutoka klabu ya Burnley mwisho wa msimu huu. (sun)

Ibrahim DiazHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Mshambuliaji wa Stoke City Bojan Krkic ,28, huenda akahamia katika klabu ya ligi ya Marekani New England Revolution ambayo imejitolea kumlipa mara mbili marupurupu yake huku dirisha la uhamisho nchini Marekani likiendelea kuwa wazi hadi tarehe mosi mwezi Mei. (sun)

Real Madrid haitamuuza kwa mkopo mwisho wa msimu huu kiungo wa kati wa Uhispania mwenye umri wa miaka 19 kinda Ibrahim Diaz ambaye walimsajili kutoka Manchester City. (AS)

Aaron lenon

Shirikisho la soka la Uingereza FA linataka kuanzisha refa wa kwanza atakayesimamia mechi za ligi ya wanawake ya.. (telegraph).

Kiungo wa kati wa Newcastle Sean Longstaff, 21, huenda akaitwa na timu ya Uingereza ilio na wachezaji wasiozidi umri wa miaka 21 baada ya kushirikishwa katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo.(Chronicle)

DR Congo imetetea agizo la kuwalipa mishahara mawaziri katika maisha yao yote

Prime Minister Bruno Tshibala standing with other officials
Waziri mkuu anayeondoka Bruno Tshibala alisaini maagizo hayo mnamo Novemba

Serikali ya Jamhuri ya Kidmeokrasi ya Congo imetetea maagizo yanayoruhusu mawaziri kulipwa mishahara na marupurupu kwa maisha yao yote.

Katika taarifa iliyotolewa Jumatatu, serikali imesema malipo hayo “sio ya kuwatajirisha maafisa”.

Maagizo mawili, yanayoruhusu mawaziri kupokea marupurupu ya kiwango cha chini zaidi $2,000 yameshutumiwa pakubwa.

Idadi kubwa ya raia nchini Congo wanaishi katika umaskini.

Serikali inayoondoka ilikuwa inawapatia mawaziri “kiwango cha chini kuwatosheleza mahitaji yao ya kimsingi, kama chakula, makaazi na huduma ya afya”.

Malipo hayo “ni ya kuwaepusha kuishia katika umaskini”, taarifa inasema.

Maagizo hayo mawili, yaliotiwa saini na waziri mkuu anayeondoka Bruno Tshibala mnamo Novemba, yaliripotiwa pakubwa hivi karibuni tu katika vyombo vya habari.

Agizo la kwanza linawapa mawaziri wakuu mishahara ya kila mwezi yalio sawa na 30% ya mshahara anaopokea sasa waziri mkuu, tiketi ya mara moja ya ndege kwa mwaka na marupurupu ya nyumba yenye thamani ya $5,000, kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters.

Agizo la pili linawapa mawaziri mishahara sawa na 30% ya mawaziri wa sasa na $1,000 kila mwezi kulipia makaazi. Watapokea pia tiketi ya mara moja kwa mwaka ya ndege, Reuters linaripoti.

new President of the Democratic Republic of Congo, Felix Tshisekedi, was sworn into office last monthHaki miliki ya pichaREUTERS

Kupita kiasi

Maagizo hayo yalishutumiwa pakubwa katika nyanja zote kisiasa.

Mshauri wa rais wa zamani Joseph Kabila amesema “hayaendani na mtazamo wetu wa kiuchumi na kijamii”.

Patrick Nkanga ameandika kwenye Twitter: “Ni kupita kiasi na ni gharama kubwa zisizohitajika kwa fedha za umma.”

Lakini serikali imetetea maagizo hayo na kueleza kwamba hayatozingatia mawaziri wa awamu iliopita, badala yake ni kwa walioko kwenye serikali ya sasa na serikali zijazo.

Rais mpya wa Jamhuri ya Kidmeorasi ya Congo, Felix Tshisekedi, aliapishwa madarakani mwezi uliopita. Alipokea wadhifa huo kutoka kwa Kabila katika ukabidhi wa kwanza wa madaraka uliofanyika kwa amani katika nchi hiyo na uliowahi kushuhudiwa katika miaka 60.

Matokeo ya uchaguzi yalishutumiwa pakubwa, huku kukiwa na ripoti za makubaliano kati ya rais Kabila na bwana Tshisekedi -hatahivyo pande zote zilikana tuhuma hizo

Wauguzi wagoma wakidai marupurupu yao Kenya

wahudumu wamegoma Nairobi
Image captionWahudumu waliomiminika katika Kaunti ya Nairobi wakidai malipo bora

Wagonjwa nchini Kenya wameanza kujawa na hofu baada ya wauguzi kuapa kuendelea na mpango wao wa kutekeleza mgomo au kuanzia leo Jumatatu.

Katibu mkuu wa Muungano wa wauguzi nchini kenya Seth Panyako alisema siku ya Jumamosi kuwa iwapo mahitaji yao ya kurudi kazini hayataangaziwa, basi hawatakuwa na chaguo jingine bali kufanya mgomo isipokuwa wauguzi katika kaunti ya Mombasa, Migori na Machakos ambao wamelipwa marupurupu yao kulingana na mkataba huo.

Amesema kuwa majadiliano kati ya serikali kuu na zile za kaunti yalioafikiwa mnamo tarehe mbili mwezi Novemba 2017 kwa huduma na marupurupu hayajaafikiwa.

Serikali ilikuwa na siku ya Jumapili pekee kuzuia mgomo huo.

Kaunti zitakazoathirika

Amesema kuwa kaunti ambazo wauguzi wake hawataripoti kazini ni Pokot Magharibi, Kisumu, Nairobi, Kisii, Taita-Taveta, Nyandarua, Trans Nzoia, Elgeyo Marakwet, Wajir, Nyeri na Kitui, hadi pale makubaliano hayo ya Novemba 2017 yatimizwe.

Matamshi yake yanajiri huku waziri wa leba Ukur Yatani akiwataka wauguzi kusitisha mgomo huo.

Mgomo wa wahudumu katika Kaunti ya Nairobi

Waziri huyo alisema kuwa ameteua kamati ambayo itaangazia maswala yote na kuandika ripoti katika kipindi cha siku 30.

Amesema kuwa swala tata ni kutotekelezwa kwa makubaliano ya kurudi kazini ambayo yaliafikiwa kati ya wahusika na kushuhudiwa na maafisa muhimu wa wauguzi, baraza la magavana na wizara ya Afya.

Akijibu hilo mwenyekiti wa baraza la magavana nchini kenya Wycliffe Oparanya aliihakikishia wizara , wauguzi na raia kuhusu juhudi zao za kushirikiana na kamati ilioundwa ili kutatua mgogoro huo.

Ajenda nne kuu za rais

Lakini akizungumza, Seth Panyako alisema kwamba baada ya kutoa ilani ya kufanyika kwa mgomo huo mwezi Novemba mwaka jana , wizara ilinyamaza na kuamua kubuni jopo la maridhiano siku ya Ijumaa.

”Tunaona kwamba huu ni mchezo unaofanywa na wizara kwa lengo la kukandamiza ajenda nne kuu za rais Uhuru Kenyatta . Kama Muungano wa wauguzi hatutakubali hilo”, aliongezea panyako.

Muungano huo umesitisha mgomo huo katika kaunti tatu.

Hatahivyo kaunti nyegine 18 bado hazijapokea ilani ya kurudi kazini baada ya kuonyesha kuwa ziko tayari kuafikia makubaliano hayo ya kurudi kazini.

Kaunti hizo ni Mandera, Tharaka Nithi na Vihiga huku zile 18 zikiwa Baringo, Laikipia, Meru, Bungoma, Nyamira, Isiolo, Kajiado, Kakamega, Kericho, Kilifi, Lamu, Nandi, Narok, Makueni, Turkana, Uasin Gishu, Bomet na Tana River.

Papa Francis awasili kwa ziara ya historia katika Umoja wa Falme za Kiarabu UAE

Pope Francis meets Abu Dhabi"s Crown Prince Mohammed bin Zayed Al-NahyanHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionThe Pope was welcomed by Abu Dhabi’s Crown Prince

Papa Francis amewasili katika Umoja wa falme za kiarabu kwa ziara ya kwanza kuwahi kufanyika na kiongozi mkuu katika kanisa katoliki Roma, katika rasi ya Arabuni.

Alitua mjini Abu Dhabi ambako alikaribishwa na mwanamfalme Sheikh Mohammed bin Zayed al-Nahyan.

Papa anatarajiwa kuhudhuria mkutano wa dini mbali mbali na Jumanne aandae misa ambapo takriban watu 120,000 wanatarajiwa kuhudhuria.

Kabla ya kuondoka alielezea wasiwasi wake kuhusu vita nchini Yemen ambapo Umoja wa Falme za kiarabu umehusika.

“Raia nchini Yemen wamechoshwa na mzozo wa muda mrefu na watoto wengi wanateseka kwa njaa, lakini hawawezi kufikia maghala ya chakula ,” Papa amesema

“Kilio cha watoto na wazazi wao kinapaa mbinguni kwa Mngu,” aliongeza.

Haijulikani wazi iwapo anapanga kulizusha suala hilo mbele ya umma au katika faragha wakati wa ziara yake. Umoja wa Falme za kiarabu unahusika katika mzozo nchini Yemen kama sehemu ya muungano unaoongozwa na Saudia.

Pope Francis is welcomed by Abu Dhabi"s Crown Prince Sheikh Mohammed bin Zayed Al NahyanHaki miliki ya pichaEPA
Image captionThe UAE Is home to nearly a million Roman Catholics

Kwanini ziara ya Papa ni muhimu Arabuni?

Kuna takriban watoliki milioni moja katika Umoja huo wa Falme za kiarabu, wengi wao kutoka Ufilipino na nchini India.

Baadhi tayari wamekuwa wakisimama kusubiri misa hiyo ya hapo kesho Jumanne. Mmoja ameliambia shirika la habari la AFP kwamba ziara ya Papa “inafungua milango kwa mazungumzo kuhusu kuvumiliana, ujumbe ambao dunia nzima unahitaji kuusikia”.

Katika ujumbe kwenye video alioutoa siku ya Alhamisi, Papa alisema : “Imani kwa Mungu inaunganisha watu na haiwatenganishi, inatufanya kuwa karibu licha ya tofuati zetu, inatutenga na uhasama na maovu.”

Alitoa heshima zake kwa Umoja huo wa flame za kaiarabu kuwa “nchi ambayo inajaribu kuwa mfano wa watu kuishi pamoja, mfano wa udugu, na eneo lililo na raia wa tabaka na tamaduni mbali mbali “.

Akiwa Abu Dhabi, Papa anatarajiwa pia kufanya mkutano na Sheikh Ahmed al-Tayeb, Imamu mkuu wa mskiti wa al-Azhar Cairo, ambao ni wadhifa mkuu wa mafunzo ya kidini kwa madhehebu ya Sunni kwa waislamu.

Mwandishi wa BBC aliyepo Abu Dhabi, anasema Vatican inatarajia kuwa ziara ya Papa itasaidia kulainisha vikwazo dhidi ya ujenzi wa makanisa katika enoe hilo, hususan katika eneo jirani Saudi Arabia ambako hakuna maeneo yanayoruhusiwa ya kuabudu kwa wasio waislamu.

Maafisa wa Vatican wanasema wanahitaji kuwa na uwepo mzito katika Umoja huo wa Falme za kiarabu, kusimamia jamii ya wakatoliki huko.

“Tumelemewa sana. Tunahitaji makanisa zaidi. Tunahitaji makasisi zaidi,” afisa mmoja amenukuliwa na shirika la habari la Reuters

Afukuzwa kazi kisa ujauzito

A working motherHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

”Nilifukuzwa kazi miezi minne baada ya kupewa likizo ya uzazi.”

“Nilikuwa tegemeo la familia yangu, sikua na muongozo wa sheria kwa hiyo nilishauriwa kutia saini ‘mkataba wa lazima’, Nilijihisi mnyonge sana.”

Haya ni maneno ya mama aliyezungumza na BBC baada ya kuchapisha makala kuhusu haki wa wanawake wajawazito kazini.

Kisa chake – na visa vya wengine wengi- vinaashiria ubaguzi unaoendelea kuwakabili wanawake wanaofanya kazi katika makampuni makubwa ya Ungereza ambapo viongozi wa ngazi ya juu wanakiuka sheria na kuwanyanyasa wanawake wanaopata ujauzito wakiwa kazini.

Lakini waathiriwa wanahofia sana kuzungumza kwasababu wamelazimishwa kutia saini mkataba wa kutozungumzia masaibu yanayowakabili.

Katika visa vingine masharti hayo yanawatishia kutozungumzia hali zao kwa ”pamoja”

Stressed mumHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Wakati mgumu

“Masharti hayo yanaziwezesha makampuni kuvunja sheria,” alisema mama aliyewasiliana na BBC.

“Unahitaji kuwa mjasiri na mvumilivu sana kushinda kesi mahakamani.”

“Nilikuwa na mtoto mchanga na wakati huo pia nilikuwa na hofu kuhusu jinsi nitakavyolipa deni la nyumba kwa hivyo sikuweza kupambana na kesi.

Karibu miaka tano sasa, baada ya kufutwa kazi katika mazingira ya kutatanisha anasema: “Tafadhali usichapishe jina langu, nataka kuangazia kisa changu tu. Nataka sheria ifanyiwe mabadiliko. Hii iliyopo haiwapatii ulinzi wanawake hata kidogo.”

Sheria iko wazi: ni kinyume cha sheria kufuta mtu kazi kwasababu ni mjamzito au yuko likizo ya uzazi.

Mama na mtotoHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Lakini wanawake wanaendelea kunyanyaswa. Ni hivi majuzi tu waziri wa biashara Kelly Tolhurst, alisema: “Ubaguzi dhidi ya wanawake wajawazito na wale waliyo likizo ya uzazi ni ukikaji wa sheria, lakini baadhi ya kina mama wapya wanashindwa kuendelea na kazi hata wakirudi kutokana na mazingira magumu ya kazi ambayo inawalazimu kuondoka.”

Mwanamke mwingine aliyewasiliana na BBC alijifungua miezi michache iliyopita na yeye pia hakutaka jina lake litajwe.

Masaibu yake yalianza pale bosi wekea alipomuita kujadali masuala ya kazi na mipango yake ya baadae.

“Nilipomwambia kuwa niko mjamzito alibadilika ghafla na kutoka wakati huo mtazamo wake kwangu ulibadilika kabisa, hilo lilinishangaza sana.” alisema.

Aliporejea kazini kutoka likizo ya uzazi mwaka uliyopita alitoa maombi ya kutaka kubadilishiwa nyakati za kazi ili aweze kumhudumia mtoto wake lakini ombi lake lilikataliwa.

“Hawakujua kwamba ningelichukua hatua zaidi. kwa kuwa najua haki yangu nilikata rufaa dhidi ya uamuzi huo.

“Kampuni iliamua kunilipa fidia na wakili wangu alinishauri nikubali ofa yao, lakini kufikia hilo nilitakiwa kutia saini mkataba wa kutozungumzia suala hilo.”

Kwa sasa mama huyo anajihisi vibaya sana. “Nilihisi kuwa hakuna aliyenijali wala kuelewa hali yangu.

“Cha kusikitisha zaidi ni kuwa ombi la mume wangu kubadilishiwa nyakati za kazi ili aweze kumhudumia mtoto pia lilikataliwa na muajiri wake. Hatua hiyo ilimaanisha sote tufanye uamuzi kwa kuzingatia haki yetu katika katiba.”

UjauzitoHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Anapendekeza serikali iongeze juhudi za kuhamasisha watu kuhusu haki zao na kuwahimiza wapaze sauti wanaponyanyaswa kazini.

Mwanaharakati Joeli Brearley, mwanzilishi wa shirika moja la kijamii ambalo linapigania haki za wanawake wanaobaguliwa kazini nchini Uingereza, anasema: “Mkataba wa kumzuia mtu kutozungumzia hali inayomkabili mara nyingi hutumiwa kumteka nyara mfanyikazi. Waajiri hutumia mkataba huo kama kikombozi cha kuwamanyamazisha wafanyikazi wao.”

Bi. Brearley anapendekeza yaliyomo kwenye mkataba huo kufuatiliwa kwa makini.

“Huwezi kufutilia mbali mkataba wa aina hiyo katika visa vingine kwasababu inamlinda mfanyikazi. Muajiri anazuliwa kisheria kumzungumzia vibaya muathiriwa kwa muajiri mtarajiwa na bila mkataba kama huo mfanyikazi huyo hatakuwa na ushahidi wa kujitetea mahakamani.”

Hata hivyo Bi. Brearley anaamini kufuatilia mkataba huo kutasaidia kukomesha “visa vya waajiri kuitumia vibaya kwa manufaa yao”.

Kile anachosisitiza ni kuhakikisha mkataba wa kumzuia mtu kuzungumzia hadharani suala fulani unawasilishwa kwa bodi maalum itakayopewa jukumu la kuchunguza yaliyomo ndani ya mkataba huo na kuchukua hatua endapo italazimika kufanya hivyo .

Mauaji ya Watoto: Waganga wa jadi wajitenga na matukio ya mauaji ya watoto Njombe, Tanzania

Waganga wa jadi
Image captionBaadhi ya Waganga wa tiba za jadi wilayani Njombe wakijadiliana jambo baada ya mkututano na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani

Waganga wa tiba za jadi wilayani Njombe nchini Tanzania wamejitenga na tuhuma kuwa wanachochea mauaji ya watoto wilayani humo.

Kwa mujibu wa serikali, uchunguzi wa awali umebaini kuwa mauaji ya watoto sita wilayani humo yamechochewa na imani za kishirikina.

Watoto hao, wakiwemo watatu wa familia moja wenye umri chini ya miaka 10 wamepatikana wakiwa wamefariki katika mazingira ya kutatanisha huku baadhi ya viungo vyao kama macho, meno na sehemu za siri vikinyofolewa.

Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola Jumatano aliliambia Bunge kuwa imani za kishirikina zimechochea matukio hayo na tayari serikali ina majina ya wahusika wote.

Hata hivyo, katika kikao chao na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Hamad Masauni wilayani Njombe waganga wa jadi wamesema wao si chanzo cha tatizo na kuitaka serikali ifanye uchunguzi zaidi

Kiongozi wa waganga wa tiba za jadi Antony Mwandulami amedai kuwa watu wamekuwa wakilipiziana visasi kwa mauaji na kusingiziwa waganga wa jadi.

“Kuna mambo mengi nyuma ya haya mauaji. Wapo ambao wanalipiziana visasi na hawaonekani lakini waganga wanalaumiwa kwa kusemwa kuwa wamepiga ramli chonganishi,” amesema Mwandulami.

Hofu yatanda

Image captionMsafara wa mazishi ya watoto watatu wa familia moja waliokumbwa na mkasa huo.

Mwandishi wa BBC Swahili Leonard Mubali anaripoti kutoka Njombe kuwa hofu imetanda wilayani hapo kutokana na matukio hayo ya mauaji.

Wazazi wameongeza uangalifu kwa watoto zao, na kuna ambao wanaacha shughuli zao na kusindikiza watoto shule.

Akizungumzia hofu hiyo waziri Masauni amesema: “Nachotaka kuwahakikishia wananchi ni kuwa macho, masikio, roho na moyo wa serikali umehamia Njombe. Waamini kuwa serikali jambo hili tumelichulia uzito mkubwa… ni jukumu letu kuwalinda wananchi ambao ndio wameiweka serikali hii madarakani. Lazima tuhakikishe kuna ulinzi, na hilo lipo ndani ya uwezo wetu na wala hatuna msalie mtume.”

Akizungumzia kikao na waganga wa jadi Masauni amesema lengo lilikuwa ni kuunganisha nguvu na kupata taarifa zaidi kutoka kwao hususan kuwataja wale ambao wanachochea uovu.

Image captionWaziri Masauni (katikati) akiogoza moja ya vikao wilayani Njombe kujadili mikasa hiyo ya mauaji ya watoto.

Mtu mmoja, kutoka kwenye familia ya watoto watatu waliouawa yumo mikononi mwa polisi huku uchunguzi zaidi ukiendelea.

Juzi Jumanne kuliibuka suitafahau baada ya wananchi wa Njombe kutaka kumpiga bwana mmoja ambaye wanadai alitaka kumteka mwanafunzi wa shule ya msingi.

Polisi iliwalazimu kutumia mabomu ya machozi ili kuutawanya umati huo wa watu wenye hasira

Matokeo EPL: Chelsea yabamizwa 4-0 na Bourmemouth, Liverpool yabanwa mbavu na Leicester

Joshua KingHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionJoshua King alikuwa mwiba ka Chelsea kwa kupachika magoli mawili na kutoa pasi ya goli moja.

Klabu ya Chelsea Jumatano usiku imekubali kipigo kizito cha goli nne bila majibu kutoka kwa klabu ya Bournemouth.

Kipigo hicho ni kikubwa zaidi kwa Chelsea kwa kipindi cha miaka 23 kwenye Ligi ya Premia. Kipigo kikubwa cha ‘mbwa koko’ ambacho Chelsea ilipokea ilikuwa Septemba 1996 walipofungwa 5-1 dhidi ya Liverpool.

Mpaka mapumziko kulikwa hakuna goli lililofungwa. Kipa wa Bournemouth Artur Boruc alikuwa nyota wa mchezo katika kipindi cha kwanza kwa kuzuia nafasi za wazi tano za Chelsea.

Gharika langoni mwa Chelsea ilianza dakika mbili tu baada ya mapumziko kwa Joshua King kuandika goli la kwanza katitika dakika ya 47.

King alikuwa mwiba mchungu kwa safu ya ulinzi ya Chelsea kwa kutengeneza goli la pili lililofungwa na David Brooks katika dakika ya 63. Goli la tatu lilifungwa na King katika dakika ya 74 kabla ya Charlie Daniels kupigilia msumari wa mwisho katika jeneza la Chelsea katika dakika za majeruhi (90+5).

Kipigo hicho kimewashusha Chelsea mpaka nafasi ya tano wakiwa sawa na Arsenal kwa alama 47 lakini Gunners wapo nafasi ya nne kwa kuwa wamefunga magoli mengi kuliko Blues.

Ushindi wa Bournemouth unaifaya klabu hiyo kupaa mpaka nafasi ya 10 kwenye msimao wa ligi na kufikisha alama 33.

Sarri abeba lawama

Maurizio SarriHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionKocha wa Chelsea Maurizio Sarri

Kocha wa Chelsea Maurizio Sarri amesema anabeba lawama zote baada ya kikosi chake kukubali kipigo hicho kizito.

Sarri amesema wachezaji wake hawakucheza kama timu kipindi cha pili na walikuwa wazito kukubali kutanguliwa.

“Labda sina uwezo wa kuwafanya wawe na ari ya kujituma wachezaji hawa,” amesema kocha huyo raia wa Italia.

“Wakati tunaenda mapumziko ilikuwa ni vigumu kufikiria kuwa kipindi cha pili kingeikuwa majanga na nitaka kujua kwa nini imekuwa hivyo … kama miezi miwili iliyopita tulikuwa tukicheza kama watu 11 tofauti na si timu moja. Nilifikiri hali hiyo ilibadilika tulipowafunga Tottenham wiki iliyopita, lakini bado. Kuna kitu lazima kibadilike.”

Chelsea walianza msimu kwa kutofungwa katika michezo 12 lakini sasa wameshapoteza michezo minne kati ya 12 waliyocheza hivi karibuni.

Liverpool yabanwa na Leicester

goliHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionLiverpool waliuanza mchezo kwa kasi na kupata goli katika dakika ya tatu kupitia Sadio Mane.

Liverpool imepoteza nafasi ya kutanua pengo kati yake na Mnchester City kileleni mwa Ligi ya Premia kwa alama saba baada ya kukubali sare ya 1-1 dhidi ya Leicester City.

Sadio Mane aliwatanguliza Majogoo wa Jiji Liverpool katika dakika ya tatu ya mchezo lakini goli hilo lilisawazishwa na Harry Maguire mwishoni kabisa mwa kipindi cha kwanza (dakika ya 45+2).

Laiti Liverpool inelipata ushindi, wangelifikisha alama 63 na kuwaacha mbali City wenye alama 56 baada ya kufungwa na Newcastle Jumanne usiku.

Sasa Liverpool wameongeza wigo wa uongozi kwa alama moja na kufikisha alama 61 na kufanya tofauti yao na City kuwa alama 5.

Kocha wa Liverpool Mjerumani Jurgen Klopp amelaumu theluji zilizodondoka wanjani Anfield zimechangia pakubwa timu yake kutokuwa na mchezo mzuri na kufanya wapate matokeo ya sare.

“Umeona mpira ulikuwa hauendi kwa kasi kabisa … na kama unamiliki mpira kwa asilimia 70 mpaka 80 basi mabo ndio yanakuwa magumu kabisa,” amesema Klopp.

Liverpool hata hivyo walinyimwa mkwaju wa penati baada ya Naby Keita kuchezewa faulo na Ricardo Pereira katika eneo la hatari

Muswada wa Vyama vya Siasa: Bunge lapitisha muswada ‘wenye utata’, sasa wasubiri saini ya Rais Magufuli

Spika NdugaiHaki miliki ya pichaBUNGE
Image captionBunge chini ya Spika Job Ndugai limepitisha muswada wa vyama vya siasa mbao umekuwa ukipingwa kwa madai kuwa utaminya Demokrasia

Hatimaye Muswada wa Mabadiliko ya Sheria ya Vyama vya Siasa Tanzania umepitishwa na Bunge la nchi hiyo na sasa utapelewkwa kwa Rais Magufuli ili ausaini na kuwa sheria.

Upitishwaji wa muswada huo umepitia vigingi kadhaa, ukikosolewa vikali na vyama vya siasa vya upinzani na asasi za kiraia ambao wanadai utaminya demokrasia nchini humo.

Hata hivyo wabunge wa chama tawala cha CCM ambao ni wengi Zaidi wameutetea muswada kwa kudai unaenda kusafisha siasa za vyama vingi.

Baada ya kupita bungeni muswada huo unatarajiwa kusainiwa na rais Magufuli ambaye serikali yake imekuwa ikibeba lawama za kuminya upinzani na uhuru wa kujieleza.

Waziri kivuli na mbunge wa Bunda, kupitia Chadema Esther Bulaya ameuita muswada huo kuwa ni ‘uonevu mkubwa dhidi ya vyama upinzani.’

Uonevu kwa mujibu wa Bulaya unadhihiri kwa msajili wa vyama vya siasa kupewa mamlaka ya kuingilia mfumo wa uchaguzi ndani ya chama akisema kutapunguza uhuru wa vyama kufanya chaguzi bila mashinikizo kutoka ofisi ya msajili.

Uonevu mwengine kwa mujibu wa upinzani ni masharti ya namna ya utoaji wa elimu ya uraia kwa kuzuia vyama rafiki kutoka nje kushiriki.

“Ni haki yao ya msingi ya kueneza itikadi za vyama vyao bila kujali mipaka ya nchi…huu ni upungufu mkubwa kwani msajili anaweza kukataa tu kutokana na maslahi yake bila kuongozwa na sheria inayopendekezwa,” amesema.

MagufuliHaki miliki ya pichaIKULU, TANZANIA
Image captionRais John Magufuli amekuwa akilalamikiwa kuminya demokrasia nchini Tanzania toka lipoingia madarakani miaka mitatu iliyopita.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama alilieleza Bunge kuwakuwa muswada huo ni kiboko.

Mhagama kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi ni amesema pamoja na mambo mengine muswada huo unalenga kumpa Msajili wa Vyama vya Siasa kuhakiki chama cha siasa wakati wowote.

“Lengo ni kuhakikisha chama cha siasa kinakuwa na sifa za usajili muda wote wa uhai wake na kueleza bayana mamlaka ya msajili wa vyama vya siasa kuhakiki muda wowote utekelezaji wa sheria ya vyama vya siasa ili kuhakikisha chama cha siasa kinazingatia na kutekeleza masharti ya usajili,” amenukuliwa na Mwananchi akisema.

Wakili Jebra Kambole ameiambia Dira TV ya BBC Swahili kuwa bado kuna ukakasi mkubwa hususani nguvu alizopewa msajili, “Watakaoanza kuathirika muswada ukianza kutekelezwa ni vyama vidogo (vya upinzani). Lakini pale msajili atakapotumia mamlaka yake ipasavyo vyama vingi vitaumia.”

Moja ya kifungu kinachopingwa ni cha Kifungu cha 19 ambacho kinasema msajili anaweza kukisimamisha usajili wa chama kwa sababu atakazozitaja na kwa muda atakaouweka mpaka ili chama hicho kiweze kujirekebisha.

Maalim Seif: Yanayotokea chini ya Magufuli, hatujawahi kuyaona Tanzania

Chama ambacho kimesimamishiwa usajili hakitaweza kufanya shughuli zote za kisiasa.

Na iwapo msajili ataona chama hicho hakijajirekebisha anaweza kukifutia usajili.

Kifungu hiki, wapinzani wanadai kinaweza kutumika kuzuia vyama kushiriki uchaguzi kwa jusimamishiwa usajili kabla yay a uchaguzi na kurudishiwa usajili baada ya uchaguzi kupita.

Awali vyama vya upinzani vilionesha kufurahishwa na baadhi ya mabadiliko yaliyoyofanywa na kamati ya bunge ya sheria.

Akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya vyama 15 vya upinzani, Jumapili Januari 27, 2019 jijini Dar es Salaam, naibu katibu mkuu wa Chadema (Zanzibar), Salum Mwalimu amesema baada ya kutoa maoni yao mbele ya kamati hiyo hivi karibuni bungeni Dodoma, hoja nyingi walizopigia kelele zimesikilizwa.

“Tulipigia kelele suala la mafunzo na adhabu zake. Kamati baada ya kupitia hoja zetu, kwanza imepunguza adhabu kutoka Sh1 milioni hadi Sh500,000 na jela kutoka miezi 6 hadi mitatu,” Mwalimualinukuliwa na Mwananchi.

Hata hivyo, alisema bado kuna utata umebaki wa kuchanganya elimu ya uraia na kujengeana uwezo ndani ya chama.

Uchaguzi DRC: Martin Fayulu atangaza kwenda mahakamani kupinga ushindi wa Tshisekedi

Martin Fayulu
Image captionMartin Fayulu amedai kuwa mshindi ameteuliwa na utawala wa Kabila ili akidhi matakwa yao

Matokeo ya uchaguzi DRC kupingwa mahakamani

Mgombea wa upinzani aliyeshindwa katika uchaguzi wa Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) uliofanyika Disemba 30 ameapa kuyapinga matokeo mahakamani.

Martin Fayulu ameiambia BBC kuwa raia wa Congo wanastahili kujua ukweli wa uchaguzi, mabao ameutaja kuwa ni “mapinduzi”.

Mgombea mwengine wa upinzani Felix Tshisekedi, alitangazwa kuibuka na ushindi katika kinyang’anyiro hicho, lakini kumekuwa na tuhuma kuwa mshindi huyo ameingia makubaliano ya kisiasa na rais aondokaye Joseph Kabila.

Tayari watu kadha wanaripotiwa kuuawa na wengine kujeruhiwa toka matokeo hayo yalipotangazwa.

Uchaguzi huo unakamilisha safari ya miaka 18 madarakani ya Joseph Kabila.

Matokeo hayo, endapo yatathibitishwa, yataweka historia ya makabidhiano ya amani ya hatamu za uongozi toka nchi hiyo ilipopata uhuru wake toka kwa wakoloni wa Ubelgiji mwaka 1960.

Kanisa lenye ushawishi mkubwa la Katoliki ambalo lilikuwa na waangalizi wa uchaguzi 40,000 limesema matokeo yaliyotangazwa hayaendani na matokeo waliyonayo.

Fayulu amesema nini?

Akiongea na mhariri wa BBC wa Afrika Fergal Keane, Bw Fayulu amesema atayapinga matokeo hayo kwenye mahakama ya katiba.

Joseph KabilaHaki miliki ya pichaAFP
Image captionMaswali yanaulizwa iwapo Kabila ametia mkono wake kwenye matokeo yaliyotangazwa

“Nitafanya kila liwezekanalo kwangu kufanya ukweli udhihiri sababu Wacongo wanataka mabadiliko,” amesema.

Fayulu hata hivyo ameweka wazi kuwa kuna uwezekano mdogo wa kushinda kesi hiyo sababu mahakama “imeundwa na watu wa Kabila” lakini amesema hataki kuwapa kisingizio wapinzani wake kuwa hakufuata sheria.

“Felix Tshisekedi ameteuliwa na Kabila ili kutekeleza matakwa ya utawala wa Kabila. Kabila ndiye bosi,” amedai Fayulu.

“Kabila hawezi kubaki na kusuka mpango na mtu ambaye hatakuwa na mamlaka yeyote… Tshisekedi anajijua kwamba hakushinda uchaguzi.”

Fayulu amesema ana hofu kuwa kutatokea vurumai kama tume ya uchaguzi (Ceni) haitatoa takwimu sahihi za “kituo kimoja kimoja cha kupigia kura” na kusisitiza kuwa ni haki ya kila Mkongomani kuandamana kwa mujibu wa sheria.

Je, kumetokea vurumai zozote?

Maelfu ya mashabiki wa Tshisekedi wameingia mitaani kwa furaha kusherehekea ushindi walioupata, lakini upande wa pili wafuasi wa Fayulu wamejitokeza mitaani kupinga matokeo hayo.

Matukio ya ghasia yameripotiwa katika eneo la Kikwit, ambapo polisi wawili na raia wawili wanasemakana kuuawa.

Kuna ripoti pia mamia ya wanafunzi wamekuwa wakipinga matokeo hayo kwa kuandamana na kutimuliwa na mabomu ya machozi katika mji wa Mbandaka.

Maandamano pia yameripotiwa katika eneo la Kisangani, lakini kusini ambapo Tshisekedi anaungwa mkono kwa wingi kumekuwa na sherehe.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) Antonio Guterres amezitaka pande zote kujizuia kufanya ghasia.

Matokeo yaliyotangazwa na CENI:

  • Felix Tshisekedi 7,051,013 (38.57%)
  • Martin Fayulu Madidi 6,366,732 (34.83%)
  • Emmanuel Shadary 4,357,359 (23.84%)

*Waliojitokeza kupiga kura wanakisiwa ni 48%.

Nini kinachoweza kufuata?

Wagombea wenye dukuduku na matokeo wanatakiwa kuwasilisha hoja zao mahakamani saa 48 toka kutangazwa kwa matokeo ya awali.

Majaji itawachukua siku saba kupitia kesi na kutoa maamuzi.

Mtaalamu wa masuala ya Katiba Jacques Ndjoli ameiambia BBC kuwa kuna matokeo ya aina tatu ambayo yanayotarajiwa : mosi mahakama inaweza kuthibitisha ushindi wa Tshisekedi, pili kuamuru kura zihesabiwe upya na tatu kufuta matokeo yote na kuamuru kura zipigwe upya.

Felix Tshisekedi at an election event in Kinshasa, December 2018Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionFelix Tshisekedi ametangazwa mshindi

Mahakama ya katiba haijawahi kubatilisha matokeo kabla, na wengi wanawaona majaji wake kuwa washirika wakubwa wa chama tawala.

Iwapo ushindi wa Tshisekedi utathibitishwa basi ataapishwa ndani ya siku 10.

Matokeo yamepokewaje?

Tshisekedi ameusifu ushindi wake na kuahidi kuwa “raisi wa Wakongomani wote”.

Msemaji wake Louis d’Or Ngalamulume amekanusha vikali uwepo wa makubaliano yoyote na Kabila.

Chama tawala cha Kabila ambacho kimeshika nafasi ya tatu hakijayapinga matokeo hayo.

Nje ya Congo kumekuwa na mchanganyiko wa maoni ya kutaka watu kuwa watulivu na wengine wakitaka ufafanuzi wa kilichotokea.

Mkuu wa Kamisheni ya AU Moussa Faki Mahamat amesema: “Ni muhimu kwa mtanziko wowote wa matokeo, hususani kuwa hayajaakisi matakwa ya wananchi, inabidi utatuliwe kwa njia ya amani kwa kutumia sheria na makubaliano ya kisiasa kwa pande zinazohusika.”

Uchaguzi DRCHaki miliki ya pichaAFP/GETTY IMAGES
Image captionWafuasi wa Bw Tshisekedi wakisherehekea mjini Goma, mashariki mwa DRC

Marekani imewasifu wapiga kura kwa kuwaita mashujaa na kutaka maswali yote tata kuhusu kura na matokeo yapatiwe majibu sahihi.

Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Jean-Yves kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters ameomba kuwepo na ufafanuzi kuhusu matokeo hayo akisema ushindi wa Bw Tshisekedi unaenda kinyume na uhalisia mashinani.

“Kanisa Katoliki la Congo lilifanya hesabu yake na kutoa matokeo tofauti kabisa,” amenukuliwa na shirika hilo.

Nchi ya Ubelgiji ambayo iliitawala DRC wakati wa ukoloni imeungana na Ufaransa katika kutilia mashaka matokeo hayo.

Waziri wa Mambo ya Nje Didier Reynders amenukuliwa la shirika la habari la Reuters akiiambia redio ya taifa RTBF kuwa Ubelgiji itatumia nafasi yake ya muda katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kutaka taarifa rasmi ya kilichotokea.

“Tuna mashaka na inabidi tuhakikishe na kujadiliana suala hili katika vikao vya Baraza la Usalama,” Bw Reynders ameongeza.

Presentational grey line
Viongozi wa DRC

Mada zinazohusiana