Raisi Donald Trump asema Jaji Kavanaugha alilengwa kisiasa

Rais wa Marekani Donald amemuomba radhi kwa niaba ya raia wa Marekani Jaji mpya wa mahakama ya upeo Brett Kavanaugh kwa kile alichokiita kwamba ni kampeni chafu za kisiasa zilizolenga kuharibu sifa binafsi ya Brett kutokana na mambo ya uzushi na uongo.

Trump ameyasema hayo katika sherehe za kuapishwa kwa jaji huyo mkuu wa mahakama ya juu ya Marekani shughuli ambazo zimefanyika katika Ikulu ya white House. Hatua ya kumthibitisha bwana Kavanaugh katika uteuzi wake huo iligubikwa na kashfa za ukatili wa kingono anaodaiwa kuufanya mwaka 1980.

Rais Donald Trump tangu awali alisikia madai ya Chama cha Upinzani cha Democratic kupinga uteuzi wa Bwana Kavanaugh ambaye binafsi amemuita kuwa ni Jaji makini na ambaye hana jambo lolote baya alilolifanya isipokuwa hizo ni jitihada za kutaka kumchafua tu.

Kauli hii ya Rais Trump imekuja huku hiki kikiwa ni kiapo cha cha awali cha bwana Kavanaugh chini ya usimamizi wa Jaji aliyemaliza muda wake Anthony Kennedy huku akiwa amebakiwa na kiapo cha mwisho kutoka kwa Rais Donald Trump.

Trump; sihusiki na makosa ya Cohen

Trump: Mkiniondoa madarakani masoko yataporomoka na mtakuwa maskini

Hata hivyo kwa hatua hiyo bado Wanasheria wakuu wa chama upinzani hawakubaliani na uteuzi wa Brett ambaye wanamtuhumu kwamba ana makosa mengi ya kinidhamu likiwemo hilo la madai ya kutaka kumbaka aliyekuwa mwanafunzi mwezake Christine Blasey enzi hizo wakisoma sekondari na kwamba wanataka kuyafikisha upya madai hayo kwa FBI.

Bwana Kavanaugh mwenye umri wa miaka 53 alithibitishwa kuwa Jaji na Baraza la Seneti siku ya Jumamosi na kushinda kwa kura 50 dhidi ya 48 zilizokuwa

Ajali ya lori la mafuta yasababisha vifo vya watu 50 DRC

Takriban watu 50 wameuawa baada ya trela ya kusafirisha mafuta kugongana na gari ndogo katika barabara kuu magharibi kwa Jamhuri ya Demokrsi ya Congo.

Ajali hiyo ilitokea karibu na mji wa Kisantu, kati ya mji mkuu Kinshasa na bandari ya Matadi.

Watu 100 walipata majeraha mabaya ya moto kwa mujibu wa Atou Matabuana, gavana wa mkono wa wa Kongo Central.

“Moto ulisambaa kwa haraka na kuteketeza nyumba zilizokuwa karibu,”hii ni kwa mujibu wa redio ya Umoja wa Mataifa ya Okapi.

Barabara kati kati mwa nchi zimetelekezwa kwa miaka mingi kutokana na vita.

Mwaka 2012 watu 220 waliuawa wakati trela ya mafuta ilipinduka na kuteketeza vijiji kadhaa.

Mmoja wa wale walioshuhudia aliiambia AFP kuwa aliona milii 53.

Daktari kwenye hospitali moja anayewatibu majeruhi alisema hakujakuwa na muda wa kuwapa matibabu waathiriwa.

‘Tuanajaribu kuwasaidia lakini kuna wale wanakufa,” Dr resor alisem.

Mji wa Kisantu uko umbali wa kilomita 120 kusini magharib mwa Kinshasa.

Map showing the locations of Kisantu, Kinshasa, Matadi in the west of the DR Congo
Image captionRamani ya Kisantu, Kinshasa, Matadi

Dereva aliyeruhusu nyani kuendesha basi afutwa kazi India

Dereva wa basi nchini India amefukuzwa kazi baada ya kumruhusu nyani aendeshe badi lake,

Dereva huyo anafutwa licha abiria hata moja kati ya abiria 30 au zaidi waliokuwa kwenye basi hiyo kutolalamika.

Hata hivyo wakati video ya nyani huyo aliyekuwa ametulia huku akiwa usukani kusambaa mitandaoni, waajiri wa dereva huyo walichukua hatua.

Maisha ya abiria hayawezi kuwekwa hatarini kwa kuruhusu nyani kushika usukani, msemaji alisema.

Hata hivyo hatua hiyo wa waajiri kumfuta dereva haijawafurahisha watumiaji wa mitandao waliofurahishwa na video hiyo.

“Vizuri sana, kwa nini mmufute. Angepewa onyo na aambiwe asirudie, mmoaj aliandika katika twitter.

Kisa hicho kilitokea siku ya Jumatatu kwa mujibu wa idara ya usafiri wa barabarani ambayo ilikuja kufahammu kuhusu kisa hicho wakati video hiyo ilanza kusambaa.

Kwa mujibu wa walioshuhudia, nyani alipanda gari na abiria mwingine lakini akakataa kuketi nyuma bali mbele ya basi.

Dereva M Prakash, ambaye alionekana kutotilia maanani sana suala hilo, alimruhusu nyania kuketi kwenye usukani huku wakiendelea na safari.

Kulingana ripoti nyania alifika kituo chake akashuka na kumuacha dereva akiendelea na safari yake.

Meng Hongwei: China yathibitisha inamzuia mkuu wa Interpol aliyepotea

China imethibitisha inamzuia mkuu wa Interpol aliyepotea Meng Hongwei.

Beijing imesema alikuwa anachunguzwa na tume ya kupambana na rushwa nchini humo kwa ukiukaji wa sheria.

Meng, ambaye pia ni naibu waziri wa wizara ya usalama wa umma China, aliarifiwa kupoeta baada ya kusafiri kutoka mji wa Lyon Ufaransa , kuliko na makao makuu ya Interpol kwenda China mnamo Septemba 25.

Interpol imesema imepokea barua ya kujiuzulu kwake mara moja kutoka kwa ofisi ya rais.

Familia yake Meng haijawasiliana naye tangu andoke katika makao hayo makuu ya Interpol nchini Ufaransa

Gazeti la South China Morning Post lilikunuu taarifa zilizosema kuwa Bw Meng, 64, alipelekwa kwenda kuhojiwa nchini China.

Haijulikani ni kwani nini alikuwa anachunguzwa na mamlaka za nidhamu au alikuwa anazuiliwa wapi.

Mapema wiki hii mwanafilamu Fan Bingbin, ambaye alitoweka nchini China, aliibuka akiomba msamaha na faini ya dola milioni 129 kwa kukwepa kulipa kodi na makosa mengine.

Meng Hongwei ni nani?

Haki miliki ya pichaEPA
Image captionMeng Hongwe

Alichaguliwa rais wa Interpol mwezi Novemba mwaka 2016, raia wa kwanza wa China kuchukua wadhifa huo na anatarajiwa kuwa katika wadhifa huo hadi mwaka 2020.

Yeye ni mkuu wa kamati kuu cha shirika hilo ambalo hutoa mwongozo mzima wa Interpol.

Kabla ya kuchukua wadhifa huo, Bw Meng alikuwa naibu waziri wa masuala ya usalama wa umma nchini China na bado yeye ni mwanachama wa cheo cha juu wa chama cha Communist.

Pia ana ujuzi wa miaka 40 ya ujuzi wa sheria ya uhalifiu nchini China hasa katika nyanja za madawa ya kulevya, ugaidi na udhibiti wa mipaka.

Baada ya kuchaguliwa kwake makundi ya haki za binadamu yalielezea wasi wasi kuwa hatua hiyo itaisadia China kuwatafuta watoro wa siasa ambao waliikimbia nchi.

Tetemeko la ardhi Indonesia: Idadi ya waliofariki dunia yafika takriban watu 832

A shattered mosque in Palu, 30 SeptemberHaki miliki ya pichaEPA
Image captionMsikiti huu Palu uliharibiwa na tsunami

Takriban watu 832 wameuawa baada ya tetemeko kubwa la ardhi na tsunami kupiga kisiwa cha Indonesia cha Sulawezi, kwa mujibu wa shirika la majanga la kitaifa.

Juhudi za kuwatafuta manusura zinaendelea na idadi ya waliofariki inatarajiwa kupanda pakubwa maeneo mengi ambayo kufikia sasa hayajafikiwa na waokoaji yakifikiwa.

Shirika hilo liloongeza kuwa eneo lililoathiriwa lilikuwa kubwa kuliko iliyodhaniwa.

Watu wengine waliripotiwa kukwama kwenye vifusi vya mango yaliyoporomka siku ya Ijumaa.

Tetemeko hilo lilichangia kutokea kwa tsunami yenye mawimbi ya hadi urefu wa miata 6.

Waokoaji wamekuwa wakichimba kwa mikono wakiwatafuta manusura kwenye mji wa Palu.

Vikosi vya uokoaji vinajaribu kuwafikia mamia ya watu ambao inawezekana wakawa hai katika mji wa Palu ambao miundombinu yake imeharibika vibaya huku wengi wao wakitajwa kukwama katika maduka na majumba makubwa.

Sehemu kubwa ya mji wa Palu imeharibiwa vibaya huku dalili za kuwapata walionasa wakiwa hai zikianza kufifia.

TsunamiHaki miliki ya pichaEPA
Image captionDaraja hili liliharibiwa na tsunami iliyosababishwa na tetemeko hilo

Katika ziara yake kwenye mji wa Palu Rais wa Indonesia Joko Widodo, amewaambia viongozi wa eneo hilo kuwa serikali kuu itatoa mahitaji yote muhimu ili matengenezo mapya ya mji huo yaweze kufanyika.

”Hakika hii ni hali ya dharura kama ilivyo ya Lombok. Kutakua na ugumu wakati, kwa siku moja au mbili na ni kazi kubwa. Uelekeo wa Barabara hii haipo imefungwa, ata uwanja wa Ndege haufanyi kazi ipasavyo,” amesema.

“Vituo vya kuzalisha umeme pia vimeharibiwa, na kati ya saba ni viwili tu ndivyo bado vinafanya kazi na wasambazaji wa mafuta wasingeweza kuyafikia maeneo kutokana na kuharibika kwa barabara. Lakini tayari tumeagiza kila kitu kama mafuta, na wasambazaji watafika siku mbili kuanzia sasa.

“Na vifaa vyote vizito vitakuja usiku wa leo, ili tuweze kuvitumia kesho pamoja na ahueni ya misaada kama vile chakula na maji safi.Baada ya kuona kila kitu kinafanya kazi kama kawaida tutaingia kwenye hatua kujenga na kuzirekebisha nyumba hizo. Na Serikali itawaaidia kama tukivyofanya Lombok.”

Palu map
Image captionRamani ya Palu

Kuna wasi wasi kuhusu hali ya mji wa Donggala ambopo kiwango cha uharibifu bado hakijulikani.

Shirika la msalaba mwekundu limekuwa likikadiria kuwa zaidi ya watu milioni 1.6 wameathiriwa na tetemeko hilo la ardhi na tsunami lililotajwa kuwa janga ambalo litazidi kuwa baya zaidi.

Makamu rais nchini Indonesia Jusuf Kalla alisema idadi kamili ya watu waliouawa inaweza kufika maelfu.

A tsunami-devastated area in Talise beach, Palu, central Sulawesi, Indonesia, 30 September 2018Haki miliki ya pichaEPA
Image captionTsunami iliacha uharibifu mkubwa

Mitetemeko midogo ya ardhi imekuwa ikiendelea kupiga kisiwa hicho tangu siku ya Ijumaa.

Baadhi ya manusura wamesema walisukumwa zaidi ya mita 500 na mawimbi yaliyoambatana na kimbunga hicho. Baadhi walikuwa na watoto wao pamoja na wapendwa wao lakini mwishoni wakajikuta wapo wenyewe.

Serikali imelimarisha jeshi na raia wauokoaji ili kusaidia kuondoa miili ya watu walioangukiwa na majengo na wale ambao bado wapo ndani ya majengo hayo wakisikika kuomba msaada.

Rais Joko Widodo yuko Palu na anakagua maeneo yaliyoathiriwa na janga hili zikiwemo fukwe za Talise, eneo kuu la kitalii lililoathiriwa vibaya na tsunami.

Miili imekuwa ikitabakaa kwenye mitaa ya mji na waliojuhiwa wanatibiwa kwenye mahema kwa sababu hospitali ziliharibiwa.

Walionusurika mjini Palu walilala nje siku ya Jumamosi kufuatia onyo la kuwatahadharisha wasirudi makwao.

Rubble of the Roa Roa hotel in PaluHaki miliki ya pichaEPA
Image captionWatu wengi walikuwa kwenye hoteli hii ya Roa Roa na baadhi walifukiwa kwenye vifusi

Mada zinazohusiana

Mambo tisa ya kushangaza kuuhusu Mwezi na Marekani ilipotaka kuulipua

Haki miliki ya pichaEPA

Umbo la mwezi hubadilika na hata rangi yake, lakini tangu jadi binadamu amekuwa akivutiwa na maumbile yake. Kuna Mwezi Mpevu, Mwezi Mwandamo, Hilali na hata wakati mwezi hupatwa na jua.

Hapa tumekuandalia mambo tisa ya kushangaza kuuhusu Mwezi.

1. Mwezi si tufe

Mwezi una umbo la yai. Ukiuangalia kile unachokiona ni moja ya sehemu ndogo za kando. Si kitu kilicho na umbo lililo sawa kwa uzito- eneo lake la kati la uzito haliko kabisa katikati mwa Mwezi bali karibu kilomita 2 kutoka sehemu ambayo inadhaniwa kuwa ndicho kitovu cha Mwezi.

2. Hatuuoni mwezi wote.

Kwa kila wakati fulani sisi huona asilimia 59 ya Mwezi. Uliobakia asilimia 41 hauwezi kuonekana kutoka duniani. Na kama huwezi kuamini, kama unaweza kwenda anga za mbali na kusimama eneo hilo la asilimia 41 huwezi kamwe kuiona dunia!

3. Mwezi wa Samawati ulitokana na volkano

Mlipuko mwa mlima kwa jina Anak Krakatau (Mwana wa Krakatoa) Julai 2018 nchini Indonesia
Image captionMlipuko mwa mlima kwa jina Anak Krakatau (Mwana wa Krakatoa) Julai 2018 nchini Indonesia

Umewahi kusikia kuhusu Mwezi wa Samawati au Buluu ambao kwa Kiingereza huitwa Blue moon? Matumizi ya msemo huu yanaaminika kuanzia mwaka 1883 kufuatia kulipuka kwa mlima wa volkano wa Krakatoa nchini Indonesia. Vumbi kubwa lilijaa angani hivi kwamba wakati uliuangalia Mwezi, ulionekana kama ulikuwa na rangi ya samawati.

Kwa kweli ni kitu ambacho hakikuwa cha kawaida ndio kikachangia msemo “once in a blue moon” ikimaanisha kitu ambacho ni nadra sana kutokea.

4. Mpango wa Marekani kuulipua Mwezi

Marekani wakati mmoja ilitaka kuulipua Mwezi kwa kutumia bomu la nyuklia

Marekani ilikua inataka sana kulipua bomu la nyuklia mwezini.

Lengo lilikuwa ni kuonyesha ubabe wa Marekani kuiwezesha kuitia kiwewe Urusi na washirika wake wakati wa vita baridi, hasa baada ya Muungano wa Usovieti kuongoza katika jitihada za kupeleleza na kutalii anga za juu, hasa baada ya kurusha satelaiti ya kwanza kwenye mzingo wa dunia, satelaiti ya Sputnik 1 mnamo 4 Oktoba 1957.

Wataalamu walikuwa pia wanachunguza madhara ambayo yangesababishwa na mlipuko mkubwa wa nyuklia kwenye mazingira.

Mradi huo wa siri ulipewa jina ‘A Study of Lunar Research Flights‘, au ‘Project A119‘ na ulianzishwa mwaka 1958. Utafiti hata hivyo ulikuwa umeanza kisiri mwaka 1949 katika kituo cha utafiti kuhusu silaha cha ARF katika Taasisi ya Teknolojia ya Illinois.

Mlipuko wa bomu hilo ungekuwa mkubwa sana hivi kwamba ungeonekana kutoka duniani.

Mpango huo haukutekelezwa kutokana na wasiwasi kwamba raia hawangeupokea vyema na pia hatari kwa binadamu iwapo mpango huo ungeenda mrama na ulifutwa rasmi Januari 1959.

Aidha, kiongozi wa mradi huo Leonard Reiffel alihofia hatua kama hiyo ingekuwa hatari kwa juhudi za baadaye za kupeleleza zaidi kwenye Mwezi na pia mpango wa kuwapeleka binadamu wakaishi huko.

Taarifa za kuwepo kwa mpango huo zilifichuliwa mwaka 2000.

5. Kupatwa kwa mwezi ‘kulikosababishwa na joka’

Kupatwa kwa jua zamani China kuliaminika kutokana na mwezi kumezwa na jua
Image captionKupatwa kwa jua zamani China kuliaminika kutokana na mwezi kumezwa na jua

Imani za kale za Kichina zilisema kuwa kupatwa kwa jua kulisababishwa na joka kulimeza jua.

Kuzuia hilo watu walipiga kelele sana wakati wa kupatwa kwa jua kumfanya joka aogope na atoroke.

Pia waliamini kuwa chura mkubwa aliishi kwenye Mwezi akiketi juu ya shimo kubwa. Mashimo makubwa kwenye Mwezi hayakusababishwa na wanyama wowote bali yalisababishwa na mawe makubwa ya anga za juu kuugonga mwezi takriban miaka bilioni 4.1 iliyopita.

6. Mwezi unapunguza kasi ya dunia.

Wakati mwezi unakaribiana sana na dunia kile kinachaoitwa Perigee hutokea. Hii inamaanisha kuwa nguvu za kuzunguka kwa dunia hutwaliwa na Mwezi kidogo kidogo hali ambayo husababisha dunia kupunguza kasi yake kwa karibu milisekunde 1.5 kwa kila karne moja.

7. Mwangaza wa mwezi

Jua lina mwangaza wenye nguvu mara 14 zaidi ya ule wa Mwezi unapokuwa mpevu. Ili Mwezi mpevu upate kuwa na mwangaza sawa na wa jua unahitaji kuwa na Miezi 398.110. Wakati wa kupatwa kwa Mwezi wakati mwezi unaingia kwenye kivuli cha dunia viwango vya joto mwezini vinaweza kushuka hadi karibu nyuzi joto 500F (260 celsius) katika kipindi cha chini ya dakika 90

8. Leonardo da Vinci aligundua kuwa mwezi haukuwa na umbo la hilali

Hilal Bayonne, New Jersey Julai 2018Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Wakati Mwezi unaonekana kuwa umbo la hilali, kile tunachokiona ni mwanga wa jua ukimulika sehemu ya Mwezi. Eneo jingine la mwezi halionekani vizuri, kulinngana na hali ya hewa. Leonardo da Vinci ndiye mtu wa kwanza anayejulikana kugundua kuwa mwezi haukuwa unapungua au kuongezeka. Ni kuwa sehemu yake nyingine ilikuwa imefichwa.

9. Kutoa majina kwenye Mwezi

Shimo kubwa la Giordano Bruno kwenye Mwezi lililo na upana wa kilomita 22Haki miliki ya pichaUNIVERSAL HISTORY ARCHIVE/GETTY IMAGES
Image captionShimo kubwa la Giordano Bruno kwenye Mwezi lililo na upana wa kilomita 22

Muungano wa Kimataifa wa Anga za Juu ndio huyapa majina mashimo yaliyo kwenye Mwezi na pia mawe, sayari na vitu vingine vinavyopatikana anga za juu. Mashimo makubwa kwenye mwezi yamepewa majina ya wanasayansi, wasanii na wapelelezi maarufu. Mashimbo yanayopatikana karibu na shimo kubwa la Apollo hupewa majina ya Wamarekani na yale yanayozunguka shimo kubwa la Mare Moscoviense hupewa majina ya Warusi.

Kangi Lugola: Kwa nini waziri hataki watuhumiwa wanyimwe dhamana wikendi Tanzania, sheria inasema nini?

LugolaHaki miliki ya pichaIKULU, TANZANIA

Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola nchini Tanzania amewataka polisi kukoma kuwanyima watuhumiwa kunyimwa dhamana hasa siku za mapumziko, kwa kisingizio kuwa si siku za kazi.

Waziri huyo alisema hilo ni kinyume cha sheria na mtu yeyote anayestahiki kupewa dhamana anafaa kuhudumiwa katika chini ya saa 24 wakati wowote ule.

Bw Lugola alisema hayo katika kijiji cha Busanza wilayani Uvinza mkoani Kigoma Jumapili.

“Hii tabia sijui imetoka wapi na imejengeka kwa baadhi ya askari polisi. Eti mtu akiingia mahabusu siku ya Ijumaa ikifika Jumamosi na Jumapili hawatoi dhamana wakisema mpaka Jumatatu, hii tabia sio sahihi na ife haraka iwezekanavyo,” alisema Lugola, kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi.

Waziri huyo alisema vituo vya polisi nchini humo huwa vinafanya kazi siku zote za wiki zikiwemo za mapumziko na haoni ni sababu gani inayoweza kuwafanya polisi kutompa mtuhumiwa dhamana.

Aliahidi kuchukua hatua dhidi ya askari yeyote atakayeshindwa kutoa dhamana kwa kosa ambalo lina dhamana.

Kwa mujibu wa waziri huyo, dhamana ni haki ya mtu endapo kosa lake linadhaminika.

Lugola: Watanzania ndio waliotulazimu kuweka masharti ya kuondoka nchini

Aidha, aliwataka huku akiwataka wananchi watakaoombwa fedha ili wapewe dhamana kuripoti tukio hilo kwa maofisa wa ngazi za juu ili askari husika achukuliwe hatua za kinidhamu.

“Kuna tabia iliyozoeleka katika jamii, eti kuingia polisi ni bure ila kutoka ni fedha, hii kauli nataka ife kwa sababu nawajua polisi na hawanidanganyi kwa lolote,” amesema.

Sheria inasema nini kuhusu dhamana?

Kwa mujibu wa maelezo katika tovuti ya jeshi la polisi Tanzania, dhamana ya polisi inafaa inatolewa bure.

“Hakuna malipo yoyote yanayotakiwa kutolewa ili mtuhumiwa au mshtakiwa akubaliwe dhamana,” inasema tovuti hiyo.

Jambo la msingi ni mtuhumiwa kuomba apewe dhamana na kutimiza taratibu kwa muijibu wa sheria.

Vigezo vya kuzingatia kabla ya mtuhumiwa kupewa dhamana ya Polisi ni:

Polisi kujiridhisha kwamba mtuhumiwa atatimiza masharti ya dhamana atakayopewa, ikiwa ni pamoja na kufika siku na saa atakayoamriwa.

Hii ni pamoja na:

  • historia yake na mshikamano wake na jamii au makazi, ajira na hali ya kifamilia na rekodi yake ya polisi, kama inajulikana, na
  • mazingira ambayo kosa lilitendeka, asili na ukubwa wa kosa, uzito wa ushahidi dhidi ya mtu huyo na taarifa nyingine zinazohusiana na uwezekano wake wa kutoroka.

Kujua makazi,ndugu na jamaa, ajira na ikibidi hali ya maisha ya mtuhumiwa na familia yake, kumbukumbu za kihalifu kama zipo.

Umuhimu wa mtuhumiwa kuwa nje kwa dhamana, ili aweze kujiandaa kukabiliana na tuhuma zinazomkabili kabla ya hajafikishwa mahakamani mfano kupata msaada wa kisheria.

Hifadhi ya jamii, kwa maana ya uwezekano wa mtu huyo kuingilia ushahidi kwa kuwatisha mashahidi au kuzuia uchunguzi wa polisi kwa jinsi yoyote ile.

Kuna sababu za kumnyima mtuhumiwa dhamana?

Kifungu cha 67 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai nchini Tanzania kinaeleza kwamba, mtuhumiwa aliye chini ya ulinzi wa Polisi anaweza kukataliwa maombi yake ya kutaka apewe dhamana, Hii ni iwapo polisi watajiridhisha kwamba mtuhumiwa hajatimiza vigezo vilivyoelezwa hapa juu. Aidha, mtuhumiwa anaweza akafutiwa dhamana aliyopewa awali.:

Kufutwa kwa dhamana ya polisi

Baada ya mtuhumiwa kupewa dhamana ya Polisi na kuwa huru dhamana hiyo inaweza kufutwa na mkuu wa kituo , chini ya kifungu cha 68 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai.

Baadhi ya sababu zinazoweza kusababisha uamuzi wakufuta dhamana ni:-

  • Kubainika kwamba mtuhumiwa anapanga mipango ya kutoroka
  • Kwa makusudi anakiuka au yu karibu kukiuka masharti ya dhamana.

Mtuhumiwa kama huyo hata hivyo atalazimika kupelekwa mbele ya hakimu kushughulikiwa kwa mujibu wa sheria mapema iwezekanavyo, na haifai kuwa zaidi ya kikao cha kwanza cha mahakama katika sehemu ambayo inawezekana kumpeleka mtu huyo kwa dhumuni hilo.

Fatuma Karume: Tutaendelea kuikosoa serikali na kutetea haki Tanzania

Anayekosa dhamana ya polisi anaruhusiwa kisheria wakati wowote, kumuomba afisa polisi kumpatia nyenzo kwa ajili ya kufanya maombi ya dhamana kutoka kwa hakimu. Polisi anafaa kufanikisha hilo ndani ya saa ishirini na nne, au katika muda mwingine wa kutosha kadri inavyowezekana baada ya kufanya maombi, na kuhakikisha amempeleka mtuhumiwa mbele ya hakimu.

Mtuhumiwa atakuwa na haki ya kupata dhamana kama:

  • anaahidi kwa maandishi kuhudhuria mbele ya mahakama iliyotajwa katika muda na mahali palipotajwa, au katika muda mwingine na mahali kama atakavyoarifiwa na afisa polisi;
  • anaahidi kwa maandishi kuzingatia masharti yatakayotajwa kuhusiana na mwenendo wake wakati ameachiwa kwa dhamana, masharti yasiyohusiana na utoaji wa dhamana, kuweka fedha au kutaifisha fedha.
  • mtu mwingine anayekubalika na afisa polisi anakiri kwa maandishi, kwamba anamfahamu mtu anayeshitakiwa na anamtambua kuwa ni mtu anayewajibika ambaye anaweza kuhudhuria mahakamani kujibu mashitaka.
  • mtu anayeshitakiwa, au mtu mwingine anayekubalika kwa afisa polisi, anaingia kwenye makubaliano, akiwa na dhamana au bila dhamana, kutaifishwa kiasi cha fedha iliyotajwa iwapo mtu aliyeshitakiwa atashindwa kuhudhuria mahakamani kujibu mashitaka; au
  • mtu anayeshitakiwa, au mtu mwingine anayekubalika kwa afisa polisi, anaweka kwa afisa polisi, kiasi fulani cha fedha kilichotajwa kitakachotaifishwa iwapo mtu aliyeshitakiwa atashindwa kuhudhuria mahakamani kujibu mashtaka.

Adhabu ya kukiuka dhamana

Dhamana inayotolewa na Polisi kwa mtuhumiwa anayekabiliwa na kosa la jinai inapaswa kuheshimiwa. Kifungu cha 69 cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai kinatoa adhabu kali kwa mtuhumiwa na mdhamini au wadhamini wanapokiuka masharti ya dhamana waliopewa.

Jacinda Ardern: Waziri mkuu wa New Zealand ahudhuria mkutano wa UN na mwanawe mchanga New York Marekan

Hii ni safari ya kwanza ya kimataifa kwa mtoto Neve tangu alipozaliwa Juni 21

Waziri mkuuu wa New Zealand, Jacinda Ardern ametoa hotuba yake ya kwanza katika kongamano la Umoja wa mataifa mjini New York.

Katika tukio ambalo si la kawaida kiongozi huyo aliingia ndani ya chumba cha mkutano wa shirika hilo la kimataifa akiwa na mtoto wake mchanga.

Japo ameandamana na mpenzi wake Clarke Gayford, Bi Ardern amechukua muda kumchezesha mwanawe mchanga kwa jina Neve Te Aroha, kabla ya kuhutubia baraza kuu la Umoja wa mataifa.

Kiongozi huyo kwa sasa anamnyonyesha bintiye Neve, ambaye ana miezi mitatu. Huu sio uamuzi wa kawaida kwa mwanamke yeyote, ikizingatiwa kuwa angemuacha nyumbani,

kwa siku sita ili aweze kuhudhuria mkutano huo muhimu wa kimataifa.

Arden ameliambia shirika la habari la New Zealanda kuwa mara nyingi yuko na mtoto wake kiiwa nchini New Zealand.

Wakati huu anapohudhuria mkutano wa Umoja wa Mataifa, Bwana Gayford atakua na jukumu la kumtunza mtoto Neve, kama ilivyoandikwa katika kadi inayotambulisha

rasmi uwepo wa mtoto huyo katika ukumbi wa mkutano.

Waziri mkuu wa New Zealand Jacinda Ardern akihutubia mkutano wa baraza kuu la umoja wa mataifa
Mpenzi wake Clarke Gayford,ambaye ni mtangazaji wa televisheni, kwa sasa anamsaidia jukumu la ulezi
Mpenzi wake Clarke Gayford,ambaye ni mtangazaji wa televisheni, kwa sasa anamsaidia jukumu la ulezi

Bi Ardern pia ameliambia gazeti la Herald nchini New Zealand,kuwa atagharamia usafiri na malazi ya mpenzi wake. “Yuko hapa kumtunza mtoto wetu”.

Kiongozi huyo amerejea kazini kutoka likizo ya uzazi mapema mwezi Agosti.

Hii ni safari ya kwanza ya kimataifa kwa mtoto Neve tangu alipozaliwa Juni 21Haki miliki ya pichaREUTERS

Msemaji wa Umoja wa mataifa Stephane Dujarric, amesema “Waziri mkuu Ardern ni kielelezo chema kwa taifa lake na hatua yake ya kuhudhuria mkutano huu akiwa na mwanawe ni ishara wazi kwamba hakuna mwakilishi bora zaidi kwa nchi kuliko mama mchapa kazi”.

Bwana Dujarric, ameongeza kuwa viongozi wanawake duniani ni 5% kwa hiyo wanahitaji kujisikia huru kadiri ya uwezo wao

Luka Modric ateuliwa mchezaji bora wa kiume Fifa, Deschamps kocha bora

Luka Modric mchezaji bora wa Fifa

Kiungo wa kimataifa wa Croatia Madrid Luka Modric,ametangazwa kuwa mchezaji bora wa Fifa wa kiume katika shughuli ya utoaji tuzo iliyofanyika usiku huu London Uingereza.

Modric mwenye miaka 33, amewapiga kumbo mchezaji mwenzake wa zamani wa Real Madrid Cristiano Ronaldo, anayechezea Juventus, kwa sasa pamoja na winga wa Liverpool Mohamed Salah.

Marta Vieira da Silva, ametwaa tuzo ya mchezaji bora kwa mara sita

Kwa upande wa wanawake mchezaji wa timu ya taifa ya Brazil na klabu ya Orlando Pride, Marta Vieira a Silva, ndie aliyechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Fifa na kuwa ni tuzo yake wa sita ya uchezaji bora akiwazidi Dzsenifer Marozsan na Ada Hegerberg.

Kocha wa mabingwa wa kandanda duniani Ufarasansa Didier Deschamps ameibuka kidedea kuwa ndie kocha bora na kuwapiku Zinedine Zidane na kocha wa timu ya taifa ya Croatia Zlatko Dalic

HaDidier Deschamps ametwaa tuzo ya kocha bora

Mohamed Salah ametwa tuzo ya goli bora(Puskas) goli ambalo alilifungwa dhidi ya Everton mwezi Desemba.Kipa wa zamani wa Chelsea Thibaut Courtois ametajwa kuwa ndie kipa bora .

Pia katika tuzo hizo kulitangazwa kikosi cha wachezaji kumi na moja wa dunia wa Fifa

Nyota kumi na moja wa kikosi cha dunia

 

Mkasa wa MV Nyerere Tanzania : Magufuli avunja bodi ya Sumatra na ile ya ushauri ya Tamesa

Rais John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi wa mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi kavu na majini SUMATRA Mhandisi Dkt. John Ndungura .

Taarifa ya Ikulu iliotolewa siku ya Jumatatu na kusainiwa na mkurugenzi wa mawasiliano ya rais Gerson Msigwa, inasema kuwa kiongozi huyo pia ameivunja bodi hiyo kuanzia leo.

Magufuli alichukua uamuzi huo kufuatia kuzama kwa kivuko cha MV Nyerere na msururu wa ajali za barabarani ambazo zimesababisha vifo, ulemavu na kuharibu mali.

Siku ya Jumapili magufuli alifutilia mbali bodi ya ushauri ya Wakala wa Ufundi na Umeme TAMESA na kumfuta kazi mwenyekiti wake John Ndunguguro kwa sababu kama hizo.

Tume kuchunguza chanzo cha ajali

Shughuli za uopoaji marehemu zikiendelea eneo la tukio
Wanawake wakisubiri miili ya wapendwa ufuoni

Waziri mkuu Kassim Majaliwa tayari ametangaza tume ya watu saba ambayo itaanza uchunguzi kuhusiana na kile kilichosababisha kuzama kwa MV Nyerere ambayo kufikia sasa imesababisha vifo vya abiria 227 ambao walikuwa wakiabiri feri hiyo.

Tume hiyo inaongozwa na afisa mstaafu wa jeshi na mbunge wa upinzani kutoka eneo hilo Joseph Lukundi miongoni mwa wengine.

Tume hiyo imepewa mwezi mmoja kukusanya ripoti na kuiwasilisha kwa rais.

Wakati huohuo, waziri huyo amefichua kwamba serikali imeanza mipango ya kutengeza feri mpya ambayo itakuwa na uwezo wa kubeba watu 200 na tani 50.

Kufikia sasa, serikali tayari imewakamata maafisa kadhaa waliokuwa wakifanya kazi katika feri .

Meli itakayoivuta MV Nyerere yawasili

Baadhi ya waogeleaji waliokuwa wakisaka miili ya watu waliofariki na walionusurika

Tayari meli iliokuwa ikibeba vifaa vitakavyotumika kuitoa kenye maji MV Nyerere imewasili katika eneo la Bwisya katika kisiwa cha Ukara, Wilayani Ukerewe.

Kamishna wa Mwanza John Mongella alisema siku ya Jumapili kwamba meli hiyo itatolewa na wataalam kutoka kwa kikosi cha uokozi wa majini.

Amesema kuwa uokozi wa chombo hicho pia utasaidia kunusuru mali iliokwama chini ya mabaki ya chombo hicho.

Hotuba ya Magufuli

MV Nyerere wakati ilipokuwa ikifanya kazi

Akizungumza moja kwa moja kupitia runinga, rais Magufuli amesema kuwa nahodha huyo tayari amekamatwa na polisi .

Aidha rais Magufuli ameagiza wale wote wanaohusika na operesheni za kivuko hicho kukamatwa ili kuhojiwa. Akihutubia taifa siku ya Ijumaa jioni rais wa Jamhuri ya Tanzania John Pombe Magufuli amesema kuwa ana habari kwamba nahodha huyo alimwachia zamu ya kuendesha chombo hicho mtu ambaye hakuwa amepata mafunzo ya kazi hiyo.

Kulingana na Magufuli huenda sababu ya kuzama kwa chombo hicho ni ‘kujaa kupitia kiasi’.

Lakini amesema kuwa kamati itakayoundwa itasaidia kutoa maelezo zaidi.

Takriban miili 160 imeopolewa kufikia sasa , kulingana na idadi ya mwisho iliotolewa kabla ya rais Magufuli kutoa hotuba yake.

Mustakabali wa mashirika yaliowekeza katika uzazi wa mpango Tanzania?

Magufuli alisema: Ni wazi kwamba miili zaidi imekwama ndani ya chombo hicho, Ripoti nilizopoikea zinaonyesha kuwa hata mizigo iliobebwa ilikuwa zaidi ya kiwango cha tani 25 zinazoruhusiwa.

Kulikuwa na tani za mahindi, kreti za pombe, vifaa vya umeme na Ujenzi. Abiria pia walikuwa wamebeba mizigo mikubwa kwa kuwa walikuwa wanatoka katika soko.