Koffi Olomidé: Nyota wa muziki Congo ahukumiwa Ufaransa kwa kupatikana na hatia ya ubakaji wa mtoto wa miaka 15

Koffi Olomidé from DR Congo and dancers of the Quarter Latin group, perform 30 April 2005 at the Iba Mar Diop stadium in Dakar
Koffi Olomidé , katika picha hii mnamo 2012 amehukumiwa akiwa hayupo mahakamani

Koffi Olomidé, mojawapo ya nyota wa muziki Afrika , amepatikana na hatia kwa ubakaji wa mojawapo ya wanengeuaji wake alipokuwa miaka 15.

Amehukumiwa miaka miwili gerezani na mahakama ya Ufaransa akiwa hayupo, baada ya kukosa kufika mahakamani.

Uamuzi huo una maana kwamba nyota huyo wa Congo atakamatwa iwapo atatekeleza uhalifu mwingine, anasema mwandishi wa BBC Nadir Djennad.

Olomidé, mwenye umri wa miaka 62, aliagizwa alipe Euro 5,000 kwa madhara aliyomsababishia mnenguaje wake huyo wa zamani.

Mahakama ya Nanterre, nje ya mji mkuu Paris, pia ilimuagiza alipe faini ya kiwango sawa kwa kuwasaidia wanawake watatu wengine kuingia nchini Ufaransa kwa njia haramu.

Wakili wa Olomidé amepongeza uamuzi huo na kuutaja kuwa ushindi, akiwarifu waandishi habari kwamba uamuzi huo utachangia kuondolewa waranti wa kimataifa wa kumkamata.

Koffi Olomide atoa wimbo mpya kuwaomba msamaha akina mama Afrika

Koffi Olomidé ni nyota wa muziki wa mtindo wa rumba na soukous ambao ni maarufu sana barani Afrika.

Olomidé alishtakiwa mara ya kwanza mnamo 2012 kwa ubakaji wa kimabavu lakini mashtaka yakapunguzwa.

Wanenguaji wanne waliokuwa wakimfanyia kazi wameiambia mahakama kwamba aliwanyanyasa kingono mara kadhaa kati ya mwaka 2002 na mwaka 2006. Wameeleza kuwa unyanyasaji huo ulifanyika katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na Ufaransa.

Wanawake hao pia walieleza kwamba walizuia kwa lazima katika nyumba moja nje ya mji wa Paris na walifanikiwa kutoroka usiku wa Juni 2006, lakini hawakurudi DR Congo kutokana na kuogopa kutafutwa na kulipizwa kisasi.

Waendesha mashtaka walikuwa wakishinikiza ahukumiwe miaka 7 gerezani lakini mahakama imetupilia mbali mashtaka ya unyanyasaji na madai ya utekaji nyara.

Olomidé alikimbilia Congo mnamo 2009 akiahidi kujitetea lakini alikosa kufika mahakamani Ufaransa katika kesi hiyo ambayo kutokana na ombi la walalamishi ilifanyika faraghani.

Muimbaji huyo ambaye jina lake halisi ni Antoine Agbepa Mumba, amejipata mashakani na sheria kwa mara kadhaa:

 • 2018 Zambia iliagiza akamatwe baada ya kutuhumiwa kumshambulia mpiga picha
 • 2016 alikamatwa na kutimuliwa baada ya kumshambulia mojawapo ya wanenguaji wake Kenya
 • 2012 alishtakiwa DR Congo kwa kumshambulia produza wake na kuhukumiwa kifungo cha miezi mitatu ambacho angefungwa iwapo angetekeleza uhalifu mwingine
 • 2008 alishutumiwa kumpiga teke mpiga picha katika kituo cha Televisheni DR Congo RTGA na kuivunja kamera yake katika tamasha , lakini walipatanishwa baadaye.

Kimbunga Idai: Serikali ya Tanzania imetoa msaada wa dawa, chakula na vifaa vya kujihifadhi kwa nchi za Msumbiji, Malawi na Zimbabwe

Mji wa Beira
Tayari kuna hatari ya maisha ya zaidi ya watoto 100,000 na watu wazima kufuatia kimbunga hicho huku mito katika maeneo yaliothirika zaidi ikivunja kingo zake , kulingana na shirika la Save the Children.

Serikali ya Tanzania imetoa msaada wa dawa, chakula na vifaa vya kujihifadhi kwa nchi za Msumbiji, Malawi na Zimbabwe kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa kimbunga cha Idai kilichosababisha mafuriko yaliyozikumba nchi hizo tangu wiki iliyopita.

Msaada huo umekabidhiwa kwa Mabalozi wa nchi hizo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Sehemu ya msaada huo utapelekwa nchi za Zimbabwe na Msumbiji unatarajiwa kusafirishwa kwa kutumia ndege za Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Akizungumza wakati zoezi la kupakia msaada huo katika ndege ya Jeshi likiendelea Mhe. Prof. Kabudi amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ameagiza kutolewa kwa msaada huo sambamba na salamu za pole kwa Marais wa Msumbiji, Malawi na Zimbabwe pamoja na wananchi wa nchi hizo kwa madhara makubwa waliyoyapata kutokana na mafuriko hayo.

Ramani ya maeneo yalioathirika na mafuriko

“Rais Magufuli baada ya kupata taarifa hizi na kuzungumza na Marais wenzake wa Msumbiji, Malawi na Zimbabwe, Tanzania imeona ni vyema kutokana na undugu wetu, umoja wetu na ujirani wetu tuweze kuwapelekea msaada angalau kidogo wa dawa na chakula na pia kuwapa pole kwa maafa haya makubwa yaliyowapata” amesema Prof. Kabudi.

Idadi ya watu waliofariki kutokana na kimbunga Idai nchini Msumbiji sasa huenda ikawa ya juu na kufikia watu 1000 rais Filipe Nyusi amesema.

Bwana Nyusi alisafiri kwa ndege katika maeneo yalioathirika zaidi siku ya Jumatatu. Alielezea kuona miili ikielea juu ya mito.

Tayari kuna hatari ya maisha ya zaidi ya watoto 100,000 na watu wazima kufuatia kikmbunga hicho huku mito katika maeneo yaliothirika zaidi ikivunja kingo zake , kulingana na shirika la Save the Children.

Helikopta za kijeshi zimetumiwa kusafirisha chakula cha msaada MalawiHaki miliki ya pichaAFP
Image captionHelikopta za kijeshi zimetumiwa kusafirisha chakula cha msaada Malawi

Mafuriko yaliofanyika mapema mwezi huu yamezidishwa na kimbunga Idai ambacho kilikumba eneo la kaskazini mwa Msumbiji mnamo tarehe 15 mwezi Machi 2019 na kusababisha unahiribifu mkubwa wa nyumba , shule, hospitali na miundo mbinu.

Kulingana na serikali ya Msumbiji takriban watu 600,000 wameathiriwa , huku maisha ya zaidi ya watu 1000 yakidaiwa kupotea huku yale ya watu 100,000 yakihitaji msaada wa dharura mjini Beira.

Kiwango cha janga hilo kinazidi kuongezeka kila dakika na shirika la Save the Children lina wasiwasi mkubwa kuhusu watoto na familia walio katika hatari huku viwango vya mafuriko vikizidi kuongezeka anasema Machel Pouw mkuu wa operesheni ya shirika hilo nchini Msumbiji.

Huge crater opened up by raine and floods

Kimbunga hicho kilishuka katika mji wa bandari wa Beira siku ya Alhamisi kikiwa na upepo wenye kasi ya hadi kilomita 177 kwa saa , lakini mashirika ya misaada yalifika katika eneo hilo siku ya Jumapili.

Mfanyikazi mmoja wa Umoja wa mataifa aliambia BBC kwamba kila nyumba mjini Beira- ambapo ni mji wenye makaazi ya watu nusu milioni iliharibiwa.

Gerald Bourke, kutoka kwa shirika la chakula duniani , alisema: Hakuna nyumba ambayo haikuathiriwa . hakuna Umeme, hakuna mawasiliano.

Barabara zimejaa magogo ya nyaya za umeme. Paa za nyumba zimeanguka pamoja na nyuta zake. raia wengi wa mji huo wamepoteza makaazi yao.

Idadi rasmi ya watu waliofariki nchini Msumbiji inadaiwa kuwa watu 84 kufuatia mafuriko na upepo mkali.

Kimbunga hicho kimewaua takriban watu 180 katika eneo lote la Afrika Kusini.

Shirika la msalaba mwekundu limeelezea uharibifu huo kuwa mbaya zaidi na wa kutisha. Watu wamelazimika kuokolewa wakiwa juu ya miti , Jamie LeSeur mkuu wa IFRC aliambia BBC.

Baadhi ya watu walikuwa wametafuta hifadhi juu ya miti

Watu 1000 wahofiwa kufariki kutokana na kimbuga Msumbiji

Nchini Zimbabwe takriban watu 98 wamefariki huku 217 wakiwa hawajulikani waliko mashariki na kusini serikali imesema.

Idadi ya watu waliofariki inashirikisha wanafunzi wawili wa shule ya St Charles Lwanga katika wilaya ya Chimanimani, ambao walifariki baaada ya bweni lao kuathiriwa kutokana na mawe yaliosombwa na maji hayo katika mlima.

Nyumba zilizosombwa na mafurikoHaki miliki ya pichaAFP
Image captionNyumba zilizosombwa na mafuriko

Malawi pia nayo iliathiriwa vibaya . Mafuriko nchini humo yaliosababishwa na mvua kabla ya kimbunga hicho kuwasili yalisababisha mauaji ya vifo 122 kulingana na mitandao ya mashirika ya misaada.

Serikali ya Uingereza inasema kuwa itatoa msaada wa kibinaadamu wenye thamani ya £6m kwa Msumbiji na Malawi.

Pia imesema kuwa itatuma mahema pamoja na maelefu ya mahema nchini Msumbiji.

Uharibifu wa Beira ni mkubwa kiasi gani?

Wengi wa wale wanaojulikana kufariki waliuawa karibu na mji wa Beira , ambao ndio mji mku wa nne kwa ukubwa ukiwa na idadi ya watu isiopungua nusu milioni kulingana na mamlaka.

Zaidi ya watu 1500 walijeruhiwa na miti pamoja na vifusi vilivyoanguka ikiwemo paa , kulingana na maafisa katika mji mkuu wa Maputo waliozunguzma na BBC.

”Karibu kila kitu kimeathiriwa na janga hili” , Alberto Mondlane , gavana wa mkoa wa Sofala unaoshirikisha Beira alisema siku ya Jumapili. Tuna watu wanaotaabika kwa sasa , wengine juu ya miti na wanahitaji sana msaada.

Mji wa bandari wa Beira uliathirika pakubwa na kimbunga hicho.Haki miliki ya pichaAFP
Image captionMji wa bandari wa Beira uliathirika pakubwa na kimbunga hicho.
Picha ya juu ya mji wa BeiraHaki miliki ya pichaIFRC/CAROLINE HAGA
Image captionShirika la msalaba mwekundi lilisafri kwa ndege likichunguza uharibifu wa kimnbunga hicho mjini Beira

”Wakaazi wa Beira wamefanya juhudi za kujaribu kufungua barabara za mji huo”, bwana LeSeur aliambia BBC.

Barabara inayounganisha Beira na maeneo mengine ya taifa hilo iliharibiwa vibaya, lakini usafiri wa ndege hadi maeneo yalioathirika pakubwa umeanzishwa.

Rais Filipe Nyusi alikata ziara yake ya Swaziland ili kutembelea maeneo yalioathirika.

Je hali ikoje nchini Zimbabwe?

Hali ya janga imetangazwa nchini Zimbabwe . Rais Emmerson Mnangagwa amerudi nyumbani mapema kutoka kwa ziara ya kuelekea UAE ili kuhakikisha kuwa anashiriki moja kwa moja katika janga hilo la kitaifa , mamlaka imesema.

Wizara ya habari imesambaza picha za wanafunzi kutoka shule ya St Charles Lwanga , ambao kwa sasa wameokolewa.

Presentational white space

Manusura katika hospitali moja katika wilaya ya Chimanimani walizungumza kuhusu vile mafuriko hayo yalivyoharibu nyumba zao na kuwasomba wapendwa wao.

”Hadi sasa sijui ni wapi mwangu yupo” , Jane Chitsuro aliambia shirika la habari la AFP . ”hakuna samani , hakuna nguo ni vifusi na mawe pekee’.

Nyumba ya Praise Chipore pia nayo iliharibiwa .

”Mwanangu alikuwa nami kitandani akasombwa na mafuriko huku mafuriko makubwa yakinisomba mie pia”, alisema.

Praise Chipore, 31, alikuwa akiemndelea kupata matibabu hospitalini ChimanimaniHaki miliki ya pichaAFP
Image captionPraise Chipore, 31, alikuwa akiemndelea kupata matibabu hospitalini Chimanimani
Presentational grey line

Je umewahi kuona tukio kama hili hapo awali

Mwandishi wa BBC Shingai Nyoka, nchini Zimbabwe anaripoti.

Safari yangu kuelekea Chimanimani iliisha ghafla wakati tulipofika katika eneo hili .

Maji ya mto yalikuwa yakipita kwa nguvu huku watu kadhaa wakiwa wamesimama katika pande mbili za daraja hili.

Shimo kubwa lililosababishwa na mafuriko

Hii ndio iliokuwa barabara kuu iliokuwa ikiunganisha mji wa Mutare kuelekea kijiji cha Chimanimani ambayo imekatwa .

Mashirika ya misaada yameshindwa kufika katika eneo hilo. Wakaazi wanaoishi katika eneo hilo wanasema kuwa hawajashuhudia tukio kama hilo.

Wanandoa wawili walio na umri mkubwa , Edson na Miriam Sunguro waliniambia kwamba wamejaribu kuwasiliana na wapendwa wao katika eneo la Chimanimani bila mafanikio.

Presentational grey line

Je hali ya hewa itabadilika?

“Kuna hatari ya mvua kubwa zaidi kunyesha katikja kipindi cha siku chache zijazo katika eneo la kaskazini mwa Msumbiji pamoja na kusini mwa Malawi , kulingana na mwandishi wa hali ya hewa wa BBC Chris Fawkes says.

Huenda kukawa na ngurumo za radi , aliongezea, lakini kuna picha za mawingu yaliowachwa na Kimbunga idai ambayo huenda yakazuia ngurumo za radi kuanza.

Kenya: Raia watumia mitandao ya kijamii kuitaka serikali iwajibike na baa la njaa

Mama mzee ambaye amekumbwa an ukame eneo la Turkana nchini Kenya
Wazee, watoto, wanawake wajawazito na watu wenye ulemavu wanaendelea kuumia kutokana na ukosefu wa chakula na maji.

Huku Wakenya wakiendelea kujadili haja ya serikali kushughulikia ukame, makali ya njaa yanaendelea kushuhudiwa katika kaunti ya Turkana ambayo imekumbwa na ukame.

Chini ya #WeCannotIgnore , Wakenya kupitia mitandao ya kijamii wamekuwa wakiitaka serikali ichukua hatua juu ya njaa inayoendelea kusababisha vifo .

Mjadala huo unaendelea huku idadi ya watu waliokufa kutokana na njaa ikipanda ambapo shule zimelazimika kufungwa huku wanafunzi wakiwafuata wazazi wao kwenye maeneo ya misitu kutafuta chakula.

Wakenya wanauliza ‘Ni nini kilitokea kwa mfumo unaotoa taarifa za mapema za maafa?’ na kwanini Wakenya wanakabiliana na njaa, katika nchi ambayo usalama wa chakula imekuwa ndio ajenda inayopewa kipaubele zaidi?.

Wazee, watoto, wanawake wajawazito na watu wenye ulemavu wanaendelea kuumia kutokana na ukosefu wa chakula na maji.

”Kila kijiji ninachotembelea, nakutana na kina mana na watoto pekee, hali yao ya afya ikiwa imedorora kabisa. Mifupa kwenye miili yao inaonekana ishara kuwa wamestahimili njaa kwa siku kadhaa” amesema mwandishi wa BBC Faith Sudi aliyetembelea eneo la Turkana. na kuongeza kuwa hata miti ya miiba ambayo inajulikana kustahimili na kushamiri katika mazingira ya jangwa imekauka.

Masomo ni miongoni mwa huduma ambazo zimekatizwa katika vijiji vingi ambavyo ukame umekithiri.

Katika shule ya msingi ya Lotukumo iliyoko katika kaunti ndogo ya Turkana ya Kati, wanafunzi wa darasa la nane pekee ndio wako madarasani kwa wote.

“Kwa sababu ya ukosefu wa chakula, wanafunzi wengi wanajiunga na wazazi wao kutafuta chakula popote watakapopata, kwa hiyo hawawezi kufika shuleni” anasema mwalimu mkuu wa shule hiyo Ebong’on Charles.

Mbunge Mwakilishi wa Wanawake katika kaunti ya Turkana Joyce Emanikor.
Image captionMbunge Mwakilishi wa Wanawake katika kaunti ya Turkana Joyce Emanikor anasema baa la njaa linapaswa kuwa historia nchini Kenya.

Darasa la pili ambalo kwa kawaida huwa na wanafunzi 70, liko na wanafunzi 11 pekee.

Darasa la kwanza halina mwanafunzi hata mmoja kwa muda wa wiki mbili sasa.

Katika kijiji cha Nadoto, nyumba nyingi havina watu. Waliobakia katika maboma ni wanawake hasaa wajawazito, wakongwe na watoto wadogo.

Bi Selina Ebei ana mimba ya miezi saba lakini amelazimika kulala siku kadhaa bila chakula.

“Kutokana na hali yangu siwezi kwenda mwituni kila siku kutafuta matunda ya Mkoma kwa sababu ni mbali na jua pia ni kali mno. Wakati mwingine ninakaa siku tano bila kutia chochote mdomoni.”

Mzee akinywa maziwa ya paketi ya msaada eneo la Turkana
Image captionKatika kijiji kimoja nyumba nyingi hazina watu wamebakia wanawake hasaa wajawazito, wazee na watoto wadogo, huku wanaume wakienda msituni kutafuta matunda mwitu

Selina ana mtoto mdogo mwenye umri wa miaka miwili na ambaye pia anamtegemea.

“Mikoma niliyochuna ikiisha, tunakaa njaa tu hadi nitakapojikaza tena kwenda mwituni kuchuma Mikoma ingine. Ninambeba huyu mwanangu mgongoni na kutembea mwendo mrefu kwa sababu hakuna mtu ambaye ninaweza kumwachia amchunge.”

“Tunayachemsha na kukunywa supu yake”

Wanaume hawako vijijini kwani wameenda na mifugo kwenye milima kuwatafutia chakula

Mbunge Mwakilishi wa Wanawake katika kaunti ya Turkana anasema kwamba wakati huu ambapo kuna serikali ya Kaunti, baa la njaa linapaswa kuwa historia.

“Ni aibu sana watu kufariki kutokana na baa la njaa katika kaunti ambayo inapokea mgao mkubwa wa mapato. Serikali ya Kaunti iko na uwezo mkubwa kuhakikisha wakaazi wanapata chakula cha kutosha wakati wa janga Kama hili”. Anasema Joyce Emanikor.

Kulingana na ripoti kutoka Kwa Wizara ya Majanga na huduma Kwa umma ya kaunti ya Turkana, wakaazi wengi katika kaunti ya Turkana hutegemea ufugaji ili kujikimu kimaisha.

Kwa sasa zaidi ya mifugo 30,000 wamefariki na wengine zaidi ya 100,000 wamehamishwa nchi jirani ya Uganda.

“Tumepoteza mifugo wengi kutokana na ukosefu wa usalama, kisha wale mifugo wadogo ambao wamesalia wanauawa na ukame. Ni sharti serikali ya Kaunti hii irejelee bajeti yake ili kuhakikisha kwamba inazingatia zaidi mahitaji ya wakaazi wa eneo hili. Na iwapo fedha zitatengwa kushughulikia ukame zisifujwe.” anasema Joyce Emanikor.

Naibu rais wa Kenya William Ruto amepuuzilia mbali madi kuwa watu wamekufa kutokana na njaa nchini Kenya
Image captionNaibu rais wa Kenya William Ruto alisema kuwa Kenya iko katika fursa nzuri sasa ya kukabiliana na ukame ikilinganishwa na miaka iliyopita.

Serikali hata hivyo imekanusha taarifa kwamba watu kadhaa wamekufa kutokana na njaa inayosababishwa na ukame ambao kwa sasa umeyaathiri maeno ya kaskazini magharibi mwa nchi .

Waziri wa tawala za kaunti Eugene Wamalwa amesema kulikuw ana vifo , lakini akaongeza kuwa haviwezi kuhusishwa na ukame.

Mwisoni ma juma, gazeti la, Daily Nation nchini humo liliripoti kuwa watu kadhaa walikufa kutokana na matatizo yenye uhusiano na njaa katika eneo la Tiaty kaunti ya Baringo.

Gazeti hilo lilisema familia zilizoathirika zilikuwa zinaishi kwa matund ya mwitumi ambayo yanachemshwa kwa saa kadhaa ili kumaliza sumu iliyomo kwenye matunda hayo.

Wakati huo huo Naibu rais wa Kenya William Ruto alisema kuwa Kenya iko katika fursa nzuri sasa ya kukabiliana na ukame ikilinganishwa na miaka iliyopita na akapinga madai kwamba watu wamekufa kutokana na njaa.

Ruto alisema kuwa nchi inachakula cha kutosha na kuongeza kuwa hakuna haja ya kuwa na hofu.

Ugoro huwekwa sehemu za siri ukichanganywa na mafuta na magadi

Ugoro
Baadhi ya wanawake Tabora hutumia ugoro kupunguza hamu ya tendo la ndoa

waswahili husema ukistaajabu ya musa utaona ya Firauni, Je unajua matumizi yote ya tumbaku ?

Mkoani Tabora nchini Tanzania wanawake wamekua wakitumia Tumbaku ili kupunguza hamu ya tendo la ndoa. Huweka sehemu ya siri kisha kuitoa baada ya muda.

Tabia hiyo imezoeleka sana miongoni mwa wanawake wasio na wenza wao, ikiwemo wajane. Lakini kwa upande wa afya, wako salama?

Wanawake hususani wasio kuwa katika uhusiano na wanaume ama kuolewa hutumia njia kumaliza hamu zao.

Je unayajua matumizi ya nyuklia kando na kuunda mabomu?

Fahamu vyanzo vya vifo vingi duniani?

”Mimi ni mjane, natumia tumbaku katika kumaliza hamu zangu kwasababu sina mwanaume na wala sitaki mwanaume mwingine, kwa wiki naweka mara mbili” anasema Zaituni shabani mmoja ya wanawake wanaotumia tumbaku sehemu za siri.

Wanawake wengine nilizunguma nao kama asha, si jina lake halisi anasema kuwa anatumia tumbaku kwasababu alikimbiwa na mwanaume wakati ana ujauzito.

” kwakeli sitaki kusikia tena wanaume mi nitabaki na tumbaku, mana nikitumia hamu yote inaisha sina haja tena” anasema asha

Wanawake wote niliozunguma nao wanakiri kuwa matumizi ya tumbaku sehemu za siri huwasaidia kumaliza hamu ya tendo la ndoa.

Tumbaku
Image captionTumbaku ikiwa shambani

TUMBAKU INATUMIWA VIPI SEHEMU ZA SIRI?

Kwa mujibu wa wanawake hawa huchukua majani makavu ya tumbaku kisha kutangwa na baada ya hapo huchanganya na mafuta kidogo pamoja na magadi, ama na mara nyingine hutumia ugoro kufanya mchangayiko huo. Baada ya hapo huweka sehemu za siri na kisha hupata muwasho ambao ndio humaliza haja ya tendo la ndoa.

” mi huwa napaka mara mbili kwa wiki na huwa naweka kwa muda kidogo kabla niondoe na kisha napata muwasho, na wala sipati maumivu yoyote nikimaliza matamanio yangu ya kufanya tendo la ndoa yanakua yameisha” anasema zaituni.

Kwa kawaida wanawake hawa baada ya kupaka tumbaku ama ugoro sehemu za siri husikia kama wamekutana kimwili na wanaume.

WANAUME WANASEMA NINI?

Katika kijiji cha ugala suala hili ni jambo la kawaida miongoni mwa wanawake lakini kwa upande wa wanaume si wengi wanajua , na wanaojua wanasema kuwa imekua siri baina ya wanawake.

“Mimi nimekua nikisia lakini mara nyingi ni kwa bahati mbaya wao wakiongea, na nikuwaliza , wanasema ni siri yao ni baina ya wanawake na si wanaume”. Anasema mzee Usantu mmoja wa wakazi wa kijiji cha Ugala.

Wanawake hawana uelewa wa kutosha kuhusu athari za tumbaku
Image captionWataalamu wa magonjwa ya wanawake wanasema matumizi haya yana athari kiafya

KUNA ATHARI ZOZOTE KIAFYA?

Kwa mujibu wa baadhi ya wanawake wanaotumia tumbaku sehemu zao za siri, wanasema hawajawahi kupata tatizo lolote kiafya.

Lakini mtaalamu wa magonjwa ya akina mama anasema kuwa baadhi ya wanawake wanaokutwa na viashiria vya saratani hasa ya kizazi wamekua na historia ya kutumia tumbaku sehemu za siri

“Hatuna utafiti wa moja kwa moja lakini data za kwetu hapa wakati tunawahoji tabia za mazoea walizonazo baadhi wamekiri kutumia tumbaku , hivyo hiyo inaweza kuwa miongoni mwa sababu na kama viashiria vingine vikiwepo” anasema daktari…

Matumizi haya ya tumbaku kwa asilimia kubwa yamechangiwa na uelewa mdogo wa wanawake wa kijiji cha ugala, juu ya madhara ya kiafya wanayoweza kupata.

Ethiopia Airline yasitisha safari za Boeing 737 Max 8, Mkurugenzi aeleza

Boeing 737 Max

Mkurugenzi wa shirika la Ndege la Ethiopia ametaka kusitishwa kwa ndege aina ya Boeing 737 Max 8 mpaka itakapothibitishwa kuwa ziko salama kuruka

Nchi nyingi tayari zimesitisha kurusha ndege hizo baada ya ajali ya siku ya Jumapili iliyogharimu maisha ya watu 157.

Tewolde Gebremariam ameiambia BBC kuwa ingawa sababu ya ajali hiyo haijajulikana bado, kuna ufanano na ile ajali ya ndege ya Lion Air mwezi Oktoba mwaka jana.

Lakini maafisa nchini Marekani wanasema ndege hiyo ni salama.

Marekani: Boeing 737 Max 8 ni salama

Mamlaka ya anga nchini Marekani imesema ”hakuna tatizo lolote katika ufanyaji wake kazi” na kuwa hakuna sababu ya msingi ya kusitisha safari zake.

Mabaki ya Ndege iliyopata ajaliHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionUchunguzi ukifanywana wataalamu katika eneo ajali ya Ndege ilipotokea

‘Kusitisha safari za ndege ni hatua nzuri’

Bwana Tewolde amesema Boeing na mamlaka ya anga nchini Marekani FAA wanaweza kuwa na sababu ya kusema kuwa 737 Max 8 ni salama.Lakini ”tahadhari kubwa” ilihitajika na wale waliositisha kuruka kwa ndege hiyo bila shaka wana sababu ya kufanya hivyo.”

Ndege zote zilikua mpya na ndege zote zilianguka dakika chache baada ya kuruka alieleza

Mamlaka za anga ikiwemo za Umoja wa Ulaya,Hong Kong,Singapore,China na Australia, zimesitisha ndege za 737 Max kuruka kwenye anga zake

Bwana Tewolde amesema mamlaka hizo zina sababu nzuri ya kufanya hivyo kwa kuwa usalama ni jambo muhimu na ”kusitisha safari ni jambo la jema”.

Wakati hayo yakijiri, wanasiasa kadhaa wa Marekani wametoa wito kwa FAA kusitisha safari za ndege aina hiyo kwa muda mpaka pale itakapothibitishwa .Lakini FAA imesema mamlaka zingine hazijatoa data zinatakazofanya Marekani ichukue hatua hiyo

Boeing imesema kuwa ina uhakika kuwa ndege ilikua salama kuruka.

Shirikisho la wafanyakazi wa ndege CWA limetaka kusitishwa kwa ndege 737 MAX kwa ” tahadhari” Umoja wa marubani umesema wanachama ambao wanawasiwasi kuhusu usalama hawatalazimishwa kurusha ndege hizo.

Southwest Airlines na American Airlines wanaendelea kutumia ndege hizo.

Kylie Jenner amekuwa bilionea mwenye umri mdogo zaidi duniani

Kylie Jenner

Kylie Jenner amekuwa bilionea mwenye umri mdogo zaidi duniani, kwa mujibu wa orodha ya mabilionea ya gazeti la Forbes.

Kylie ambaye ndiye mdogo zaidi katika familia ya Kardashian amepata utajiri wake kutokana na biashara ya vipodozi.

Akiwa na umri wa miaka 21-alianzisha na anamiliki kampuni ya vipodozi ya Kylie Cosmetics, biashara ya urembo ambayo imedumu kwa miaka mitatu sasa na kuingiza mapato ya takriban dola milioni $360m mwaka jana.

Alifikia mafanikio haya mapema kuliko muasisi wa mtandao wa kijamii wa Facebook Mark Zuckerberg ambaye alikuwa bilionea akiwa na umri wa miaka 23.

“Sikutarajia chochote. Sikujua hali ya baadae.

“Lakini kutambuliwa inafurahisha. Ni jambo zuri la kunitia moyo,” Bi Jenner aliliambia jarida la Forbes.

Shughuli zakwama katika uwanja wa ndege Kenya

Orodha ya Forbes inaonyesha muasisi wa The list shows Amazon , Jeff Bezos, akiendelea kushikilia nafasi ya kwanza kwa binadamu tajiri zaidi duniani.

Jumla ya utajiri wake ni dola bilioni $131 ,kulingana na jarida la Forbes, ameongeza hadi dola bilioni 19bn kutoka mwaka 2018.

Lakini kiwango cha mapato ya mabilionea wote kwa ujumla kimeshuka kutoka dola trilioni $9.1

Miongoni mwa mabilionea ambao utajiri wao unapungua ni muanzilishi wa Facebook Mark Zuckerberg.

Umeshuka kwa dola bilioni $8.7bn katika kipindi cha mwaka uliopita ulishuka kwa dola bilioni $62, kwa mujibu wa orodha ya jarida la Forbes

Hisa zake katika Facebook wakati mmoja zilipungua kwa thamani yake ya theluthi moja wakati kampuni ilipokua ikikabiliana na kashfa. Hisa za kampuni ya mauzo ya mtandaoni ya Amazon zimefanya vizuri na hivyo kuboresha akaunti za benki za Bwana Bezos na mwanya kati yake na Bill Gates, ambaye yupo katika nafasi ya pili ni mpana kiasi, ingawa utajili wa bwana Gates umepanda kwa doala $96.5bn kutoka dola $90bn alizokuwa nazo mwaka jana.

Kwa mabilionea wote waliotajwa kwenye orodha hiyo ni wanawake 252 tu na mwanamke tajiri zaidi aliyejitafutia utajiri mwenye ni mogul Wu Yajun wa Uchina kupitia kampuni yake ya makazi , akiwa na utajiri wenye thamani ya takriban dola bilioni $9.4bn.

Idadi ya wanawake waliojitafutia utajiri wao imeongezeka kwa mara ya kwanza na kufikia hadi wanawake 72 kutoka wanawake 56 mwaka jana.

Mkurugenzi Mkuu wa Amazon Jeff BezosHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionJeff Bezos – bado ni tajiri anayeendelea kuwa tajiri

Orodha ya jarida la The Forbes ya mabilionea ni kielelezo cha utajiri cha tarehe 8 Februari 2019.

Gazeti hilo hutumia viwango vya bei katika masoko ya hisa vya siku hiyo na viwango wa mauazo ya pesa kutoka kote duniani.

Kulingana na Forbes kuna mabilionea wachache wakiwemo takribani 2,153 miongoni mwao wakiwa katika orodha ya mwaka 2019, kiwango hicho kikiwa kimeshuka ambapo mwaka 2018 vwalikuwa 2,208 . Kwasehemu moja , hii inaelezea ni kwa nini wastani wa utajiri wao ni sawa na thamani ya dola $4bn, ikiwa ni chini ya dola bilioni 4.1bn.

Forbes pia ilibaini kwamba mabilionea 994 miongoni hali yao ya utajiri sio nzuri ikilinganishwa na mwaka jana.

Luisa Kroll, ambaye ni naibu mhariri wa masuala ya utajiri katika jarida la Forbes, amesema: “Hata nyakati za mtikisiko wa uchumu na raslimali mjasiliamali hupata njia za kupata utajiri .”

Mabilionea duniani

Watu wenye utajiri zaidi duniani

Kuna raia 52 wa Uingereza kwenye orodha. Walioko juu ni Hinduja brothers, Srichand na Gopichand, ambao wanamiliki Hinduja Group, wakiwa na jumla ya utajiri wenye thamani ya dola bilioni $16.9bn.

Nyuma yao ni James Ratcliffe, muasisi wa kampuni ya kemikali ya Ineos, mwenye utajiri wa dola bilioni $12.1bn, ambaye ametajwa kama tajiri binafsi.

Jim RatcliffeHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionJim Ratcliffe humiliki asilimia 60% ya kampuni ya Ineos, kampuni ya kemikali aliyoianzisha

Tajiri mwingine anayeibuka ni Safra Catz ambaye ni Mkurugenzi mwenza wa kampuni ya programu ya Oracle, ambaye kwa mujibu wa jarida la huingiza mapato ya dola milioni $41m ya mshahara na ameorodheshwa kama mmoja wa wakurugenzi wanawake wanaolipwa mshahara mkubwa zaidi duniani.

Mark ZuckerbergHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionHisa za kampuni ya Facebook ziliporomoka na kupunguza utajiri wa Mark Zuckerberg

Marekani ina mabilionea 607, idadi hiyo ikiwa ni kubwa kuliko nchi nyingine yoyote duniani.

Uchina inachukua nafasi ya pili ikiwa na mabilionea 324. Lakini orodha ya mabilionea imeshuhudia mabadiliko makubwa – ina mabilionea wapya 44 kwenye orodha huku 102 wakitoka kwenye orodha hiyo.

Kuhuka kwa thamani ya euro kumewaponza mabilionea wa Ulaya ambao hawakujitokeza kwa wingi kwenye orodha ya matajiri wa dunia, huku wakionekana wawili tu miongoni mwa watu 20 tajiri zaidi dunia. : Mkurugenzi mkuu wa kammpuni ya Ufaransa ya bidhaa za burudani LVMH Bernard Arnault (aliwekwa nafasi ya 4), na muasisi wa kampuni ya Index inayomiliki maduka kama Zara-Amancio Ortega (akaorodheshwa katika nafasi ya 6 ).

Forbes linasema kuwa watu 247waliokuwemo kwenye orodha ya mabilionea mwaka jana kwa sasa wametoka. Miongoni mwao ni Domenico Dolce na Stefano Gabbana, wanamitindo na waanzilishi wa Dolce & Gabbana.

Mwenyekiti wa kampuni ya usambazaji wa bidhaa Li & Fung, Victor Fung, pia hayupo tena miongoni mwa mabilionea wa jarida la Forbes, baada ya kuwepo kwenye ododha hiyo kwa miaka 18

Rais wa Algeria Bouteflika, amesema hatagombea muhula mwigine wa Urais

Abdelaziz Bouteflika

Rais wa Algeria Abdelaziz Bouteflika, amepeleka mbele uchaguzi wa urais uliotakiwa kufanyika tarehe 8,april na kusema kuwa hatagombea tena,

Nia ya kugombea kwake ilizuia maandamano ya nchi nzima kwa wiki kadhaa sasa.

Ameongoza Algeria kwa miaka 20 sasa, lakini hajaonekana muda mrefu katika maeneo ya wazi , kutokana na ugonjwa wa kiharusi alioupata mwaka 2013.

Tarehe mpya ya uchaguzi haijatajwa bado, mabadiliko katika baraza la mawaziri yatafanyika hivi karibuni, taarifa iliyotolewa kwa niaba ya Bouteflika imetoa maelezo hayo.

Hakukua na tamko kuwa rais huyo atajiuzulu kabla ya tarehe mpya ya uchaguzi.

Rais BouteflikaHaki miliki ya pichaAFP
Image captionwaandamanaji wakitumia picha za kukejeli kwa Rais Bouteflika

Wakati huo huo, waziri mkuu wa Algeria Ahmed Ouyahia alijiuzulu na nasafi yake kuchukuliwa na waziri wa mambo ya ndani Noureddine Bedoui ambaye anakumbwa na kazi kubwa ya kutengeneza serikali mpya.

Bouteflika alisema nini?

”hakutakua na muhula wa tano” ilisema taarifa kutoka kwa Rais Bouteflika, ”hakuna maswali katika hilo, ukizingatia hali yangu ya kiafya, na umri wangu, kazi yangu ya mwisho kwa watu wa Algeria ni kuhakikisha wanapata uongozi mpya” aliendelea kusema katika taarifa yake.

Alisema wiki iliyopita kuwa kama atachaguliwa tena hatokaa sana madarakani atajiuzulu, lakini tamko hilo halikuacha watu kuandamana.

maandamanoHaki miliki ya pichaAFP
Image captionMaandamano yalihamasishwa kupitia mitandao ya kijamii

Tamko la kutogombea kwa rais Bouteflika, limepongezwa na mataifa mengine, ikiwemo Ufaransa, ambapo waziri wa mambo ya nje, Jean-Yves Le Drian amesema ufaransa imefurahishwa na uamuzi huo na kuwa ni wakati wa kupata serikali mpya.

Kiongozi wa kwenye TV

Kwa mara ya mwisho alionekana akihutubia Umma mwaka 2014 -hotuba ya shukrani kwa raia wa Algeria kwa kuuamini utawala wake baaa ya kushinda uchaguzi uliokuwa umetangulia.

Aliahidi kutekeleza suala la mgawanyo wa madaraka, kuupa nguvu upinzani na kuhakikisha haki za raia zinafuatwa.

Baadhi waliona kuwa hii ni ishara ya mabadiliko ya sera katika uongozi , lakini hakua ushahidi wa kuonekana kwake kwa muda mrefu.

Raia wa nchi hiyo wamekua wakibahatika kumuona mara chache kwenye Televisheni akisalimiana na ujumbe kutoka nchi za kigeni wanaofika nchini Algeria.

Au kumuona kwenye ufunguzi wa mkutano mwaka 2016-akionekana amekaa kwenye kiti cha magurudumu, akionekana dhaifu, mwenye uchovu lakini mwenye tahadhari

Mpaka mwaka 2018,ikawa wazi kuwa Chama chake kimempendekeza kuwania tena uchaguzi wa mwaka huu.

Alikua kwenye ufunguzi wa Msikiti na vituo vya treni za umeme katika mji mkuu wa Algiers.Wiki chache baadae alikua kwenye ziara kutazama ujenzi wa Msikiti mkubwa wa tatu duniani uliogharimu dola za Marekani bilioni mbili.

wanda imesisitiza kuwa haijafunga mpaka baina yake na Uganda

Waziri wa mambo ya nje wa Rwanda, Richard Sezibera amekanusha ripoti ya kwamba taifa hilo limefunga mpaka kati yake na Uganda.

Sezibera alisema hayo katika mkutano wake na waandishi wa habari katika makao makuu ya wizara ya mambo ya nje mjini Kigali mapema leo Jumanne.

”Shughuli ya ujenzi wa barabara katika mji wa mpakani wa Gatuna umefanya magari kuelekezwa katika mpaka wa Kagitumba,”

Waziri huyo alinukuliwa katika Twitter yake rasmi ya kazi akiongeza kuwa ujenzi huo utakamilika mwezi Mei mwaka..

Kuhusiana na uhusianao wamataifa hayo mawili alisema: “Uhusiano wetu kwa sasa sio mzuri vile lakini tunashughulikia hilo”

Bwana Sezibera aliongeza kuwa Rwanda inaendelea na majadiliano na majirani zake kuhusiana na masuala kadhaa ikiwa ni pamoja na kuzuiliwa kiharamu kwa raia wake nchini Uganda.

Image captionUjenzi wa barabara katika mpaka wa Gatuna upande wa Rwanda

Alisema kuwa suala la kuunga mkono makundi yaliyojihami yanayopinga Rwanda pia ni baadhi ya mambo yanayojadiliwa.

Wizari Sezibera pia amekanusha ripoti ya vyombo vya habari kuwa zinazodai kuwa taifa hilo limepeleka vikosi maalum vya kijeshi katika mpaka wake na Uganda tangu ilipochukua hatua ya kuifunga.

“Hakuna wanajeshi waliyopelekwa mpakani. Hakuna ubaya wowote ikiwa Rwanda imeamua kuimarisha usalama wa mpaka wake japo hilo halijafanyika.”, alisema.

”Nataka kuwahakikishia wanyarwanda kuwa wako salama!”

Huku hayo yakijiri Uganda imeishutumu Rwanda kwa kufunga mipaka baina ya nchi hizo mbili.

Alhamisi iliyopita mamlaka ya mapato ya Rwanda iliamrisha maroli ya mizigo kutotumia tena mpaka wa Gatuna kwa madai ya shughuli za ujenzi wa kituo kimoja cha mpakani ‘one stop border’ baina yake na Uganda.

Mkwamo wa shughuli katika mpaka wa Rwanda Uganda.

Eneo hilo lina umuhimu mkubwa kibiashara kieneo.

Ni eneo ambalo huruhusu kupita kwa bidhaa kutoka mji mkuu wa Uganda Kampala, au Mombasa pwani ya Kenya.

Wakaazi hapo wanasema ni kama ‘ghala kwa biashara kutoka maeneo hayo’.

Akizungumza na BBC, Diwani Abel Bizimana katika eneo la Kisoro anaeleza kwamba, ‘Hali haijabadilika. Tunaathirika kama viongozi wa kieneo, kama jumuiya ya wafanyabiashara na wateja pia tunaowahudumia.’

Abel ameeleza kuwa maisha yamebadilika pakubwa.

Kutokana na matatizo ya kibiashara na udhibiti wa watu kutoka na kuingia katika eneo hilo, watu ambao kawaida huja kupokea bidhaa kutoka mjini na wilaya ya Kisoro sasa inaarifiwa hawaji tena, wakiwemo hata waendesha boda boda ambao pia wamesitisha shughuli zao.

Maelfu wajitokeza kuomboleza kifo cha Ruge Mutahaba

Ruge MutahabaHaki miliki ya pichaCLOUDS MEDIA GROUP TANZANIA
Image captionMkurugenzi wa vipindi na uzalishaji Clouds Media Group Tanzania,Ruge Mutahaba

Maelfu ya raia wa Tanzania jijini Dar es Saalam, wanaendelea kuomboleza kifo cha Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji wa Clouds Media Group Tanzania, na mhamasishaji mkubwa wa vijana katika matumizi ya vipaji na fursa, Rugemalila Mutahaba maarufu kama Bosi Ruge.

Waziri mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa na baadhi ya viongozi wengine wa kitaifa akiwemo Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Tulia Akson wamefika nyumbani kwa Marehemu na kumuelezea wasifu wake. Mipango ya kurejesha mwili wa marehemu kutoka nchini Afrika kusini alikopelekwa kwa matibabu inafanyika

Huzuni

Msongamano wa waombolezaji ni mkubwa waliofika nyumbani kwa marehemu wakiwemo viongozi mbalimbali na watu maarufu. Waziri mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa anamuelezea Ruge kuwa Kielelezo cha tafsiri ya kiongozi kijana mwenye fikra na maono chanya kusaidia wengine na nchi kwa ujumla

“Vijana hasa katika eneo hili la sanaa, walikuwa na kiongozi ambaye alikuwa tayari kuwaongoza na kuwasaidia, nayasema haya kuonyesha namna ambavyo tulivyopoteza mwenzetu, lakini kubwa ndani ya serikali kuisaidia utafasiri ‘filosofia” ya uzalendo na fursa kwa watanzania.

Viongozi mbalimbali wa Tanzania wamejitokeza kwa wingi kwenye maombolezoHaki miliki ya pichaGLOBAL PUBLISHERS
Image captionWaziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa akiwa

Kwa vijana wengi kifo cha Ruge ni taa iliyozizima katikati yam situ mnene kwenye giza nene, wengi wao hawaoni kesho yao inafafanaje.

Rehema Jonas ni mmoja wa vijana waliofanikiwa kupitia programu za vijana katika kujenga uwezo wao , kujitambua na kuchukua hatua iitwayo ‘fursa’ amesema ”sisi ni vijana ambao tuko mtaani tunavipaji tu vya kuweza kufanya jambo Fulani, kwa hiyo mimi maisha yangu yote nimekuwa nikiishi kwa kauli ya Ruge. Tangu ameanza kuumwa nilianza kuona giza mbele, alikuwa ni zaidi ya Bosi, mshauri na rafiki”.

Buriani Ruge Mutahaba

Msanii maarufu na wa siku nyingi wa muziki wa kizazi kipya ambaye amelelewa na kukuzwa kimuziki na Ruge kupitia kituo chake cha sanaa cha Tanzania House of Talents (THT), Lameck Ditto anakiri kuwepo kwa hofu ya muelekeo wa muziki huo. ” Kwanza ni mshituko na hiyo hofu inakuja kwa sababu alikuwa mtu aliyekuwa anaweka mawazo yake yote katika kazi, lakini ametufundisha ni kuhakikisha tunajitahidi kwa kadiri tunavyoweza kukabiliana na changamoto tunazopitia”.

Kwa upande wake Joseph Kusaga, Mkurugenzi mwenza wa kampuni ya Clouds Media Group(CMG) inayomiliki vituo maarufu vya Televisheni na Radio vya Clouds, Joseph Kusaga, ametoa matumaini kwa vijana akisema kuwa vijana waliopita kwenye mikono yake watakuja kuendeleza yale mazuri aliyoyafanya.

Atiku Abubakar – mwanasiasa bilionea ambaye ni bingwa wa kutengeneza pesa

Atiku AbubakarHaki miliki ya pichaAFP

Kuna wagombea zaidi ya 70 ambao wanataka kumng’oa madarakani rais Muhammadu Buhari, lakini ni Atiku Abubakar pekee ambaye mwenye ubavu.

Abubakar ni mtu maarufu nchini Nigeria kwenye nyanja za kisiasa na biashara.

Amefikia moja ya cheo kikubwa kabisa cha utumishi, makamu wa raisi, na pia ni tajiri mkubwa aliyenufaika na sekta ya mafuta.

Ofisi kubwa zaidi ya nchi hiyo, urais, umekuwa ukimpiga chenga. Ameshajaribu mara tatu kabla na kuangukia pua.

Jumamosi Februari 16, kwa mara nyengine tena, mwanasiasa huyo mwenye miaka 72 anatupa karata yake, akiwaahidi wananchi kuwa uzoefu wake katika siasa na biashara ni dawa ya changamoto za nchi.

Hata hivyo wakosoaji wake wanamhusisha na kashfa za matumizi mabaya ya fedha, na kudai hilo tu linatosha kumfanya asipewe hatamu katika nchi ambayo rushwa ni tatizo kubwa.

Amekanusha vikali tuhuma hizo akidai zina mkono wa siasa ndani yake.

Endapo atachaguliwa, changamoto kuu mbele yake zitakuwa ongezeko kubwa la ukosefu wa ajira, umasikini wa kutupwa, bunge lililotawaliwa na matabaka ya kikanda, na uchumi unaoyumba kutokana na kutegemea pakubwa sekta ya mafuta.

Amekuwa akipiga kampeni ya kujitofautisha na rais wa sasa, Buhari, ambaye amekuwa akilalamikiwa kwa shidaa za kiuchumi.

Wanaompinga Buhari wanadai kuwa kaliba yake ya kubana matumizi, kutokubali mabadiliko kumekuwa ni kikwazo katika kuingoza na kuleta mabadiliko nchini Nigeria.

Wanasema kwa upande wapili, Abubakar, ni mtu rafiki na anayeshaurika na ana uwezo wa kuunganisha ulimwengu wa siasa na biashara, hali ambayo wafuasi wake wanadai inaweza kunyanyua uchumi na kuliunganisha taifa.

Oil facilities in Lagos harbourHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionUchumi wa Nigeria unategemea kwa kiwango kikubwa hifadhi zake za mafuta ambazo ni kubwa zaidi barani Afrika.

Mwanasiasa Nguli

Abubakar ni mgombea kupitia chama cha People’s Democratic Party (PDP), ambacho kimekuwa na ushawishi mkubwa kwa miongo miwili iliyopita. Alikuwa ni afisaa wa PDP pindi chama hicho kilipoundwa wakati wa ukomo wa utawala wa kijeshi. Kupitia chama hicho amehudumu kwa mihula miwili kama makamu wa raisi.

Lakini pia ametia wakati mgumu ndani ya chama hicho, akikikacha mara mbili na kwenda kuungana na makundi ya wapinzani.

Alihama mara ya kwanza mwaka 2006 wakati akichunguzwa mwenendo wake alipokuwa makamu wa rais akituhumiwa kuhamisha dola milioni 125 pesa ya umma kwenda kwenye biashara zake. Shutuma kama hizo zilitolewa kwenye ripoti ya bunge la seneti Marekani mwaka 2010 ambapo alishutumiwa kuhamisha “pesa za mashaka” dola milioni 40 kuingia Marekani akitumia akaunti ya mkewe raia wa Marekani.

Tuhuma zote hizo hazijawahi kuwasilishwa mahakamani na Abubakar amekuwa akidai kuwa kuna mkono wa kisiasa.

Mwezi Januari 2019, alitembelea Marekani kumaliza uvumi kuwa hakanyagi nchi hiyo kwa kuwa angekamatwa.

Presentational grey line
Atiku AbubakarHaki miliki ya pichaAFP
 • Amezaliwa 1946 katika jimbo la kaskazini la Adamawa
 • Mmiliki tanzu wa kampuni kubwa ya mafuta aliyofungua kwenye kontena
 • Aliongoza mipango ya ubinafsishji akiwa makamu wa rais
 • Amepambana na tuhuma za rushwa anazodai kuwa ni za kisiasa
 • Mwanzilishi wa Chuo Kikuu (American University) ambacho kimewasomesha bure baadhi ya mabinti waliotekwa na wanamgambo wa Boko Haram na kupona.
 • Baba yake, muislamu safi, alifungwa jela kwa muda kwa kujaribu kumzuia asisome shule za elimu ya kimagharibi.
 • Shabiki wa klabu ya Arsenal, ana wake wanne na watoto 28.
Presentational grey line

Kutengeneza Pesa

Tajriba ya Abubakar katika biashara inahusishwa na kukuwa kwa kampuni ya mafuta ya Intels ambayo yeye ni mmoja ya waaznilishi wake mwaka 1982. Kampuni hiyo ilianzia kwenye ofisi ya kontena na kukuwa kwa kiwango cha mabilioni ya naira, na kuajiri zaidi ya watu 10,000.

Pia ametoa wakfu na sadaka sehemu ya utajiri wake ikiwemo kuanzisha chuo maarufu cha American University katika jimbo lake la nyumbani la Adamawa. Chuo hicho hivi karibuni kimewasomesha bure baadhi ya mabinti waliotekwa na wanamgambo wa Boko Haram na kupona.

American University, Yola, Adamawa stateHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionAbubakar ni mwanzilishi wa Chuo Kikuu (American University) ambacho kimewasomesha bure baadhi ya mabinti waliotekwa na wanamgambo wa Boko Haram na kupona.

Abubakar anajitambulisha yeye kuwa ni mmoja wa wanuafaika wa elimu ya kimagharibi na anapingana vikali na kundi la Boko Haram. Amezaliwa kwenye familia ya Waislamu na baba yake ambaye alikuwa mfanyabiashara na mfugaji kutoka kabila la Fulani alifungwa jela kwa muda kwa kujaribu kumzuia asisome shule za elimu ya kimagharibi.

“Baba alikuwa ana hofu ya mabadiliko ambayo yalikuwa yakiikabili Nigeria katika kipindi hicho,” ameandika Buhari katika kitabu chake.

Baada ya kumaliza masomo yake, alijiunga na idara ya forodha katika bandari ya Lagos, japo rushwa ilikuwa kubwalakini anasema yeye hakujihusisha nayo hata kidogo.

Akiwa serikalini alianza kunua ardhi na nyumba kwa ajili ya biashara na mwishowe kuingia katika biashara ya mafuta.

“Niligundua mapema kabisa kuwa nina upeo mzuri wa biashara,” anaandika kwenye kitabu chake kiitwa ‘Making Money’ ama kutengeneza pesa.

Posters for Atiku AbubakarHaki miliki ya pichaAFP

Utaifishaji

Mwaka 1989 Abubakar alijiuzulu katika utumishi wa umma na kujikita kwenye siasa. Aligombea urais kwa mara ya kwanza mwaka 1991 na kujitoa kwenye kinyang’anyiro baada ya kuwa mshindi wa tatu kwenye mzunguko wa kwanza. Hata hivyo uchaguzi huo baadae ulifutwa na jeshi.

Ukandamizwaji ulizidi miaka ya 90 chini ya dikteta Jenerali Sani Abacha. Abubakar akakimbilia kizuizini London.

Alirejea Nigeria mwaka 1997 baada ya Abacha kupunguza makali yake, na kuwa makamu wa rais mwaka 1999 baada ya kumpigia chapuo Olusegun Obasanjo, katika kiti cha urais.

Muhammadu Buhari (L) and Atiku Abubakar (R)Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionAbubakar (kulia) kwa muda mfupi alihamia chama cha APC na kuungana na Buhari.

Akiwa madarakani kama mtu wa pili mwenye mamlaka zaidi aliongoza juhudi za ubinafsishaji, na kujipatia sifa kama mwanamageuzi kwa upande mmoja lakini akikashifiwa kama bepari kwa upande wa pili.

Katika kitabu chake, amejivuni kuwezesha mabadiliko kwenye sekta ya benki, simu za mkononi pamoja na kukua kwa uchumi kulikoiwezesha Nigeria kulipa madeni yake mengi.

Abubakar anasema atazirejesha siku za furaha akipata madaraka mwaka huu. Lakini uwezo wake wa kufanya hivyo utategemeana na nguvu zilizopo nje ya uwezo wake.

“Ni ngumu kutabiri atafanikiwa katika lipi,” anasema mhariri wa BBC wa , Aliyu Tanko, ” kwa uchumi ambao unategemea pakubwa bei ya mafuta.”

Abubakar ana wake wanne na watoto 28.