Atiku Abubakar – mwanasiasa bilionea ambaye ni bingwa wa kutengeneza pesa

Atiku AbubakarHaki miliki ya pichaAFP

Kuna wagombea zaidi ya 70 ambao wanataka kumng’oa madarakani rais Muhammadu Buhari, lakini ni Atiku Abubakar pekee ambaye mwenye ubavu.

Abubakar ni mtu maarufu nchini Nigeria kwenye nyanja za kisiasa na biashara.

Amefikia moja ya cheo kikubwa kabisa cha utumishi, makamu wa raisi, na pia ni tajiri mkubwa aliyenufaika na sekta ya mafuta.

Ofisi kubwa zaidi ya nchi hiyo, urais, umekuwa ukimpiga chenga. Ameshajaribu mara tatu kabla na kuangukia pua.

Jumamosi Februari 16, kwa mara nyengine tena, mwanasiasa huyo mwenye miaka 72 anatupa karata yake, akiwaahidi wananchi kuwa uzoefu wake katika siasa na biashara ni dawa ya changamoto za nchi.

Hata hivyo wakosoaji wake wanamhusisha na kashfa za matumizi mabaya ya fedha, na kudai hilo tu linatosha kumfanya asipewe hatamu katika nchi ambayo rushwa ni tatizo kubwa.

Amekanusha vikali tuhuma hizo akidai zina mkono wa siasa ndani yake.

Endapo atachaguliwa, changamoto kuu mbele yake zitakuwa ongezeko kubwa la ukosefu wa ajira, umasikini wa kutupwa, bunge lililotawaliwa na matabaka ya kikanda, na uchumi unaoyumba kutokana na kutegemea pakubwa sekta ya mafuta.

Amekuwa akipiga kampeni ya kujitofautisha na rais wa sasa, Buhari, ambaye amekuwa akilalamikiwa kwa shidaa za kiuchumi.

Wanaompinga Buhari wanadai kuwa kaliba yake ya kubana matumizi, kutokubali mabadiliko kumekuwa ni kikwazo katika kuingoza na kuleta mabadiliko nchini Nigeria.

Wanasema kwa upande wapili, Abubakar, ni mtu rafiki na anayeshaurika na ana uwezo wa kuunganisha ulimwengu wa siasa na biashara, hali ambayo wafuasi wake wanadai inaweza kunyanyua uchumi na kuliunganisha taifa.

Oil facilities in Lagos harbourHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionUchumi wa Nigeria unategemea kwa kiwango kikubwa hifadhi zake za mafuta ambazo ni kubwa zaidi barani Afrika.

Mwanasiasa Nguli

Abubakar ni mgombea kupitia chama cha People’s Democratic Party (PDP), ambacho kimekuwa na ushawishi mkubwa kwa miongo miwili iliyopita. Alikuwa ni afisaa wa PDP pindi chama hicho kilipoundwa wakati wa ukomo wa utawala wa kijeshi. Kupitia chama hicho amehudumu kwa mihula miwili kama makamu wa raisi.

Lakini pia ametia wakati mgumu ndani ya chama hicho, akikikacha mara mbili na kwenda kuungana na makundi ya wapinzani.

Alihama mara ya kwanza mwaka 2006 wakati akichunguzwa mwenendo wake alipokuwa makamu wa rais akituhumiwa kuhamisha dola milioni 125 pesa ya umma kwenda kwenye biashara zake. Shutuma kama hizo zilitolewa kwenye ripoti ya bunge la seneti Marekani mwaka 2010 ambapo alishutumiwa kuhamisha “pesa za mashaka” dola milioni 40 kuingia Marekani akitumia akaunti ya mkewe raia wa Marekani.

Tuhuma zote hizo hazijawahi kuwasilishwa mahakamani na Abubakar amekuwa akidai kuwa kuna mkono wa kisiasa.

Mwezi Januari 2019, alitembelea Marekani kumaliza uvumi kuwa hakanyagi nchi hiyo kwa kuwa angekamatwa.

Presentational grey line
Atiku AbubakarHaki miliki ya pichaAFP
  • Amezaliwa 1946 katika jimbo la kaskazini la Adamawa
  • Mmiliki tanzu wa kampuni kubwa ya mafuta aliyofungua kwenye kontena
  • Aliongoza mipango ya ubinafsishji akiwa makamu wa rais
  • Amepambana na tuhuma za rushwa anazodai kuwa ni za kisiasa
  • Mwanzilishi wa Chuo Kikuu (American University) ambacho kimewasomesha bure baadhi ya mabinti waliotekwa na wanamgambo wa Boko Haram na kupona.
  • Baba yake, muislamu safi, alifungwa jela kwa muda kwa kujaribu kumzuia asisome shule za elimu ya kimagharibi.
  • Shabiki wa klabu ya Arsenal, ana wake wanne na watoto 28.
Presentational grey line

Kutengeneza Pesa

Tajriba ya Abubakar katika biashara inahusishwa na kukuwa kwa kampuni ya mafuta ya Intels ambayo yeye ni mmoja ya waaznilishi wake mwaka 1982. Kampuni hiyo ilianzia kwenye ofisi ya kontena na kukuwa kwa kiwango cha mabilioni ya naira, na kuajiri zaidi ya watu 10,000.

Pia ametoa wakfu na sadaka sehemu ya utajiri wake ikiwemo kuanzisha chuo maarufu cha American University katika jimbo lake la nyumbani la Adamawa. Chuo hicho hivi karibuni kimewasomesha bure baadhi ya mabinti waliotekwa na wanamgambo wa Boko Haram na kupona.

American University, Yola, Adamawa stateHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionAbubakar ni mwanzilishi wa Chuo Kikuu (American University) ambacho kimewasomesha bure baadhi ya mabinti waliotekwa na wanamgambo wa Boko Haram na kupona.

Abubakar anajitambulisha yeye kuwa ni mmoja wa wanuafaika wa elimu ya kimagharibi na anapingana vikali na kundi la Boko Haram. Amezaliwa kwenye familia ya Waislamu na baba yake ambaye alikuwa mfanyabiashara na mfugaji kutoka kabila la Fulani alifungwa jela kwa muda kwa kujaribu kumzuia asisome shule za elimu ya kimagharibi.

“Baba alikuwa ana hofu ya mabadiliko ambayo yalikuwa yakiikabili Nigeria katika kipindi hicho,” ameandika Buhari katika kitabu chake.

Baada ya kumaliza masomo yake, alijiunga na idara ya forodha katika bandari ya Lagos, japo rushwa ilikuwa kubwalakini anasema yeye hakujihusisha nayo hata kidogo.

Akiwa serikalini alianza kunua ardhi na nyumba kwa ajili ya biashara na mwishowe kuingia katika biashara ya mafuta.

“Niligundua mapema kabisa kuwa nina upeo mzuri wa biashara,” anaandika kwenye kitabu chake kiitwa ‘Making Money’ ama kutengeneza pesa.

Posters for Atiku AbubakarHaki miliki ya pichaAFP

Utaifishaji

Mwaka 1989 Abubakar alijiuzulu katika utumishi wa umma na kujikita kwenye siasa. Aligombea urais kwa mara ya kwanza mwaka 1991 na kujitoa kwenye kinyang’anyiro baada ya kuwa mshindi wa tatu kwenye mzunguko wa kwanza. Hata hivyo uchaguzi huo baadae ulifutwa na jeshi.

Ukandamizwaji ulizidi miaka ya 90 chini ya dikteta Jenerali Sani Abacha. Abubakar akakimbilia kizuizini London.

Alirejea Nigeria mwaka 1997 baada ya Abacha kupunguza makali yake, na kuwa makamu wa rais mwaka 1999 baada ya kumpigia chapuo Olusegun Obasanjo, katika kiti cha urais.

Muhammadu Buhari (L) and Atiku Abubakar (R)Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionAbubakar (kulia) kwa muda mfupi alihamia chama cha APC na kuungana na Buhari.

Akiwa madarakani kama mtu wa pili mwenye mamlaka zaidi aliongoza juhudi za ubinafsishaji, na kujipatia sifa kama mwanamageuzi kwa upande mmoja lakini akikashifiwa kama bepari kwa upande wa pili.

Katika kitabu chake, amejivuni kuwezesha mabadiliko kwenye sekta ya benki, simu za mkononi pamoja na kukua kwa uchumi kulikoiwezesha Nigeria kulipa madeni yake mengi.

Abubakar anasema atazirejesha siku za furaha akipata madaraka mwaka huu. Lakini uwezo wake wa kufanya hivyo utategemeana na nguvu zilizopo nje ya uwezo wake.

“Ni ngumu kutabiri atafanikiwa katika lipi,” anasema mhariri wa BBC wa , Aliyu Tanko, ” kwa uchumi ambao unategemea pakubwa bei ya mafuta.”

Abubakar ana wake wanne na watoto 28.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *