Afukuzwa kazi kisa ujauzito

A working motherHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

”Nilifukuzwa kazi miezi minne baada ya kupewa likizo ya uzazi.”

“Nilikuwa tegemeo la familia yangu, sikua na muongozo wa sheria kwa hiyo nilishauriwa kutia saini ‘mkataba wa lazima’, Nilijihisi mnyonge sana.”

Haya ni maneno ya mama aliyezungumza na BBC baada ya kuchapisha makala kuhusu haki wa wanawake wajawazito kazini.

Kisa chake – na visa vya wengine wengi- vinaashiria ubaguzi unaoendelea kuwakabili wanawake wanaofanya kazi katika makampuni makubwa ya Ungereza ambapo viongozi wa ngazi ya juu wanakiuka sheria na kuwanyanyasa wanawake wanaopata ujauzito wakiwa kazini.

Lakini waathiriwa wanahofia sana kuzungumza kwasababu wamelazimishwa kutia saini mkataba wa kutozungumzia masaibu yanayowakabili.

Katika visa vingine masharti hayo yanawatishia kutozungumzia hali zao kwa ”pamoja”

Stressed mumHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Wakati mgumu

“Masharti hayo yanaziwezesha makampuni kuvunja sheria,” alisema mama aliyewasiliana na BBC.

“Unahitaji kuwa mjasiri na mvumilivu sana kushinda kesi mahakamani.”

“Nilikuwa na mtoto mchanga na wakati huo pia nilikuwa na hofu kuhusu jinsi nitakavyolipa deni la nyumba kwa hivyo sikuweza kupambana na kesi.

Karibu miaka tano sasa, baada ya kufutwa kazi katika mazingira ya kutatanisha anasema: “Tafadhali usichapishe jina langu, nataka kuangazia kisa changu tu. Nataka sheria ifanyiwe mabadiliko. Hii iliyopo haiwapatii ulinzi wanawake hata kidogo.”

Sheria iko wazi: ni kinyume cha sheria kufuta mtu kazi kwasababu ni mjamzito au yuko likizo ya uzazi.

Mama na mtotoHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Lakini wanawake wanaendelea kunyanyaswa. Ni hivi majuzi tu waziri wa biashara Kelly Tolhurst, alisema: “Ubaguzi dhidi ya wanawake wajawazito na wale waliyo likizo ya uzazi ni ukikaji wa sheria, lakini baadhi ya kina mama wapya wanashindwa kuendelea na kazi hata wakirudi kutokana na mazingira magumu ya kazi ambayo inawalazimu kuondoka.”

Mwanamke mwingine aliyewasiliana na BBC alijifungua miezi michache iliyopita na yeye pia hakutaka jina lake litajwe.

Masaibu yake yalianza pale bosi wekea alipomuita kujadali masuala ya kazi na mipango yake ya baadae.

“Nilipomwambia kuwa niko mjamzito alibadilika ghafla na kutoka wakati huo mtazamo wake kwangu ulibadilika kabisa, hilo lilinishangaza sana.” alisema.

Aliporejea kazini kutoka likizo ya uzazi mwaka uliyopita alitoa maombi ya kutaka kubadilishiwa nyakati za kazi ili aweze kumhudumia mtoto wake lakini ombi lake lilikataliwa.

“Hawakujua kwamba ningelichukua hatua zaidi. kwa kuwa najua haki yangu nilikata rufaa dhidi ya uamuzi huo.

“Kampuni iliamua kunilipa fidia na wakili wangu alinishauri nikubali ofa yao, lakini kufikia hilo nilitakiwa kutia saini mkataba wa kutozungumzia suala hilo.”

Kwa sasa mama huyo anajihisi vibaya sana. “Nilihisi kuwa hakuna aliyenijali wala kuelewa hali yangu.

“Cha kusikitisha zaidi ni kuwa ombi la mume wangu kubadilishiwa nyakati za kazi ili aweze kumhudumia mtoto pia lilikataliwa na muajiri wake. Hatua hiyo ilimaanisha sote tufanye uamuzi kwa kuzingatia haki yetu katika katiba.”

UjauzitoHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Anapendekeza serikali iongeze juhudi za kuhamasisha watu kuhusu haki zao na kuwahimiza wapaze sauti wanaponyanyaswa kazini.

Mwanaharakati Joeli Brearley, mwanzilishi wa shirika moja la kijamii ambalo linapigania haki za wanawake wanaobaguliwa kazini nchini Uingereza, anasema: “Mkataba wa kumzuia mtu kutozungumzia hali inayomkabili mara nyingi hutumiwa kumteka nyara mfanyikazi. Waajiri hutumia mkataba huo kama kikombozi cha kuwamanyamazisha wafanyikazi wao.”

Bi. Brearley anapendekeza yaliyomo kwenye mkataba huo kufuatiliwa kwa makini.

“Huwezi kufutilia mbali mkataba wa aina hiyo katika visa vingine kwasababu inamlinda mfanyikazi. Muajiri anazuliwa kisheria kumzungumzia vibaya muathiriwa kwa muajiri mtarajiwa na bila mkataba kama huo mfanyikazi huyo hatakuwa na ushahidi wa kujitetea mahakamani.”

Hata hivyo Bi. Brearley anaamini kufuatilia mkataba huo kutasaidia kukomesha “visa vya waajiri kuitumia vibaya kwa manufaa yao”.

Kile anachosisitiza ni kuhakikisha mkataba wa kumzuia mtu kuzungumzia hadharani suala fulani unawasilishwa kwa bodi maalum itakayopewa jukumu la kuchunguza yaliyomo ndani ya mkataba huo na kuchukua hatua endapo italazimika kufanya hivyo .

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *