Zuma amtaja Castro kuwa mtetezi wa masikini

castro

Viongozi wa nchi za Amerika ya Kusini na maelfu ya raia wa Cuba wamehudhuria ibada ya mazishi ya aliyekuwa Rais wa Cuba Fidel Castro aliyefariki dunia siku ya Ijumaa iliyopita akiwa na umri wa miaka 90. Marais wa Mexico, Ecuador, Bolivia, Venezuela, Afrika Kusini na Zimbabwe pamoja na viongozi wa nchi za Carribean wako katika ukumbi wa mapinduzi mjini Havana kuhudhuria ibada hiyo.Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma ameisifu Cuba akisema chini ya utawala wa Fidel Castro, nchi hiyo ilipiga hatua kubwa katika sekta ya elimu na afya na kuzisaidia nchi za Afrika katika mapambano yao ya kunyakua uhuru kutoka kwa Wakoloni na kuongeza Castro atakumbukwa kwa imani yake kwamba watu masikini wana haki ya kuishi maisha ya hadhi. Majivu ya mwili wake ulioteketezwa yatazikwa Jumapili mjini Santiago.

#DW

Comments

comments

Random Posts