Zawadi za sibuka lotto zawafikia wakazi wa mbeya na songwe.

1.Mbeya

Mwakilishi wa Sibuka Media Ulimboka Mwakilili akizungumza na Washindi wa Sibuka Lotto kutoka Mkoa wa Songwe kabla ya kuwakabidhi zawadi walizojishindia katika hafla iliyofanyika Mji mdogo wa Mlowo Wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe.

2.mbeya

Mwakilishi wa Sibuka Media Ulimboka Mwakilili akizungumza na Washindi wa Sibuka Lotto kutoka Mkoa wa Mbeya kabla ya kuwakabidhi zawadi walizojishindia katika hafla iliyofanyika Igawa Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya

3.mbeya

Katibu Mkuu Chama cha Waandishi wa Habari za Utalii na Uwekezaji Tanzania(TAJATI) (katikati), Venance Matinya akimkabidhi Baiskeli msindi wa Sibuka Lotto, Eward Kiswaga  kutoka Mji mdogo wa Rujewa Wilaya ya Mbarali mkoani Mbarali

4.mbeya

Katibu Mkuu Chama cha Waandishi wa Habari za Utalii na Uwekezaji Tanzania(TAJATI), Venance Matinya akimkabidhi Mpira msindi wa Sibuka Lotto Hemed Komba kutoka Igawa  Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya.

5.mbeya

Katibu Mkuu Chama cha Waandishi wa Habari za Utalii na Uwekezaji Tanzania(TAJATI), Venance Matinya akimkabidhi Redio kubwa  msindi wa Sibuka Lotto, Mussa Mboto kutoka Tunduma  mkoani Songwe.

6.mbeya

Katibu Mkuu Chama cha Waandishi wa Habari za Utalii na Uwekezaji Tanzania(TAJATI), Venance Matinya akimkabidhi Redio kubwa  msindi wa Sibuka Lotto, Job Kabinji kutoka Vwawa  mkoani Songwe

7.mbeya

Daniel Mwanisenga mshindi wa Baiskeli kutoka Sibuka Lotto akijaribi kupanda baiskeli yake baada ya kukabihiwa

8.mbeya

Baadhi ya zawadi za Washindi wa Sibuka Lotto.

9.mbeya

WAKAZI 6 kutoka Mikoa ya Songwe na Mbeya wamenufaika na kufikiwa na zawadi walizoshinda katika shindano la Bahati nasibu linaloendeshwa na SIBUKA MEDIA linalojulikana kwa jina la SIBUKA LOTTO lenye kauli mbiu Selema kwa Elfu.

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi zawadi kwa Washindi Mwakilishi wa Sibuka Media Mkoa wa Mbeya, Ulimboka Mwakilili alisema mchezo wa Sibuka Lotto ulianza rasmi Septemba 21, mwaka huu na unatarajia kufikia tamati Disemba 9 mwaka huu kwa kuchezeshwa droo kubwa.

Alisema zawadi zinazoshindaniwa ni pamoja na Trekta kubwa aina ya John Deere, Majembe ya kukokotwa na Ng’ombe (Plau),Baiskeli, Pampu za kupulizia dawa shambani na mipira ya miguu yenye viwango vya Kimataifa inayotambuliwa na Shirikisho la Soka Duniani (FIFA).

Aliongeza kuwa Droo ndogo huchezeshwa kila wiki siku ya Jumamosi ambapo washindi 16 hupatikana Nchi nzima na kupewa zawadi za Bodaboda, Baiskeli, Redio Seti 5 na Mipira ya miguu 5.

Alisema katika Droo ya mwisho zawadi zitakazoshindaniwa ni pamoja na Trekta kubwa 1, Bodaboda 50, Pampu 50,Redio 50, Baiskeli 50 na Mipira ya Miguu 50.

Aliwataja Washindi wa Droo hiyo kwa Mkoa wa Mbeya kuwa ni Hemed Komba kutoka Mbarali aliyepata Mpira na Eward Kiswaga mkazi wa Rujewa Wilaya ya Mbarali aliyejinyakulia Baiskeli aina ya Phoenix.

Kwa upande wa Mkoa wa Songwe aliwataja Washindi kuwa ni Zakayo Mwasomola mkazi wa Kamsamba aliyepata Mpira mmoja, Mussa Mboto mkazi wa Tunduma na Job Kabinji Mkazi wa Vwawa wote wakiwa wamejishindia Redio kubwa aina ya Sub Woofer  pamoja na Daniel Mwanisenga mkazi wa Kamsamba aliyepata Baiskeli aina ya Phoenix.

Kwa upande wake Washindi hao ambao zawadi hizo walikabidhiwa na Katibu Mkuu wa Chama cha Waandishi wa Habari za Utalii na Uwekezaji Tanzania (TAJATI) Venance Matinya, waliupongeza uingozi wa Sibuka Media kwa kuendesha droo hiyo na kukabidhiwa Zawadi pasipo kificho.

Walisema Mchezo wa Sibuka upo wazi tofauti na makampuni mengine ambayo yakiandaa mashindano zawadi kwa washindi hazijulikani na hutolewa kwa kificho jambo linaloashiria kutokuwa na ushawishi wa kucheza.

  • #SIBUKAMEDIA
  • #SIBUKALOTTO
  • MBEYA

#

Comments

comments