Zaidi ya vijana 205 Mjini DODOMA wamekutana katika kongamano la kutoa maoni na Maboresho ya Sera ya Maendeleo ya Vijana

Dodoma

Zaidi ya vijana 205 Mjini DODOMA wamekutana katika kongamano la kutoa maoni na Maboresho ya Sera ya Maendeleo ya Vijana itakayotoa fursa ya vijana kushiriki kikamilifu shughuli za maendeleo.

Akifungua Kongamano la Kutoa Maoni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayesimamia Kazi, Ajira,Vijana na Watu Wenye Ulemavu ERIC SHITINDI amewataka vijana kujadili kwa mapana athari chanya na hasi za matumizi ya Teknolojia katika mitandao kwa vijana.

Mkurugenzi wa idara ya kazi ofisi ya waziri mkuu JAMES KAJUGUSI amesema kutokana na mabadiliko ya kiuchumi,kisiasa,kiteknolojia ,serikali imeamua kukusanya maoni ya wadau mbalimbali yatakayowezesha kupata sera itakayojibu changamoto za vijana.

Naye Katibu mkuu ofisi ya waziri mkuu anayesimamia kazi,ajira,vijana na watu wenye ulemavu ERIC SHITINDI amewataka washiriki wa kongamano na watoa mada kuhakikisha wanajadili kwa mapana suala la malezi kwa vijana likiwemo la matumizi ya teknolojia ambayo kwa sasa imekuwa na matumizi mengi yakiwemo ya kuhalifu.

Baadhi ya vijana wajasiriamali,wamesema  kwa muda mrefu vijana wamekuwa wakijaribu kupata mwelekeo wa mafanikio bila kupata miongozo ya kuelekea mafanikio jambo ambalo limekuwa likisababisha vijana wengi kujiingiza katika vishawishi na kupoteza dira ya maisha.

  • #SIBUKAMEDIA

Comments

comments