Yanga waendeleza vipigo kwa kuiadhibu Mbeya City

Ligi Kuu soka Tanzania bara imeendelea Jumanne katika uwanja wa Sokoine, kwa wenyeji Mbeya City kuwakaribisha Mabingwa wa Ligi Kuu Yanga.Yanga ambao msimu huu wa Ligi Kuu wamefungwa mechi moja na Coastal Union katika uwanja wa Mkwakwani Tanga, wameibuka na ushindi wa goli 2-0, magoli ambayo yamefungwa na beki wao wa kimataifa wa Togo anayeichezea klabu hiyo Vicent Bossou dakika ya 15 na Amissi Tambwe akapachika goli la pili dakika ya 84.

Kabla ya mchezo Yanga ambao walitangazwa Mabingwa baada ya Azam FC kupokonywa point tatu, walikuwa wanataka kushinda mchezo huu ili kuweka heshima ya kutwaa Ubingwa pasipo kutegemea point za mezani.

Comments

comments