WIZARA YA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA IMEWASILISHA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA MWAKA 2017/2018.

 

TANZANIA

WIZARA YA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA IMEWASILISHA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA MWAKA 2017/2018 HUKU IKISISITIZA KUWA HALI YA  ULINZI NA USALAMA WA MIPAKA YA NCHI KWA UJUMLA NI SHWARI LICHA YA KUWEPO KWA CHANGAMOTO KATIKA BAADHI YA NCHI ZA UKANDA WA AFRIKA MASHARIKI MAZIWA MAKUU NA PEMBE YA AFRIKA.

AKIWASILISHA BAJETI HIYO  LEO BUNGENI MJINI DODOMA WAZIRI WA WIZARA HIYO DK HUSSEIN MWINYI AMETAJA MAENEO HAYO KUWA NI PAMOJA NA JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA KONGO, BURUNDI, SOMALIA NA SUDAN KUSINI AMBAPO PIA AMESEMA MPANGO WA MWELEKEO WA BAJETI WA WIZARA HIYO KWA MWAKA WA FEDHA 2017/18 UNAKUSUDIA KUIMARISHA UTENDAJI KAZI NA KUONGEZA UFANISI WA JESHI KATIKA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAKE KULINGANA NA DIRA NA DHIMA YA WIZARA

AKIZUNGUMZIA VITENDO VYA UHALIFU DOKTA MWINYI AMESEMA KATIKA KUKABILIANA NA VITENDO HIVYO WIZARA KUPITIA JESHI LA WANANCHI LA TANZANIA(JWTZ) IMEENDELEA KUSHIRIKIANA NA VYOMBO VINGINE VYA USALAMA NA MATAIFA MENGINE KATIKA KUPAMBANA NA MATISHIO YA KIUSALAMA YAKIWEMO UGAIDI, UHARAMIA NA BIASHARA HARAMU YA DAWA ZA KULEVYA.

KWA UPANDE WAKE MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MAMBO YA NJE, ULINZI NA USALAMA ADADI RAJABU AMEISHAURI SERIKALI KULIPATIA FEDHA ZA MAENDELEO ZILIZOIDHINISHWA NA BUNGE FUNGU 38 NGOME AMBALO LINAHUSIKA NA MAMBO YA MSINGI KWA UWEPO WA NCHI NA KWA KUWA KASMA ZA MATUMIZI MUHIMU ZIPO KATIKA FUNGU HILO.

WIZARA HIYO IMEOMBA KIASI CHA SHILINGI  TRILIONI 1.725 KWA AJILI YA MATUMIZI YA KAWAIDA NA MATUMIZI YA MAENDELEO ILI IWEZE KUTEKELEZA MAJUKUMU YAKE.

  • Mwandishi : Barnaba Kisengi
  • #SIBUKAMEDIA

Comments

comments