Wito umetolewa kwa vijana nchini kujihusisha na elimu ya afya ya uzazi kwa kuwa wengi wao wamekuwa wakikabiliana na changamoto mbalimbali kutokana na ukosefu wa afya ya uzazi.

Afya ya uzazi

Wito umetolewa  kwa vijana nchini kujihusisha na elimu ya afya ya uzazi kwa kuwa wengi  wao wamekuwa wakikabiliana na changamoto mbalimbali kutokana na ukosefu wa afya ya uzazi.

Akitoa wito huo jijini Dar es salaam katika warsha iliyoandaliwa na shirika la umoja wa mataifa linaloshughulikia idadi ya watu (UNFPA)  meneja mradi wa AMUA BW. ADAM MBYALU amesema ukosefu wa elimu ya uzazi husababisha mimba za utotoni na maambukizi ya VVU.

Nae afisa uhusiano na mawasiliano wa UNFPA BW. BRIGHT WARREN amesema changamoto inayowapata watoto wa kike ni kubwa na inasababisha kushindwa kutimiza malengo waliyojiwekea.

WARREN amesema ipo haja ya vijana kupewa elimu ya afya mara kwa mara ili kupunguza vifo vya uzazi,mimba za utotoni na kupunguza ongezeko la watoto wa mitaani.

Nae Bi. IDDA SAERA kutoka Maisha package amesema wa watoto wa kike wanakuwa na wakati mgumu wakati wa siku za hedhi hivyo kwa kuwajali wametengeneza taulo za kike zitakazowasaidia kujisitiri kwa gharama nafuu hasa wakati wa masomo.

  • #SIBUKAMEDIA

Comments

comments