Wema Isaack Sepetu anatuhumiwa kujihusisha na dawa za kulevya

Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu imehairisha kesi inayomkabili mrembo wa TANZANIA BI. WEMA ISAACK SEPETU anayetuhumiwa kujihusisha na dawa za kulevya baada ya kukutwa na bangi nyumbani kwake.

Kwa mujibu wa wakili wa serikali ONOLINA MOSHI upelelezi wa kesi hiyo umekamilika kinachosubiriwa ni tarehe ya kuanza kusikilizwa.

WEMA na mfanyakazi wake wa ndani wamepanda kizimbani leo jijini Dar es salaam mbele ya hakimu Thomas Simbu katika mahakama ya kisutu ambapo kesi hiyo ilihairishwa hadi tarehe moja juni mwaka 2017.

WEMA na mfanyakazi wake wa ndani wanatuhumiwa kuhusika na biashara ya dawa za kulevya baada ya kukutwa na bangi nyumbani kwake.

Mwandishi : Tuse Kasambala

#SIBUKAMEDIA

Comments

comments