Waziri WILLIAM LUKUVI ameliagiza Jeshi la Polisi mkoani Dodoma kuwakamata baadhi ya Maafisa Ardhi .

Lukuvi

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi WILLIAM LUKUVI ameliagiza Jeshi la Polisi mkoani Dodoma kuwakamata baadhi ya Maafisa Ardhi na Wanasheria ambao wamehusika katika uuzaji wa shamba la kiasi cha hekta mbili na nusu mali ya MADINA OMARY mkazi wa bagamoyo mkoani pwani.

LUKUVI ametoa kauli hiyo ofisini kwake mjini Dodoma mbele ya waandishi wa habari wakati akimrejeshea mama huyo ardhi yake, huku akitaka maafisa ardhi na wanasheria kufuata taratibu zote za uuzaji ardhi wakati wa kuuza ardhi.

Waziri LUKUVI amekabidhi hati ya umiliki wa ardhi kiasi cha hekta mbili na nusu Mama MADINA OMARY ambaye alidhurumiwa ardhi yake iliyoko katika eneo la MSALATO nje kidogo ya mji wa Dodoma baada ya hati yake kuibiwa nyumbani kwake.

Akikabidhi hati hiyo Waziri LUKUVI amewaonya wanasheria wenye tabia kama  hiyo hiyo kuacha mara moja na juahidi kwamba watake bainika hatua kali za kishria zitachukuliawa dhidi yao.

  • #SIBUKAMEDIA

Comments

comments