Waziri wa viwanda na biashara Mh. Charles Mwijage amefungua engo la kampuni ya Taifa ya vifaa vya ujenzi la China National Building Material Group Limited.

wachina uzinduzi.Still003

Waziri wa viwanda na biashara Mh. Charles Mwijage mapema leo amefungua rasmi jengo la kampuni ya Taifa ya vifaa vya ujenzi la China National Building Material Group Limited (CNBM) lililopo mikocheni jijini Dar es salaam.

Akizungumza mgeni rasmi katika ufunguzi huo wa kampuni hiyo Mh.Mwijage amesema kuwa kampuni hiyo ni ya kimataifa na yenye viwango ambayo imejenga zaidi ya asilimia 65 ya viwanda vyote vya saruji na vioo  duniani.

Waziri Mwijage amesema kuwa kampuni ya CNBM ina uwezo mkubwa katika uzalishaji wa cement  na imekuwa ikizalisha tani 530 milioni kwa mwaka wakati uwezo wa Tanzania katika viwanda vilivyosimikwa ni tani milioni 10.8 na kubainisha kuwa kiasi kinachohitajika nchini ni tani milioni 4.8.

wachina uzinduzi.Still001
President XI YOUQING

Ameongeza kuwa CNBM inatarajiwa kushirikiana na mwekezaji mwingine ambaye anakwenda kujenga kiwanda Tanga kitakachozalisha  tani milioni saba za cement na kubainisha kuwa hakuna kiwanda kinachozalisha tani milioni saba Tanzania.

Aidha CNBM  kwa kutambua umuhimu wa uwekezaji na uzalishaji wa vifaa vya ujenzi hapa wamekuwa wakitoa maelekezo kwa wataalam nchini  badala ya kununua vifaa hivyo nje ya nchi.

Amebainisha viwanda bora vya nyaya barani Afrika kuwa ni vitatu kimoja kikiwa Nigeria,Afrika kusini na cha tatu kinajengwa Mwenge Tanzania chenye uwezo wa kuzalisha kilomita 100 za nyaya kwa masaa nane.

wachina uzinduzi.Still002

Nae Balozi wa China nchini Tanzania Bw. Lv Youqing amesema kuwa urafiki baina ya  Chinana Tanzania ni wa kihistoria tangu kwa Rais Xi Jinping ambapo urafiki huo umekuwa  mwendelezo hadi kwa serikali ya  awamu ya tano ya Rais John Magufuli.

wachina uzinduzi.Still004

Aidha Mkurugenzi wa China National Building Material Group Limited  (CNMB)  Bw. Andy Chen amesema kampuni hiyo inatoa fursa ya kazi kwa watanzania pamoja na kutoa mafunzo yatakayowasaidia kuendana na sera ya Tanzania ya viwanda.

  • Mwandishi : Tuse Kasambala
  • #SIBUKAMEDIA

Comments

comments

Random Posts