WAZIRI wa Viwanda na Biashara, ameipongeza kampuni ya CNBM kutoka CHINA iliyojenga kiwanda cha vifaa vya ujenzi.

 

WAZIRI wa Viwanda na Biashara,  DKT.CHARLES MWIJANGE, ameipongeza kampuni ya CNBM  kutoka CHINA iliyojenga kiwanda cha vifaa vya ujenzi.

Akizungumza wakati wa kuweka jiwe la msingi la kiwanda hicho kilichopo TABATA-MATUMBI jijini DAR ES SALAAM,Waziri amesema kiwanda hicho kitakuwa kinasambaza vifaa vya ujenzi hapa nchini.

Amesema TANZANIA na CHINA zimekuwa na ushirikiano wa muda mrefu hivyo Tanzania itaendelea kuwaunga mkono wawekezaji wenye nia njema kwa serikali hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchumi wa viwanda.

Aidha waziri ameongeza kuwa kituo hicho kitawasaidia Watanzania kujipatia ajira na kuongeza ufanisi kwa vijana nchini kwa kunufaika na kituo hicho.

Kwa upande wake Balozi mpya wa CHINA hapa nchini, BI WANG KE, amempongeza Mwenyekiti wa kampuni hiyo ya CNBM, SONG ZHIPING, kwa kuanzisha kituo hicho.

#SIBUKAMEDIA

Comments

comments