Waziri wa mambo ya ndani ya Nchi MWIGULU NCHEMBA amewataka wananchi kuwa na imani na vyombo vya usalama

usalama

Waziri wa mambo ya ndani ya Nchi MWIGULU NCHEMBA amewataka wananchi nchini kuendelea kuwa na imani kubwa na vyombo vya usalama katika kulinda raia na mali zao.

Waziri MWIGULU amesema hayo mkoani SINGIDA na kusisitiza kuwa kama yeye ndiye aliyepewa dhamana ya usalama wa raia na mali zao katika wizara ya mambo ya ndani hapatatokea hata kitongoji kimoja kitaonekana kimeshindikana ndani ya nchi hii.

Aidha waziri MWIGULU amesema kuwa hata watu wanaoshambulia watu watashughulika nao mmoja mmoja hasa waliobeba jina la watu wasiojulikana kwahiyo wananchi waendelee kuliamini jeshi la polisi nchini wakati huu ambapo wanaendelea na kazi ya upelelezi wa kuwakamata watu wote waliohusika na shambulio kwa mbunge TUNDU LISU.

Akizungumzia suala la vyombo vya nje kufanya uchunguzi nchini,Waziri MWIGULU ameongeza kuwa Tanzania ni nchi huru inajitegemea hivyo upelelezi utafanywa na  watakamatwa na vyombo vyetu na kufikishwa katika vyombo vya sheria.

  • #SIBUKAMEDIA

Comments

comments