Waziri wa Habari,Sanaa,Utamaduni na Michezo DKT.HARRISON MWAKYEMBE, amewashukuru watanzania wote kwa ushirikiano na upendo waliouonyesha

Waziri wa Habari,Sanaa,Utamaduni na Michezo DKT.HARRISON MWAKYEMBE  amewashukuru watanzania wote kwa ushirikiano na upendo waliouonyesha wakati wa msiba wa mke wake marehemu LINAH MWAKYEMBE.

Akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake  jijini DAR ES SALAAM,Waziri amesema anatambua mchango wa kila mmoja aliyeshiriki kuanzia ugonjwa na hata mazishi ya mke wake.

Amesema familia inapenda kutoa shukrani za pekee kwa Rais DKT.JOHN POMBE MAGUFULI,Waziri Mkuu KASSIM MAJALIWA,Makamu wa Rais SAMIA HASSAN SULUHU,Spika wa Bunge JOB NDUGAI,wabunge,mawaziri,wakuu wa mikoa na wilaya wote walioguswa na msiba huo.

Aidha Waziri DKT.MWAKYEMBE amewashukuru madaktari na wakazi wa mkoa wa MBEYA hasa wilaya ya KYELA kwa ushirikiano wao na kusisitiza kuwa mungu pekee atawalipa kwa namna walivyojitoa kumfariji wakati wa ugonjwa mpaka msiba.

Marehemu LINAH GEORGE MWAKYEMBE alifariki dunia  tarehe 15 Julai mwaka huu katika hospitali ya AGHA KHAN baada ya kuugua kwa muda mrefu,na amezikwa wilayani KYELA,Mkoani MBEYA tarehe 19 Julai,2017.

 

Comments

comments