Waziri wa Habari Utamaduni,Sanaa na Michezo BW.NAPE NNAUYE na Naibu Waziri wa Jamhuri ya watu wa CHINA BW.DONG WEI

IMG-20170323-WA0000

Waziri wa Habari Utamaduni,Sanaa na Michezo BW.NAPE NNAUYE na Naibu Waziri  wa Jamhuri ya Watu wa CHINA BW.DONG WEI wamesaini mkataba wa makubaliano katika program ya utekelezaji katika masuala ya Utamaduni.

Akizungumza jijini DAR ES SALAAM  mara baada ya makubaliano hayo ya kiserikali waziri nape amesema atasimamia na kuhakikisha nchi hizo mbili zinadumu katika kushirikiana kukuza uchumi wa Taifa kupitia Utamaduni.

Akizungumza baada ya kutia saini Naibu Waziri wa Utamaduni wa CHINA BW.WEL amesema kuwa serikali ya CHINA imekusudia kutoa fedha kiasi cha YUAN 4000 kwa ajili ya vifaa vya ofisini na kuwa mwaka huu imekusudia kuwaalika watanzania kwenda mafunzoni china ili kupata mafunzo ya kung fuu.

Aidha BW.WEI ameongeza kuwa mbali na masuala ya utamaduni CHINA itahakikisha inashirikiana vema  na TANZANIA ili kukuza na kuendeleza sekta ya viwanda na uchumi.

#SIBUKAMEDIA

Comments

comments