Waziri Ndalichako Amezindua Mfuko wa Bodi ya Mamlaka ya Elimu Tanzania

vlcsnap-2017-03-07-15h29m45s773

Waziri wa elimu sayansi,teknolojia na mafunzo ya ufundi Profesa Joyce Ndalichako amezindua bodi ya mfuko wa mamlaka ya elimu nchini ambayo jukumu lake ni kusimamia na kuhakikisha miradi yote kupitia wizara ya elimu inatekelezwa vema.

vlcsnap-2017-03-07-15h33m21s436

 Akizindua bodi hiyo ya usimamizi mapema leo jijini Dar es salaam  Ndalichako amesema kuwa changamoto kubwa inayowakabili  mamlaka ya elimu ni utekelezaji hafifu  wa miradi ambayo fedha zake  hazikuweza kufanya kazi kwa mwaka wa fedha 2013-2014 na  2015 ambapo jumla ya miradi 59 haijatekelezwa.

vlcsnap-2017-03-07-15h35m59s365

 Waziri Ndalichako amefafanua kuwa jumla ya fedha zote za mradi  ambazo zinapaswa kufanya kazi hiyo ni  bilioni 29 bilioni 827 na kuwaasa kuacha kubeba jukumu lote wenyewena badala yake wafanye mgawanyo wa majukumu ili kurahisisha mchakato katika miradi.

vlcsnap-2017-03-07-15h33m57s039

Amemwagiza kaimu mkurugenzi mamlaka ya elimu Bi.Graceana Shirima kuhakikisha fedha za miradi yote iliyoombwa kutoka hazina inaanza kutekelezwa hadi kufikia tarehe thelasini ya mwezi wa sita mwaPrka 2017.

vlcsnap-2017-03-07-15h34m50s445

 Ameongeza kuwa ni muhimu kuanza ujenzi wa miradi  ya nyumba za walimu na mabweni ya wanafunzi mapema kwakuwa wamekuwa wakisababisha mkwamo .

 Nae mwenyekiti wa bodi ya mamlaka ya elimu Tanzania Profesa Maurice Mbago ametoa shukrani kwa Rais wa jamuhuri wa muungano Tanzania kwa kumteua mwaka 2016 na kusema  kuwa bodi hiyo itafanya kazi kwa weledi kwakuwa jukumu kubwa lililopo ni kusimamia sera mikakati mbalimbali ya kitaifa katika kuhakikisha utawala bora nchini.

Imeandaliwa na Tuse Kasambala

#SIBUKAMEDIA

Comments

comments

Random Posts