Waziri mkuu wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa afungua kongamano la uwekezaji kati ya China na Tanzania

Waziri mkuu wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa afungua kongamano la uwekezaji kati ya China na Tanzania

Waziri mkuu wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa amefungua na kushiriki kwenye kongamano la uwekezaji kati ya China na Tanzania mjini Beijing China na kutumia fursa hiyo kukutana na wakuu wa makampuni mbalimbali, ambayo yana ushirikiano na Tanzania, na yale ambayo yanatafuta fursa za uwekezaji nchi Tanzania.

Waziri Mkuu amesema uhusiano mzuri wa kidiplomasia kati ya China na Tanzania ni msingi mzuri wa ushirikiano wa kiuchumi kati ya pande mbili. Waziri Mkuu Majaliwa amesema,

“Tanzania na China ni marafiki wa kweli, na tunashirikiana katika maeneo mbalimbali ya kikanda na ya kimataifa, lakini tunabadilishana uzoefu kupitia ziara za viongozi wan chi zetu hizi mbili na tumekuwa tukiimari sha mahusiano yetu mazuri yaliyopo na imekuwa chachu ya mahusiano kati ya serikali hizi mbili. Tanzania ina fursa nyingi za uwekezaji kwa wawekezaji kutoka China, tumeandaa mazingira mazuri ya uwekezaji wa kibiashara utulivu wa kisiasa kiuchumi na serikali wezeshi ba kwenu wachina tumewapa nafasi ya mbele kabisa. Mabibi na mabwana nikiwa nahitimisha napenda kutumia fursa hii kuwafahamisha kuwa kama unataka kuwekeza Afrika wekeza Tanzania, nawakaribisha kuja kuwekeza Tanzania karibu sana Tanzania Xie Xie .”

Mh Waziri mkuu Bw Majaliwa yuko hapa Beijing kuhudhuria mkutano wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika utakaanza kesho, na amekuja hapa China akiongoza ujumbe mkubwa wa mawaziri na maofisa waandamizi kutoka kituo cha uwekezaji cha Tanzania TIC, kituo cha uwekezaji Tanzania EPZ, na maofisa kutoka serikali ya mapinduzi ya Zanzibar na wa serikali ya Jamhhuri ya Muungano.

Comments

comments