Waziri mkuu Kassim Majaliwa, Makamu wa Rais Kuhamia Mkoani Dodoma.

majaliwa

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,MAJALIWA KASSIM MAJALIWA amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,DKT.JOHN POMBE MAGUFULI anatarajia kuhami makao makuu ya nchi DODOMA wakati wowote kutoka sasa huku makamu wa Rais Mama SAMIA SULUHU HASSAN akitarajiwa kuhamia mwishoni mwa mwaka huu na si 2020 kama ilivyotangazwa.

Hayo yamesemwa leo na Waziri Mkuu wakati wa uzinduzi wa ofisi za Umoja wa Mataifa DODOMA ambapo amesema hadi sasa watumishi 2,346 kutoka wizara zote wakiwemo mawaziri, makatibu wakuu na wakurugenzi wameshahamia DODOMA.

Rais MAGUFULI alitangaza kuhamia Dodoma  katika sikukuu za mashujaa zilizofanyika kitaifa kwa mara ya kwanza mjini humo mwaka 2016 tangu nchi ipate uhuru ambapo uamuzi huo ulipokewa na Waziri Mkuu MAJALIWA aliyetangaza ratiba ya uhamiaji wa Serikali katika kipindi cha miaka mitano baada ya yeye mwenyewe kuhamia Septemba Mosi, 2016.

Kwa mujibu wa waziri mkuu awamu ya kwanza iliyomhusisha yeye mwenyewe, mawaziri wote, makatibu wakuu, naibu makatibu wakuu wote na angalau idara moja au mbili ilianza Septemba 2016 hadi Februari 2017.

Awamu ya pili ilikuwa kati ya Machi 2017 hadi Agosti 2017 ambayo iliwahusisha watendaji wa wizara mbalimbali  na awamu ya tatu ilianza Septemba 2017 hadi Februari 2018 na ya nne Machi 2018 na Agosti 2018.

Waziri mkuu amesema  awamu ya tano ambayo ni Septemba 2018 hadi Februari 2020 itakuwa kuhamisha watumishi wa wizara waliobakia jijini Dar es Salaam na ya sita itakuwa ni kati ya Machi 2020 hadi Juni 2020 ambapo Ofisi ya Rais ikiongozwa na Rais, Makamu wa Rais watahamia Dodoma.

  • #SIBUKAMEDIA

 

Comments

comments