WAZIRI MKUU AZINDUA SAFARI ZA NDEGE ZA ATCL KWENDA DODOMA.

download (3)

Waziri mkuu Kassim Majaliwa Jana amezindua rasmi safari ya kwanza ya ndege Air Tanzania Bombadier Q400 kwenda mkoani Dodoma na kuwa miongoni mwa abiria waliosafiri na ndege hiyo.
Akizungumza kabla ya kuanza safari Majaliwa amesema uwepo wa ndege hiyo ni fursa pekee kwa wabunge,wafanyabiashara na wananchi kuitumia kwa ajili ya safari zao.
Ndege hiyo iliruka kwenye uwanja wa Julius Nyerere alfajiri ikiwa na abiria79 ambayo itafanya safari zake siku mbili kwa wiki kuelekea Dodoma ambapo nauli ya mwanzo itakuwa ni shilingi 165,000 tu za kitanzania.

#Sibukamedia

Comments

comments