waweza:Utafiti waeleza umaarufu wa Rais Magufuli, vyama vya upinzani washuka

Utafiti uliofanywa na taasisi ya utafiti isiyo ya kiserikali Twaweza umebaini kuwa umaarufu wa Rais wa Tanzania, Dokta John Magufuli umeshuka kutoka asilimia 96 mwaka 2016 hadi kufikia asilimia 55 mwaka huu.

Asilimia 55 ya wananchi wanaukubali utendaji wa Rais Magufuli tangu alipoingia madarakani mwaka 2015. Kukubalika huku kumepungua kutoka 96% mwaka 2016, na 71% mwaka 2017.

Kiwango cha kukubalika kwa Rais kimeshuka kutoka kwenye rekodi ya juu kuwahi kuwekwa na Rais wa Tanzania mpaka rekodi ya chini tangu takwimu hizi zianze kukusanywa mwaka 2001.

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Freeman Mbowe amesema”umashuhuri wa Rais unaposhuka chini unaakisi kuwa hali ya maisha ya wananchi inazidi kuwa ngumu, umasikini, elimu , huduma za kijamii, changamoto za uwekezaji na wafanyabiashara kufunga biashara zao”.

Wakati huo huo serikali imekanusha dhana kwamba umaarufu wa Rais John Pombe Magufuli unapungua kama taasisi hiyo ya kiserikali inayojihusisha na utafiti nchini humo ya Twaweza inavyodai kwenye ripoti yake.

Katibu wa itikadi na uenezi wa Chama cha Mapinduzi CCM Bwana Humphery PolePole amesema Rais Magufuli bado ni maarufu sana nchini Tanzania kutoka na sera zake.Hasa katika uboreshaji katika masuala kama elimu, afya na miundombinu ya barabara na umeme.

Twaweza: Watanzania ‘hawako tayari kuandamana’

Vyama vya siasa

Utafiti huu umebaini kuwa karibu wananchi wote wanafahamu vyama vikuu vitatu vya siasa nchini ambavyo ni CCM (100%), Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) (97%) na Chama cha Wananchi (CUF) (83%).

Umaarufu wa vyama vingine miongoni mwa wananchi ni mdogo sana. Miongoni mwa vyama vingine, National Convention for Construction and Reform (NCCR Mageuzi) (54%) kinajulikana zaidi, kikifuatiwa na Tanzania Labour Party (TLP) (41%) na ACT-Wazalendo (32%). Jamii kwa ujumla inavifahamu vyama vikubwa vya siasa. Kwa upande wa vyama vidogo

vinafahamika zaidi miongoni mwa wanaume, vijana, wananchi wenye uwezo wa kifedha na wakazi wa maeneo ya mijini.

”Namna ambavyo vyama mbadala vimekuwa vikitendewa kama vile kukamatwa, kumewafanya watu wawe na hofu na kurudi nyuma, wachache wanajiamini kuonyesha msimamo kuhusu chama wanachokifuata”.Alisema Mbowe

Japokuwa Chadema, CUF, ACT na NCCR Mageuzi vinafanya kazi kwenye mazingira magumu, vinapaswa kujiuliza kwa nini viwango vya kukubalika kwa viongozi waliochaguliwa vimeshuka. Zaidi, kwa nini vyama

hivi vinahangaikakutafuta kuungwa mkono kwenye maeneo ya mijini, ambayo tayari wanaungwa mkono? ”Ikiwa vyama hivi vimejikita zaidi kwenye masuala ya kisiasa, labda ni wakati mwafaka sasa wa

kuangaliauwezekano wa kushughulikia wasiwasi wa wananchi kuhusu hali zao za kiuchumi” imeeleza ripoti hiyo.

Comments

comments