Wavulana 4 zaidi waliokwama pangoni Thailand ‘waokolewa’

 

Wapigaji mbizi kaskazini mwa Thailand wamewaokoa wavulana wanne zaidi kutoka pango lililofurika maji.

Hii inaashiria kuwa kwa jumla, wavulana 8 wameokolewa salama huku watu watano wakiwa bado wamesalia ndani ya pango.

Vijana hao 12 na kocha wao wa soka walikwama ndani ya pango tangu Juni 23 baada ya mvua kubwa kusababihsa mafuriko.

Wanajeshi wa majini wa Thailand wanaoongoza operesheni hiyo wamethibitisha kuwa jumla ya wavulana 8 wameokoloewa salama.

Wavulana 4 waliokolewa salama kutoka pangoni siku ya Jumapili.

Lakini operasheni hiyo ilisitishwa usiku ili mitungi ya hewa ya kusaidia kupumua ipate kujazwa.

Wakoaji waliamua kuendelea na oparesheni hiyo hatari kuwaokoa kufuatia hofu kuwa huenda maji yangeongezeka tena.

Mamilioni ya lita za maji yamekwisha kutolewa kutoka ndani ya pango hilo,ili kurahisisha kazi ya uokoaji.

Kazi hiyo inaharakishwa kufuatia utabiri wa hali ya hewa unaodai kwamba huenda mvua kubwa itanyesha jambo ambalo litasababisha ugumu wa kazi ya kuwaokoa watoto hao.

Kiongozi wa kikosi cha uokoaji ambaye gavana wa jimbo la Chang Raiu Narongsak Osottanakorn, amesema uokoaji huo wenye mazingira ya hatari utawachukua takribani siku nne kutegemeana na hali ya hewa, japo kuwa jana kwamba amesisitiza kila kitu kinaenda sawa.

Maafisa wa huduma za dharura

Comments

comments