Wauguzi na wakunga kuombwa kufatilia makongamano ya Kisayansi.

Wakunga

Chama cha Wakunga Tanzania, kimewaomba wakunga na wauguzi nchini kufuatilia makongamano mbalimbali ya kisayansi yanayowahusu ili waweze kujifunza .

Hayo yamebainishwa jijini DAR ES SALAAM na Kaimu Mkurugenzi Huduma za Kiuguzi BW.ROBERT ALOYCE wakati wa maadhimisho ya siku ya wakunga katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Amesema wakunga wote wanapaswa kujenga desturi ya kupenda utafiti ili kujijengea heshima kama wanataaluma na kuongeza kuwa  kusoma kutaboresha huduma wanazozitoa na kusaidia kupunguza vifo vya kina mama wajawazito na watoto wakati wa kujifungua.

  • #SIBUKAMEDIA

Comments

comments

Random Posts