Watu walio na vitambi wako hatarini kupata magonjwa ya Kisukari pamoja na shinikizo la damu.

Kwa mujibu wa uchunguzi wa kitaalamu Imeelezwa kuwa watu walio na vitambi wako hatarini kupata magonjwa ya Kisukari pamoja na shinikizo la damu.

Kauli hiyo imetolewa na Afisa lishe Wilaya ya Mkalama Bi Eliwandisha Kinyau alipokuwa akizungumza na sibuka fm wakati wa kupima hali za lishe kwa watumishi wa Wilaya hiyo.

Bi Eliwandisha amesema kuwa kinachosababisha kupata kitambi ni mrundikano wa mafuta tumboni ambayo yanaweza kupanda mpaka kwenye moyo na kusababisha damu kupita kwa shida hali inayopelekea shinikizo la damu.

Aidha amesema kuwa ili kuepusha hatari hiyo watu wanatakiwa kutumia vyakula vilivyo katika makundi matano vikiwemo vyakula vya protini wanga na nishati ambapo vinatakiwa kuliwa kwa kiasi kwa kila kundi moja.

Hata hivyo ametoa wito kwa Wananchi kupenda kupima afya zao hususani hali yao ya lishe ili kuweza kuepukana na maradhi mbalimbali.

  • Mwandishi : Saulo Steven
  • #SIBUKAMEDIA

Comments

comments