Watu kumi na moja washikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kuhusika katika mauaji ya kikatili

Jeshi la polisi

Jeshi la polisi mkoa wa Dodoma linawashikilia watu kumi na moja kwa tuhuma za kuhusika katika mauaji ya kikatili kwa kumchinja mwanamke mmoja katika kitongoji cha changombe katika wilaya chamwino mkoa wa Dodoma.

Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma LAZARO MAMBOSASA amesema mauaji hayo yametekelezwa katika nyumba ya mganga wa jadi ASHURA MKASANGA katika kitongoji changombe.

Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma lazaro mambo sasa mbele ya waandishi wa habari anabainisha kuwa mnamo tarehe 08/08/2017 majira ya 04:00  usiku katika Kitongoji cha CHANG’OMBE, kijiji cha CHAMWINO – IKULU, MARIAM SAIDI, miaka 17, mkazi wa KIGOMA, ameuwawa kwa kukatwa shingo yake na kutenganishwa na kiwiliwili na kuchoma moto kichwa.

Kamanda MAMBO SASA ametoa wito kwa wakazi wa wilaya ya chamwino kushirikiana na jeshi la polisi kuwafichua waliohusika kutekeleza tukio hilo.

katika tukio jingine kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma lazaro mambo sasa amesema mmtu mmoja amefariki dunia kwa kufukiwa na kifusi katika machimbo ya mchanga katika eneo la ntyuka katika manispaa ya Dodoma.

Aidha ameishauri idara ya Madini na Mazingira kufanya ukaguzi katika machimbo ya mchanga na vifusi pamoja na kutoa elimu kwa wachimbaji ya kujihami katika kazi zao.

  • Mwandishi : Barnaba Kisengi
  • #SIBUKAMEDIA

 

Comments

comments