Watu 17 wamenusurika kufa ziwa VICTORIA baada ya boti waliokuwa wakisafiria kuzama ziwa VICTORIA.

BOTI

Watu 17 wamenusurika kufa ziwa VICTORIA baada ya boti waliokuwa wakisafiria kuzama ziwa VICTORIA.

Boti hiyo MV JULIUS iliyokuwa inasafiri kutoka kisiwa kimoja kuelekea jijini MWANZA imezama Ziwa VICTORIA ikiwa imebeba watu na mzigo wa magunia ya dagaa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa KAGERA, AUGUSTINE OLLOMI amesema kuwa watu wote waliokuwa kwenye boti hiyo wameokolewa na wako salama.

Kamanda OLLOMI amewaambia waandishi wa habari kuwa  chanzo cha boti hiyo iliyokuwa na gunia 250 za dagaa kuzama ni hitilafu iliyotokea muda mfupi baada ya kuanza safari na kusabanisha iegemee upande mmoja.

Note : Picha Iliyotumika Katika habari hii ni Mfano.

  • #SIBUKAMEDIA

Comments

comments