Watu 12 wamefikishwa mahakamani nchini UGANDA kwa mashtaka ya mauaji ya wanawake tisa katika eneo la kaskazini nje ya mji mkuu KAMPALA.

UGANDA

Watu 12 wamefikishwa mahakamani nchini UGANDA kwa mashtaka ya mauaji ya wanawake tisa katika eneo la kaskazini nje ya mji mkuu KAMPALA.

Watu hao wakiwemo wanawake wawili kwa pamoja wanashtakiwa kwa makosa ya ugaidi na wizi wa kutumia nguvu.

Jumla ya wanawake 19 wameuawa katika maeneo ya mji wa KAMPALA tangu mwezi Mei wengi kati yao walikuwa wamebakwa na kukatwa viungo vyao, huku miili yao ikiachwa porini na pembezoni mwa barabara.

Mkuu wa polisi nchini UGANDA amesema imani za kishirikina zinahusishwa katika baadhi ya mauaji.

  • #SIBUKAMEDIA

Comments

comments