Watanzania wameshauriwa kuliombea Taifa la KENYA ili uchaguzi huo upite kwa amani na utulivu.

KENYA

Siku moja kabla ya wakenya kupiga kura nchini humo watanzania wameshauriwa kuliombea Taifa hilo ili uchguzi huo upite kwa amani na utulivu.

Baadhi ya watanzania akiwemo diwani mstaafu wa kata ya RABUOR wilaya ya RORYA, BW. YAMO ODEMBA amesema KENYA na TANZANIA ni nchi jirani hivyo machafuko yakitokea nchini KENYA yanaweza kuleta madhara TANZANIA pia.

Naye mkuu wa wilaya ya LUDEWA, BW. ANDREA TSERE amewaomba watanzania kuendelea kuliombea taifa la KENYA ili uchaguzi wao ifanyike kwa amani na haki ili kuepuka macahafuko kama yaliyotokea mwaka 2007.

Hata hivyo BW. DAVID KAGOSE ambaye ni mkazi wa MBAGALA RANGI TATU amewaomba wananchi wa KENYA kutojiusisha na udanganyifu wa Aina yoyote badala yake wamuombe mungu awape amani nchini kwao.

Kesho wananchi wa KENYA watapiga kura kwa ajili ya kuwachagua viongozi mbalimbali ambapo mchuano mkali ni kati ya Rais wa sasa UHURU KENYATTA kutoka chama cha JUBILEE  na BW.RAILA ODINGA KUTOKA MUUNGANO WA NASA ambae anagombea nafasi hiyo kwa mara ya tatu sasa.

  • #SIBUKAMEDIA

Comments

comments

Random Posts