Watanzania wamejitokez Kwa Wingi Bandaniri Kupima afya zao.

Mkuu wa Mkoa

Wakazi mbalimbali kutoka ndani ya jiji la DAR ES SALAAM na mikoa jirani wamejitokeza kwa wingi bandarini kwa ajili ya kupatiwa matibabu na madaktari bingwa wa magonjwa mbalimbali kutoka nchini CHINA.

Radio sibuka fm wamefika eneo hilo na kushuhudia umati mkubwa wa wananchi wenye matatizo mbalimbali ya kiafya wamefika kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Meli hiyo ya  jeshi la majini kutoka China (Navy) imeingia nchini ili kutoa matibabu ya bure kwa  siku tano kuanzia leohadi Ijumaa Novemba 24 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari ,Mkuu wa Mkoa wa DAR ES SALAAM,PAUL MAKONDA amewataka wananchi kuondoa hofu kwani kila mmoja atapatiwa matibabu na dawa anazostahili ili kumaliza tatizo alilokuwa nalo.

Makonda amewataka Watanzania kufika kwenye meli hiyo waweze kunufaika na matibabu ya bure hasa wale wanaosumbuliwa na magonjwa sugu, yenye kuwaletea matatizo kila mara na mengine yanayowasibu.

#SIBUKAMEDIA


 

 

 

Comments

comments