Watanzania waishio nje ya nchi wakaribishwa kuwekeza nchini mwao

Image captionWatanzania waishio nje ya nchi maarufu kiwanda cha mafuta cha makonyo

Serikali ya Tanzania imeendelea kufungua milango kwa Watanzania waishio nje ya nchi maarufu kama DIASPORA kuja nchini kuwekeza katika juhudi za kuliletea maendeleo taifa.

Katika Kongamano la tano la Diaspora mwaka huu lililofanyika mwishoni mwa wiki na kufunguliwa na Rais wa Zanzibar Dokta Ali Mohamed Shein na kufungwa na Makamu wa pili wa Rais wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar Seif Ali Idd, viongozi hao wamesema kila mmoja ana jukumu la kuijenga nchi yake kwa kutumia nafasi na uwezo wake.

Rais wa Zanzibar amesema serikali inathamini michango wanayoendelea kuitoa kwa nchi katika sekta mbakimbali ikiwemo elimu na afya kwa kuchangia vifaa na ujenzi wa miundo mbinu pamoja na huduma.

Ameongeza kuwa panapotokea changamoto ni njema kuzitatua pamoja kutokana na kwamba mafanikio na changamoto ni za wote pamoja, na kuongeza kuwa kila mmoja ajihisi kuwa anajukumu lililo sawa kuijenga nchi kwa nafasi yake na uwezo alionao, kiuchumi na taaluma.

Kwa upande wake Makamu wa Pili wa Rais wa serikali ya mapinduzi Zanzibar Dokta seif Ali Idd amewataka wana diapora kufuatilia masuala yanayojiri ndani ya nchi yao ili kuweza kufahamu hatua mbalimbali za maendeleo ya nchi na kuweza kufaidika na kutumia fursa mbalimbali za kiuchumi zilizopo na zitakazo ibuka baadaye

Pemba
Image captionWatanzania waishio nje ya nchi maarufu kiwanda cha mafuta huko kisiwani Pemba

Wakizungumzia changamoto zao wana Diaspora kwa upande wao walielezea changamoto na yale ya moyoni wamesema kuna urasimu unaosababisha utendaji wa serikali kuwa taratibu hali inayowafanya kukata tamaa.

Vitu vingine vinavyolalamikiwa ni pamoja na sheria za ardhi.

Lakini hata hivyo wapo wanaoamini kwamba hali itabadilika taratibu, pale pande zote mbili zikielewana.

Kwa mujibu wa takwimu za serikali wana Diaspora huchangia kiasi cha shilingi trilioni moja kwa mwaka.

Katika kongamano hilo la tano la Diaspora Tanzania, mbali na washiriki kupata elimu ya masuala ya uhamiaji lakini pia walipata fursa tya kutembelea maeneo ya utalii, viwanda na hospitali, kama juhudi za serikali kuwahamasisha, kuhakikisha kwamba wanakuza uchumi wa nchi.

Comments

comments