Wasomi kote nchini wameombwa kuisadia jamii na serikali katika kupunguza changamoto

Wasomi kote nchini wameombwa kuisadia jamii na serikali katika kupunguza changamoto zinazoikabili jamii kwa kutumia teknolojia ili kupiga hatua kimaendeleo.

Wahitimu wa Chuo Kikuu cha MT.JOSEPH, BW.FRED CHACHA na CHARLES RUTA wameyasema hayo leo wakati wakitambulisha mfumo wa ukataji tiketi kwa njia ya kielektroniki hapa nchini na kusema kuwa ikiwa wasomi watajitoa katika kuisaidia serikali na jamii maendeleo yatapatikana kwa kasi pamoja na ukuaji wa uchumi.

Wakizungumzia faida zitakazopatikana kutokana na matumizi ya mfumo huo wamesema ni kuongeza mapato ya serikali,kupunguza usumbufu kwa abiria ikiwa ni pamoja na wamiliki wa vyombo vya usafiri kujua idadi ya abiria waliopo ndani ya vyombo hivyo.

  • #SIBUKAMEDIA

Comments

comments