Washindi wa Shindano la TIGO la Rich for change Maker Wakabidhiwa Zawadi ya Dollar 20 Elfu.

tgo 1 (1)

Wajasiriamali wadogo wameombwa kuendelea kushiriki katika shindano la Rich of change makers ili kupanua wigo wa biashara  na uchumi ili kujikwamua na umasikini.

Wito huo umetolewa mapema leo jijini Dar es salaam na mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Tigo (T) Limited Bw. Diego Muterez wakati akikabidhi hundi kwa washindi wa shindano hilo na kuongeza kuwa mpaka sasa kampuni yake jumla ya wajasiriamari nane ambao wameweza kuwafikia watoto 250 Tanzania nzima.

tgo 1 (3)

Mapema wakizungumza na washindi wa shindano hilo mrembo wa Tanzania 2005 Nancy Sumari na Sophia Mbega wameishukuru kampuni ya tigo kwa kuendesha shindano hilo na kuongeza kuwa kupitia fedha walizopata watawasaidia vijana wengi wa kitanzania ili waweze kutimiza ndoto zao.

 tgo 1 (2)

Washindi hao wamezawadiwa hundi ya dola za kimarekani 20,000 kila mmoja pamoja na kupatiwa ushari wa kitaalam kutoka kampuni ya tigo

Imeandaliwa na Stanley Burushi

#SIBUKAMEDIA

 

Comments

comments