Wanawake takribani milioni 214 waishio katika mazingira hatarishi kutoka nchi zinazoendelea duniani wanakadiriwa kukosa njia bora za uzazi wa mpango.

DAR ES SALAAM

223bdf73-71f5-4f5f-ba62-a4fb5b79560d

Wanawake takribani milioni 214 waishio katika mazingira hatarishi kutoka nchi zinazoendelea  duniani wanakadiriwa kukosa njia bora  za uzazi wa mpango.

Kaimu Mwakilishi  Mkazi  wa Shirika la umoja wa mataifa la idadi ya watu (UNFPA) Dr. Hashina Begum amewaambia waandishi wa habari jijini DAR ES SALAAM kuwa jumla ya wanawake kutoka mataifa 69 duniani wamekuwa wakikosa fursa ya afya ya uzazi.

 Dr.Begum amebainisha kuwa ili kukuza uchumi na kuleta maendeleo duniani ni lazima kukabiliana na changamoto hiyo inayowakumba zaidi wanawake  masikini pamoja na wakimbizi.

 Aidha Dr. Begum amesema kuwa ni vema jamii kutoa fursa kwa wanawake kupewa elimu hasa ya afya ya uzazi wa mpango kwakuwa wanawake wanaotumia njia ya uzazi wa mpango wanapunguza vifo kwa asilimia 30 na kwa watoto kwa asilimia 12 katika utekelezaji wa lengo la UNFPA ifikapo mwaka 2030.

 Nae Dr. Cosmas Swai kutoka wizara ya Afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto amesema kuwa wizara ya afya kwa kushirikiana na UNFPA na wadau wengine wa afya wamejipanga vema katika maadhimisho ya siku ya idadi ya watu duniani ambayo Itafanyika tarehe 11 -12julai,2017 katika viwanja vya Mwembe yanga ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa  Naibu Waziri wa Afya Dk.Khamis Kigwangala.

 Kwa upande wake Afisa mawasiliano na utetezi kutoka Chama cha uzazi na malezi bora Tanzania (UMATI) Bi Josephine Mugishagwe ameitaka jamii kujitokeza ili kupata huduma za upimaji wa hiari wa VVU,matumizi sahihi ya kondom, Afya ya saratani ya shingo  ya uzazi,Huduma ya uzazi wa mpango ambazo zitatolewa bure.

kk

 Kaulimbiu ya mwaka 2017 ya maadhimisho ya siku ya kimataifa ya idadi ya watu duniani ni “Uzazi wa Mpango kuwezesha watu na kuendeleza Mataifa

#imeandaliwa na Tuse Kasambala

#sibuka media

Comments

comments